Mwanaume Halii

Mwanaume Halii

MWANAUME HALII

Wanaume wamefundishwa kuwa miamba, wasilie, wasilalamike, wasionyeshe uchungu. Lakini nyuma ya uso mgumu na sauti ya kujiamini, kuna wanaume wanaovunjika taratibu ndani kwa ndani.

Kuna mwanaume anayeamka kila siku kwenda kazini, akiwa hajalala usiku mzima kwa mawazo. Kuna mwanaume anayehangaika kutimiza majukumu, huku moyo wake umeelemewa na presha ya kutosikika, kutosaidiwa, na kutoeleweka.

Jamii inamwambia “kuwa jasiri,” lakini haimwambii wapi pa kulia na kusikilizwa Inamwambia “vumilia,” lakini haimpi nafasi ya kupumua. Matokeo yake, wanaume wengi wanakufa kimya, sio kwa risasi, bali kwa msongo wa mawazo, huzuni, na kukosa pa kusemea.

Afya ya akili ya kwa mwanaume sio udhaifu. Kuongea ni ujasiri. Kusema “nimeelemewa” si kushindwa, ni kuhitaji msaada. Dunia inahitaji wanaume waliopona ndani, si waliobeba mzigo wa siri hadi wakuvunjika.

Abuuabdillah ✍️
Sijasoma uzi wako ila mimi nasema MWANAUME HSLII HADHARANI (isipokuwa anapoumizwa ama kujeruhiwa mwilini)
 
Kuna njemba waliibana mlangoni wakati wa kugombea kuingia mwendokasi, ikawa inalia "mamaaaa".

Hayajakukuta tu.
 
Ndivyo tulivyo, hata kwenye nyakati ngumu tunatabasamu...

Hata panapo heka heka tunatulia kimya...

Cc: Mahondaw
 
Wakuu mimi inapobidi ntalia kilio kabisa, kitu ambacho siwezi kufanya ni kulalamika hicho tu ndio siwezi, ila kulia, aah! ikibidi ntalia tu wakuu. Kama naweza kucheka kwanini nisiweze kulia?.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom