Wanaume wengine ving'ang'anizi mno...
Nikiwa napita pita mitaa ya mji wa watu nilikutana na kisa kimoja.
Nikiwa napita mitaa fulani fulani nikakutana na mkusanyiko wa watu kama kumi hivi na mwanamke akiwa ameshikilia kiuno anachonga ile mbaya. Nikasogea karibu ili nijue kulikoni. nilivyosogea nikasikia huyo mdada akimsema jamaa mmoja ambaye alikuwa kimya kama kanyeshewa mvua.
Huyu dada nikamsikia akisema kuwa "nimekuita hapa ili umuone mume wangu kwa sababu ulidhani mimi ni mtu wa kiivyo, fedha zako ulizokuwa unanipa kwa ajili ya chipsi sema nikiasi gani ili mume wangu akurudishie" pembeni palikuwa na mwanaume amekaa ametulia ambaye inadaiwa ndiyo mume wa huyo dada. Jinsi kisa kilivyokuwa ni kwamba huyu jamaa alikuwa akimtokea huyu dada ambaye kazi yake anauza duka la dawa (pharmacy).
Sasa huyu jamaa alikuwa akienda mara kwa mara kwa huyu dada na kutoa ofa mbalimbali ikiwamo ya kumnunulia chipsi na soda. Sasa huyu dada alivyokuwa anasumbuliwa akamwambia huyu jamaa wakutane mahali fulani ambapo wataongea zaidi. sasa huyu jamaa alipofika hapo ndiyo kizazaa hiki kikaanza.
Kwanza huyu mdada alimtambulisha jamaa kwa mume wake. Halafu akamwambia nilikuona unanisumbua sana kila napokueleza nimeolewa ulikuwa haunielewi sasa huyu hapa ni mume wangu.
Ongea sasa yote uliyokuwa unaniambia mbele ya mume wangu" jamaa alivyoambiwa hivyo akawa anajichekeshachekesha tu, jamaa akasema nilikuwa sina nia mbaya kama unavyodhani bali mambo ya kawaida tu.
Mume wa jamaa akawa anamuangalia tu bila kusema kitu, jamaa alivyoona mambo yanakuwa mabaya akaamua kuondoka huku mdada akimtupia maneno ya kashfa kuwa "kama amezoea kuzoa zoa siyo hapa, mimi nina mume wangu na ninajiheshimu" Jamaa nilimuona akiondoka huku akiongea mwenyewe kwa maneno ambayo sikuyaelewa.
Nami nikaondoka huku yule mdada na mtu aliyedai ni mume wake wakicheka. Sasa nikajiuliza huyu ni mume wake kweli au wa kuchonga ili kumuumbua jamaa? kama alijua ana mume kwanini alikuwa anakula vya watu?
Aisee, kwahiyo uliacha shughuli zako ukajisogeza kusikiliza kinachoendelea, kazi unayo
Nimekereka
Kimekukera nini....
huyo mwanamke na anayejiita mumewe, wamenikwaza. hasa huyo mwanamke ambaye amekula vya watu akaogopa kwenda kutoa k mwenzake alipe
Nikiwa
napita pita mitaa ya mji wa watu nilikutana na kisa kimoja.
Nikiwa napita mitaa fulani fulani nikakutana na mkusanyiko wa watu kama
kumi hivi na mwanamke akiwa ameshikilia kiuno anachonga ile mbaya.
Nikasogea karibu ili nijue kulikoni. nilivyosogea nikasikia huyo mdada
akimsema jamaa mmoja ambaye alikuwa kimya kama kanyeshewa mvua.
Huyu dada nikamsikia akisema kuwa "nimekuita hapa ili umuone mume wangu
kwa sababu ulidhani mimi ni mtu wa kiivyo, fedha zako ulizokuwa unanipa
kwa ajili ya chipsi sema nikiasi gani ili mume wangu akurudishie"
pembeni palikuwa na mwanaume amekaa ametulia ambaye inadaiwa ndiyo mume
wa huyo dada. Jinsi kisa kilivyokuwa ni kwamba huyu jamaa alikuwa
akimtokea huyu dada ambaye kazi yake anauza duka la dawa (pharmacy).
Sasa huyu jamaa alikuwa akienda mara kwa mara kwa huyu dada na kutoa ofa
mbalimbali ikiwamo ya kumnunulia chipsi na soda. Sasa huyu dada
alivyokuwa anasumbuliwa akamwambia huyu jamaa wakutane mahali fulani
ambapo wataongea zaidi. sasa huyu jamaa alipofika hapo ndiyo kizazaa
hiki kikaanza.
Kwanza huyu mdada alimtambulisha jamaa kwa mume wake. Halafu akamwambia
nilikuona unanisumbua sana kila napokueleza nimeolewa ulikuwa haunielewi
sasa huyu hapa ni mume wangu.
Ongea sasa yote uliyokuwa unaniambia mbele ya mume wangu" jamaa
alivyoambiwa hivyo akawa anajichekeshachekesha tu, jamaa akasema
nilikuwa sina nia mbaya kama unavyodhani bali mambo ya kawaida tu.
Mume wa jamaa akawa anamuangalia tu bila kusema kitu, jamaa alivyoona
mambo yanakuwa mabaya akaamua kuondoka huku mdada akimtupia maneno ya
kashfa kuwa "kama amezoea kuzoa zoa siyo hapa, mimi nina mume wangu na
ninajiheshimu" Jamaa nilimuona akiondoka huku akiongea mwenyewe kwa
maneno ambayo sikuyaelewa.
Nami nikaondoka huku yule mdada na mtu aliyedai ni mume wake wakicheka.
Sasa nikajiuliza huyu ni mume wake kweli au wa kuchonga ili kumuumbua
jamaa? kama alijua ana mume kwanini alikuwa anakula vya watu?
Ungekwenda polisi
Hahahaaa ninyi watu....msitufanye tuogope kupokea hata ofa za soda...
Kwani wewe ukihongwa hujui??
asante sana mdada. Swali dogo tu, hivi mtu anasoma ili aajiriwe au atumie ujuzi aliupata kwa maendeleo ya taifa lake? maendeleo ya taifa yanaletwa na watu walioajiriwa? Mbona una akili mgando? kweli nchi hii majanga.sio kosa lake ajira za sociology ni ngumu sana kupata kama huna ndugu wa kukupigia pande hivo huishia kuzunguka zunguka tu mitaani....