Mwanaume Halii

Mwanaume Halii

Dr leader

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2016
Posts
1,041
Reaction score
1,294
MWANAUME HALII

Wanaume wamefundishwa kuwa miamba, wasilie, wasilalamike, wasionyeshe uchungu. Lakini nyuma ya uso mgumu na sauti ya kujiamini, kuna wanaume wanaovunjika taratibu ndani kwa ndani.

Kuna mwanaume anayeamka kila siku kwenda kazini, akiwa hajalala usiku mzima kwa mawazo. Kuna mwanaume anayehangaika kutimiza majukumu, huku moyo wake umeelemewa na presha ya kutosikika, kutosaidiwa, na kutoeleweka.

Jamii inamwambia “kuwa jasiri,” lakini haimwambii wapi pa kulia na kusikilizwa Inamwambia “vumilia,” lakini haimpi nafasi ya kupumua. Matokeo yake, wanaume wengi wanakufa kimya, sio kwa risasi, bali kwa msongo wa mawazo, huzuni, na kukosa pa kusemea.

Afya ya akili ya kwa mwanaume sio udhaifu. Kuongea ni ujasiri. Kusema “nimeelemewa” si kushindwa, ni kuhitaji msaada. Dunia inahitaji wanaume waliopona ndani, si waliobeba mzigo wa siri hadi wakuvunjika.

Abuuabdillah ✍️
 
Mwanaume hapaswi kulia, lakini pia mwanaume mwenye maamuzi hawezi akakubali kupitia hayo yote pasipo kuchukua hatua.
Alafu.....
Kwanza unazungumzia wanaume wa aina gani??
Maana nisije nikakubishia kumbe unazungumzia wanaume wapaka poda na kucha rangi...🤔
 
Mwanaume ni jinsia
 
MWANAUME HALII

Wanaume wamefundishwa kuwa miamba, wasilie, wasilalamike, wasionyeshe uchungu. Lakini nyuma ya uso mgumu na sauti ya kujiamini, kuna wanaume wanaovunjika taratibu ndani kwa ndani.

Kuna mwanaume anayeamka kila siku kwenda kazini, akiwa hajalala usiku mzima kwa mawazo. Kuna mwanaume anayehangaika kutimiza majukumu, huku moyo wake umeelemewa na presha ya kutosikika, kutosaidiwa, na kutoeleweka.

Jamii inamwambia “kuwa jasiri,” lakini haimwambii wapi pa kulia na kusikilizwa Inamwambia “vumilia,” lakini haimpi nafasi ya kupumua. Matokeo yake, wanaume wengi wanakufa kimya, sio kwa risasi, bali kwa msongo wa mawazo, huzuni, na kukosa pa kusemea.

Afya ya akili ya kwa mwanaume sio udhaifu. Kuongea ni ujasiri. Kusema “nimeelemewa” si kushindwa, ni kuhitaji msaada. Dunia inahitaji wanaume waliopona ndani, si waliobeba mzigo wa siri hadi wakuvunjika.

Abuuabdillah ✍️
Ni kweli. Ila analizwa kwa kuchunwa na kugeuzwa chawa wa mama
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom