Mwanaume andaa future nzuri kwa wanao, ila usitegemee lolote kwa wanao

Mwanaume tafuta pesa kwa bidii, wape watoto elimu bora, wape mahitaji yao muhimu, jenga nyumba nzuri waishi vizuri, lakini ukizeeka usitegemee lolote kutoka kwa wanao.

Enjoy maisha ya uzee kwa pesa zako mwenyewe ulizochuma ujanani.
Sasa hizo Nguvu za kuwaandalia watu wasio na Msaada kwangu nazitoa wapi na Ili iwaje?

Hizo pesa za ku enjoy utazitoa wapi wakati zimeishia Kwa Watoto?
 
Ushauri mzuri ila ukimlea mtoto wako vyema utakula matunda uzeeni japo hutawategemea ila utafurahia kile ulichopanda kwao
Inafuatana na mambo kadhaa
1. Aina ya mke atakayekuwa naye (kuku wa kisasa au wa kienyeji)
2. Ulimpata kutoka kwa mke wa ndoa au single mother
3. Anakumbuka mazuri uliyomfanyia au ndo wale wanaoimba "bora nimpende mama yangu"
 
Na huo ndio ukweli sasa ninyi endeleeni kukataa ndoa na kujaza single mothers mitaani mkifikiri mnawakomoa wanawake, fainali uzeeni mwisho wa siku mama atabaki na watoto wake watamlea wakati baba atabaki na malaya wake aliokuwa anawanunua, mnaacha kutulia na familia zenu na kuwapa muda wake zenu na watoto wenu mnajikuta miamba kuzini na malaya na kulewa na washkaji kila siku
Mkuu hata kwa walio na ndoa , mwanaume anabaki peke yake , na mama anamsagia baba kunguni kwa watoto .

Apo kila mtu ashinde mechi zake
 
Mkuu hata kwa walio na ndoa , mwanaume anabaki peke yake , na mama anamsagia baba kunguni kwa watoto .

Apo kila mtu ashinde mechi zake
Ni wachache kulinganisha na walioamua kuwa mabachela hadi uzeeni wengi unakuta baba na mama wamezeeka wote, tena baba na mama wakiwa wote ni rahisi watoto kuwatumia hela wote maana watajisikia vibaya kumtumia mama pekee, ila wazazi wakitengana atahudumiwa mama tu baba atapambana na hali yake
 
Ni wachache kulinganisha na walioamua kuwa mabachela hadi uzeeni wengi unakuta baba na mama wamezeeka wote, tena baba na mama wakiwa wote ni rahisi watoto kuwatumia hela wote maana watajisikia vibaya kumtumia mama pekee, ila wazazi wakitengana atahudumiwa mama tu baba atapambana hali yake
Ni kwel ila tupambane , tuweke na akiba, uzeeni fainali.
 
Mwanaume tafuta pesa kwa bidii, wape watoto elimu bora, wape mahitaji yao muhimu, jenga nyumba nzuri waishi vizuri, lakini ukizeeka usitegemee lolote kutoka kwa wanao.

Enjoy maisha ya uzee kwa pesa zako mwenyewe ulizochuma ujanani.
Upo sahihi kabisa

Safi kabisa
 
Akili za kitoto! We are all investors. Tunapanda ili baadaye tuvune. Kama huwezi kuvuna, yanini kupoteza fedha? Hizo pesa ambazo ulitakiwa kuenjoy uzeeni ndizo unatumia kuinvest kwa mtoto. Acheni akili za kijinga
Sasa, unataka maisha Bora ya mtoto wako, atengeneze nani?dunia/maisha hayakomi, wewe ukifa, yanaendelea, ni vzr kuacha watu watakaoijenga dunia iwe vzr, kuliko wewe ulivyoikuta, sasa, unaacha mtoto hana elimu nzuri, hana Mali, atawezaje kuwa raia Bora?
Ni jukumu la mzazi, kutoa/kuandaa mazingira mazuri ya kesho yq mtoto
 
Unaweza kuwa sahihi Mkuu kwa upande mwingine lakini mwisho wa siku kwangu hii huwa ni kama kamari yaani inawezekana watoto wakufae na hata wasikufae pia.

Hivyo yakubidi ujiandae kisaikolojia ili usije dondoka na kuwaachia radhi hasa pale ikitokea wakawa busy kuzisaidia familia zao halafu we ukawa kijisehemu ambacho kwake si namba moja huku hata hizo gharama zote ulizozitumia kwake asizifikirie wala kuzikumbuka kamwe.
Haya ndiyo mawazo ya kiutu uzima! Ukweli wa mambo ni kuwa watoto wa kiume wa siku hizi, hawasaidii wazazi wao wa kiume. Heri wa kike
 
Sasa, unataka maisha Bora ya mtoto wako, atengeneze nani?dunia/maisha hayakomi, wewe ukifa, yanaendelea, ni vzr kuacha watu watakaoijenga dunia iwe vzr, kuliko wewe ulivyoikuta, sasa, unaacha mtoto hana elimu nzuri, hana Mali, atawezaje kuwa raia Bora?
Ni jukumu la mzazi, kutoa/kuandaa mazingira mazuri ya kesho yq mtoto
Huyu anatafuta karo ya mtoto wake
Halafu litoto la JF ati likifanikiwa mbeleni linadai kwanini hakujiwekea akiba ya uzeeni
Anatafuta Karo.jpg

Mingi ya mitoto inayosupport huu Upuuzi ni ya single mother
 
Na huo ndio ukweli sasa ninyi endeleeni kukataa ndoa na kujaza single mothers mitaani mkifikiri mnawakomoa wanawake, fainali uzeeni mwisho wa siku mama atabaki na watoto wake watamlea wakati baba atabaki na malaya wake aliokuwa anawanunua, mnaacha kutulia na familia zenu na kuwapa muda wake zenu na watoto wenu mnajikuta miamba kuzini na malaya na kulewa na washkaji kila siku
Duh.. umeandika kitu kikubwa mno. Kuanzia leo natulia
 
Mwanaume tafuta pesa kwa bidii, wape watoto elimu bora, wape mahitaji yao muhimu, jenga nyumba nzuri waishi vizuri, lakini ukizeeka usitegemee lolote kutoka kwa wanao.

Enjoy maisha ya uzee kwa pesa zako mwenyewe ulizochuma ujanani.
Uzee hauji na amani
Na wala hauna starehe yoyote,ni maisha yanayokuwa sustained na Madawa ,jinsi unavyozeeka ndivyo viungo vyako vinakwisha,utaamka tu siku moja ,miguu inauma, pressure haziko sawa,macho yanaleta ukungu,visukari vinapanda ,stroke na kadha wa kadha ,ni mwili unakupa taarifa ujiandae kuondoka,zidisha ibada ,unganisha watoto wako,weka mambo sawa ili usiache ugomvi ukisepa.

Sent from my TECNO BE6 using JamiiForums mobile app
 
Muhimu mwanaume fanya majukumu yako kama mzazi/mlezi ila kumbuka kuweka akiba kwaajili yako mwenyewe nguvu zitakapokuwa zimeisha.
Na pia hakikisha unakua na watoto angalau wawili nje ya ndoa. Utakuja kunishukuru
 
Back
Top Bottom