Mwanaume haruhusiwi kufanya jambo hili

Habari wadau, moja kwa moja kwenye mada, kuna mambo mengi ambayo mwanaume haruhusiwi kufanya kutokana na taratibu za kabila, dini, familia, maumbile au jamii aliyopo.

Moja kati ya mambo ambayo hayaruhusiwi ni kulala bila nguo (yaani kama alivyozaliwa) hata baada ya kushiriki tendo na mwenza wake. Hii ni kwasababu ya vitu mbalimbali;

1. Mwanaume anapaswa kuwa mlinzi wa familia hivyo chochote kitakachotokea ambacho kinahatarisha usalama wa familia anapaswa kuwa wakwanza kutoka ili kuangalia au kubambana. Hivyo anapaswa kuwa tayari nyakati zote kwani anaweza asiwe na muda wa kujisitiri.

2. Kunapotokea hatari kwa jirani mfano hatari ya moto au kuvamiwa na mnyama mwanaume anapaswa kujumuika na wenzake ili kupambana katika kuzima moto au kumpambana na myama huyo hivyo anapaswa kuwa tayari.

3. Aibu aliyonayo mwanaume humfanya asiwe na amani ya kulala bila nguo (hata na boxer tu).

Mdau unadhani mambo gani mengine ambayo mwanaume haruhusiwi/ hapaswi kufanya kwa mtazamo wako?

Wadada/wanawake muwe huru kuchangia.

Sent using Jamii Forums mobile app
kumtumia demu nauli ,
 
Mwanaume haruhusiwi kukaa ndani siku nzima (utadharaulika)....toka asubuhi urudi jioni hata kama hauna mchongo.
Dunia ya Leo sio 1970.
Hata kutoa pesa bank sio lazima uende bank ..

Kutoka nyumbani na kwenda kutafuta kunahitaji mipango,,, usione watu wanatoka tu majumbani,
Wenzio wana pa kwenda.,utawafuata huko wanapokwenda mwishowe kila mmoja anaingia ofisini,,wewe unabaki kutoa macho
 
Tofauti. Ya mwanaume na mwanamke ni za kimaumbile ya kimwili tu Ila kwingne tupo sawa kabisa
 
Dunia ya Leo sio 1970.
Hata kutoa pesa bank sio lazima uende bank ..

Kutoka nyumbani na kwenda kutafuta,
Yote ni mipango,, usione watu wanatoka tu majumbani,
Wenzio wana pa kwenda.,utawafuata huko wanapokwenda mwishowe kila mmoja anaingia ofisini,,wewe unabaki kutoa macho
😂🤣🤣 siku hizi watu wana-download pesa wakiwa kwenye shuka.
 
siku hizi watu wana-download pesa wakiwa kwenye shuka.
Mkuu hujuwi kama popote ulipo unaweza kufanya muamala wa kibank ?
Popote ulipo unaweza ukawa busy na marketing za online na ukapiga. Pesa?
Popote ulipo unaweza uka connect chochote na kupiga pesa?

Dunia ya Leo sio lazima mchakarikaji upaushe mashati mgogoni na kusaga viatu upande..
Kila kitu kipo kiganjani.

Kukaa ndani bila kutoka nje haimaanishi sio mtafutaji..

Sent from my M2101K7BG using JamiiForums mobile app
 
Dunia ya Leo sio 1970.
Hata kutoa pesa bank sio lazima uende bank ..

Kutoka nyumbani na kwenda kutafuta,
Yote ni mipango,, usione watu wanatoka tu majumbani,
Wenzio wana pa kwenda.,utawafuata huko wanapokwenda mwishowe kila mmoja anaingia ofisini,,wewe unabaki kutoa macho
kabisaaa
 
Tofauti. Ya mwanaume na mwanamke ni za kimaumbile ya kimwili tu Ila kwingne tupo sawa kabisa
Kama uko sawa na wanawake ni wewe peke yako.
Utakuwaje sawa na mtu anabadilisha mood bila sababu?
Utakuwaje sawa na mtu anaongea Kama redio.
Utakuwaje sawa na mtu mwenye hila, MTU ambae pesa zake ni zake, zako ni zenu?
Utakuwaje sawa na mtu unamnunulia iPhone lkn muda wote anawinda Infinix yako aone ikoje.
 
Back
Top Bottom