mwanaume asiyetaka kuoa

mkonowapaka

JF-Expert Member
Feb 19, 2010
1,493
767
Habari JF..
Katika maisha kuna stages kadhaa hadi kufikia uzee kadri Mungu atakavyokupa maisha marefu...
Ivyo ni jukumu letu kama wanadamu kujipanga ili kuvuka kila steji..
Wazazi wamekua makini kuwasaidia vijana wao tangu kuzitafuta mimba zao;kuwazaa kuwalea na kuwasomesha...
Kwa wanaume unakuta kijana amesoma na amemaliza vzur stej zote na ana kazi nzuri...

Swali linakuja pale unakuta kijana amevuka miaka 30 na bado hajafikiria kuwa na mwenza wa maisha...kumekua na ongezeko kubwa sana la wanaume wasiotaka kuoa au akioa haoi kwa wakati muafaka...let's say anaoa kwenye 40's bila sababu zozote za msingi...hii inachangia kuja kuzaa wajukuu badala ya watoto;wanashindwa kutimiza majukum muhmu kwa watoto wao na ukizingatia magonjwa ya siku izi by 50 mzazi anaondoka...
Nawakumbusha vijana kujipanga mapema sio tu kikaz na kiuchumi bali pia na kifamilia...the earlier the better...
 
hata mimi nashangaa watu wanakazania watu kuoa, kama mtu unataka kupata mipresha ww jifanye kuoa mapema utakufa na kisukari/BP.

Ila ukiona unataka kuoa na uoe, ukiona hakuna umuhimu achana na hiyo habari gonga chapa lapa.
 
Jama kuoa ni lazima? Muache,kama hayuko tayari kuoa au hataki kuoa ni yeye,uwezi jua labda ni style yake ya maisha aliyoichagua.
 
kuoa siyo jambo la msingi. kupata mtoto ndio jambo la msingi ...........
MP.
 
1WAKORINTHO 7-38 MAANDIKO YANASEMA HIVI Kwa maneno mengine:yule anayeamua kuoa anafanya vema,naye anayeamua kutooa anafanya vema zaidi.
 
kila kitu kina sababu za msingi unaweza kukimbilia kuoa ukajuta kwani waolewaji nao hawapo! i mean sio wote wanaopenda kuwa mama! unakuta mtu kila anapogusa anaumizwa aoe vivyo hivyo!?
 
Kuna watu wanaoa au kuolewa imradi na wao waonekane katika jamii wameoa au kuolewa
 
Kusoma vizuri na kuwa na kazi nzuri SIO tiketi ya kuwa na Ndoa nzuri

Tusichanganye mambo

Zipo ndoa nzuri lakini hawaja soma na ni wa kipato cha chini

Wasio taka kuoa wana au matatizo ya kisaikolojia au wameguswa na matokeo mabaya ya ndoa walizoziona

Ni Vizuri wakapata msaada na kwa kumshirikisha MUNGU matatizo yao yataondoshwa na wakapata ndoa nzuri

NI MTAZAMO WANGU TU
 
Wanawake wa kula nao maisha wapo wa kila sampuli.
Kuoa kunakua hakuna tena umuhimu. hata watoto wazalisha bila kuoa. what more?
 
Back
Top Bottom