Mwanaume anapodanganywa na msichana

Zinduna

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2011
Posts
2,377
Reaction score
3,394



Hebu wanaume leo mnipe ushuhuda, kama hamjawahi kukutana na hiki kizungumkuti cha wanawake.

1.
Unakutana na binti anakuchangamkia na kila mnapokutana anakusalimia kwa bashasha huku akikupa tabasamu maridhawa linalokushawishi kumtongoza kutokana na kuvutiwa naye, lakini unapothubutu kumwambia ya moyoni anakutolea nje kifedhuli kiasi cha kukuumiza moyo wako


2. Inatokea kila asubuhi uendapo kazini na urudipo kazini unakutana na binti huyu mnayeishi naye mtaa mmoja na kila mkutanapo anakutupia macho ya mahaba huku akikusalimu kwa heshima na upendo, mara mojamoja mnapata fursa ya kuongea mawili matatu kuhusu maisha na pilika za mjini na anaonekana kuvutiwa na wewe kwa jinsi unavyozungumza naye kwa upendo,anaonekana dhahiri kukupenda na haachi kujipitisha pitisha pale inapotokea uko kibarazani kwako ukipunga upepo, moyo unakulipuka kwa mapenzi unaona huyu ndiye, lakini unapojaribu kumtupia nyavu anachomoa na kukupotezea mazima humuoni tena na anaanza kukukwepa. Unajikuta ukijiuliza huyu mwanamke ni mzima kweli au ana wazimu?


3. Mnakutana kwenye Party au Klabu, wakati wakucheza mziki anakufuata na kukuomba mcheze,unapocheza naye anakuchezea kwa manjonjo ya kimahaba huku akikushika shika nakukugeuzia makalio yake na ma hipps yaliyojazia jazia na wewe ukipata fursa yakuyashika na kuufurahia utukufu wa Muumba kiasi cha kusababisha maumbile yako ya chini kututumka kwa ashki na tamaa ya kimwili huku akili yako ikikwambia,’leo lazima nikaufaidi huu utukufu wa Mungu.’ Mara muda wa kufunga mziki umefika na kwa kuwa ni usiku wa manane kila mmoja sasa anatoka kutafuta usafiri wa kurudi kwake. Ukiwa umefuatana naye kutoka nje ya Klabu huku ukijiamini utamudu kumshawishi uondoke naye kwenye Ki Vitz chako cha mkopo, mara anakuonyesha jamaa aliyepaki Toyota MarkX akimsubirina anakujulisha,

‘Yule ni mpenzi wangu amenifuata, ahsante kwa kampani, uwe na usiku mwema…!‘

Anakuaga hivyo na kukuacha ukiwa umeduwaa. Unabaki ukisaga meno na kung’ata midomo kwa hasira……



4.
Mnafanya kazi katika jengo moja, na mara kwa mara mnakutana kwenye mghahawa kwa chakula cha mchana na wakati mwingine kwa evening coffee, wewe unakuwa ni mtu wa utani mwingi na masighara, na kila unapofanya utani anacheka na anaonekana kuufurahia utani wako na pia anaonekana kuvutiwa na uwepo wako kila mnapokutana, kwa kifupi ni kwamba anaonekana dhahiri kukupenda. Jambo hilo linakufanya utake kumvuta ili awe mpenzi wako, si kajilengesha…! Unapojaribu kumuomba mtoko ili upate wasaa wa kumtongoza anakutolea nje na kukwambia hayuko interested na wewe… unabaki unashikwa na mshangao, ni kitu gani hiki kinakutokea…


Hebu wanaume nipeni mauzoefu yenu kama mlishawahi kukutana na moja kati ya hivi visirani nilivyovieleza hapo juu

CC:
Kaizer, Asprin Kiranga The Boss, Nyani Ngabu, Mwita Maranya, Preta, snowhite, gfsonwin, King'ast, Ruttashobolwa, lara 1, Mr Rocky

Mkuje mtoe maushuhuda yenyu




 
Inakeraa! Kuna msichana tulizoeana saan, tulikua as friends tunachat paka sa nanee nyt, tunatumiana mashair ya mapenz, tunasoma pamoja niteee paka latee night, na mambo mengineee meng outing nyingiii so day the day nlipo mtamkia! It was ending of our friendship.. akaanza zarauuu! Lol paka leo hatusemeshani
Tukiingia lecture room kila mtu kivyakeeee

I regret
 
Unakutana na binti hapa Jamii Forum. Anakupm kila saa. Anakupa like hatakama umepost utumboo,anakusifia jukwaani mpaka unahisi mzIgo utapewa hata kabla ya kuomba.Ila siku unamcheki pm anakupa namba za simu. Mnaanza kuchati kwenye simu unamtongoza halafu anakutosa kama vile sio yeye hapa JF.
 
Namba 3 imefanana na tukio lilowahi kunitokea. Dah mtu unakua umeshajihakikishia ushindi kabisa. Kweli football sio dakika tisini tu unaweza kulia dakika za nyongeza.
 
Hizi namba 1,2,4 kwa uzoefu wangu huwa ni vunga.yamenikuta zaidi ya mara tatu.cha kushangaza nikikaa kimya na mimi nashangaa vinaanza kujirengesha.

Au akikuona na chuma nyingine anajinunisha,visa kibao.

Hii namba tatu,madomo zege inawatokea sana.huwezi cheza na demu unamshika kiuno mpaka anatoka jasho,hujajua hatma ninini.kama ana mtu itajulikana mapema sana hata huo muziki hatutacheza.
 
Mh! Kuna mmoja huyo, mpaka mtoko nilitoka nae!!! Ila akanichinjia baharini!!! Wanawake bwana! Sijui huwa wanafikiria nini!!!
 
Yamenitokea sana dawa yake usiamini mwanamke nawanafanya hivo makusudi kutimiza tu hulka ya kike dawa yao wakikutega naww watege ni kucreate question mark vichwan mwao mpaka wachanganyikiwe inaboa kweli.

Yaan unakuta demu anakushobokea mpaka kero full uchokozi ukimtongoza umeharibu anaaza dharau dawa ndo hiyo wakitega ww unategua than na ww unatega
 
namba 3 imefanana na tukio lilowahi kunitokea. Dah mtu unakua umeshajihakikishia ushindi kabisa. Kweli football sio dakika tisini tu unaweza kulia dakika za nyongeza.
Hahahah. Mkuu hawa viumbe wana akili kama samaki.. siku nyingine usijihakikishie ushindi mpaka refa amepuliza kipenga
 
Kuna wanawake ambao wanatafuta confidence kwa watu so wanajipima na mwanaume ambaye anamuona ni size yake, anajweka weka karibu ukimtongoza tu anajiona kumbe yupo kwenye form bado.
Na usimtongoza siku unakija sikia maneno kwa washkaji jamaaa kaonyeshwa sign zote lakini kashindwa kula mzigo unaeza itwa domo zege.

Game simple hili kuwa mind reader soma nyuso ujue huyu anataka nini, ukiona ni mtu wa drama (drama queen)
wew kuwa director, muongoze kama Cow wako vile unamtengeneza akili yake ajue kuwa anafanikiwa kumbe anapangwa, Unakuja Kula mzigo bila kutia hata neno moja.

MWISHO SIKU ATAJIONA KUWA ALIZANI ANAPANDA KUMBE ANAVUNWA……
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…