Mwanaume hakutakiwa kuteseka kisa mapenzi, kutokujitambua na upumbavu ndio kunawafanya kuwa hivyo

Hakuna mjanja wa wajanja,

Kila mtu na mjanja wake..

Huyo anayekuliza wewe na yeye anamlilia mwingine..

Na huyo unayemlilia wewe mwingine anamuona dada wa kazi.

That's human nature.
 
By default wanadamu tulipoumbwa kila jinsia ilipewa majukumu yake, jukumu la viumbe wenye jinsia ya kiume (wanaume) wameumbwa kutawala jinisia ya kike (kike) katika kila Nyanja na jinsia ya kike imeumbwa kutawaliwa na jinisa me.

Sio maneno yangu bali ni maneno ya vitabu vyote vya dini Quran na bible pia science/psychology inakubaliana na hilo, mwanaume anajiona mkamilifu zaidi pale anapoweza kumtawala (sio kimabavu), kumuongoza na kumuhudumia mwanamke na mwanamke anajisikia amani na usalama zaidi anapopata mwanaume anayeweza kusimamia misingi ya uanaume wake yaani kutawala, kuongoza na kuhudumia .

Ikitokea jinsia moja imeenda kinyume na mfumo huo wa asili chaos must happen, labda mwanamke anapesa zake na maisha mazuri anataka afanye vile vitu anavyotakiwa kufanya mwanaume ajili ya kiburi cha pesa zake lazima mwanaume huyo kama anajitambua apinge (rebel) ajabu sasa mwanaume akiamua kuvumilia huyo mwanamke ajili ya pesa alizonazo mwanamke huyo atamdharau na kumuona fala sababu ameshindwa kusimama katika misingi ya kiume mahusiano hayo hayatadumu,that’s nature bwana.

Mwanaume umepewa dhamana kubwa duniani haijalishi mwanamke ana mapembe, mabawa, mkia, miiba au ana umri mkubwa na cheo zaidi yako bado atabaki kua mwanamke mtu na kanuni ni ileile atabaki kua chini yako daima, vijana wa sasa sijui mnafeli wapi aisee yaani mnadhalilisha jinisa na mamlaka yenu mbele ya wanawake.

Mwaume unayejielewa haiwezekani unalia, unashindwa kulia kisa mwanamke wako kakuzingua ni aibu mazee. Halafu wanawake wa sasa washajua wanaume wa sasa ni maboya tu hivyo wanakanyagia mafuta tu ya kuwaumiza maana washajua hamjui dhamana yenu duniani. Hivi unaanzaje kulia kisa mwanamke?

Wanaume tunapendwa sana na Mungu sijui hamjui au ni vipi hebu tembea mtaani, mitando ya kijamii uone wadada wazuri walivyojazana hao wote wameumbwa ajili ya mwaume awafaidi. Kwa hesabu za haraka duniani kuna watu zaidi ya bilioni 7 wanaume billion 3 na wanawake billion 4, yaani tukisema leo kila mwaume aoe mke mmoja mmoja kuna billion 1 ya wanawake itabaki haina kazi inapuyanga tu.

Logic
ya mungu kuumba wanawake wengi kuliko wanume ni kwamba kila mwaume apate uwanja mpana wa kuchagua mwanamke amtakae, pia kaumba wanawake wengi ili isije kutokea hata kwa bahati mbaya mwaume kuteseka kisa mapenzi/mwanamke.

Mungu anasikitika na kushangaa sana anapoona mwanaume analia na kuteseka kisa mwanamke mmoja wakati kashaumba wengi ni wewe kuchagua tu.

Mungu fundi sana yaani kaumba kikosi cha kwanza cha wanawake kisha akaumba Subs pia ili ikitokea uwanjani mmoja hakabi inavyopaswa basi anatolewa chap sub kutoka benchi anaingia kuendeleza kabumbu sasa wewe mwanaume unaona kabisa player uliyenaye analeta mazabe uwanjani badala ya kumuweka benchi uchukue sub wewe unabaki kulialia, walahi Mungu atawapa kipigo nyie maana mnashindwa kutumia raslimali zake ipasavyoo.

Halafu sasa wanawake hua wanapenda mwanaume mwenye wanawake wengi aua mwenyekuweza kupata mwanamke yoyote wakati wowote usipokua hivyo mwanamke anadharau anajiona keki anajua huna pengine pa kwenda. Hapo ndio utaona mwanaume anaomba msamaha kwa kosa alofanya mwanamke kisa asiachwe. Ngedere wewe

Wanaume achene ubwege wa kulialia kisa wanawake, simamieni misingi ya uanaume kenge nyie.​
Aisee hivi kumbe kuna wanaume wenzetu wanalialia kisa wanawake?. Something must be done!.

Sent from my 2201116TG using JamiiForums mobile app
 
Shaurini mtakavyoshauriana
Ila wamiliki wa *tamu ndo sie....

Msisahau alikuwepo Samson ila pia alikuwepo Delilahh..
Samsoni mzembe Sana,Adam ndio kabisaaaa. Mwanamke wa kunifanyia Mimi studentTeacher walichofanyiwa Adam na Samsoni hayupo na hatakuwepo. Nina nguvu ambazo zinawindwa kwa kutumia wanawake tena warembo lakini hola,ni miaka zaidi ya 15 sasa nazilinda kwa udi na uvumba. Mwanamke kujidanganya kutumia utamu wake kutaka kunipumbaza na kunipenyezea agenda zake nyeusi hilo kwangu hata Shetani anajua wazi limebuma!

Sent from my 2201116TG using JamiiForums mobile app
 
Halafu sasa wanawake hua wanapenda mwanaume mwenye wanawake wengi aua mwenyekuweza kupata mwanamke yoyote wakati wowote usipokua hivyo mwanamke anadharau...
Hapa ndo wanawake hushangaza sana 🙄 Kwamba akijua umeweka kambi kwake pekee, anakuona pimbi.
Wanapenda kila mwanaume awe polygamous!
 
Back
Top Bottom