Mwanaume alivyoumbuliwa

Mwanaume alivyoumbuliwa

SOCIOLOGISTTZ

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2013
Posts
2,615
Reaction score
929
Nikiwa napita pita mitaa ya mji wa watu nilikutana na kisa kimoja.

Nikiwa napita mitaa fulani fulani nikakutana na mkusanyiko wa watu kama kumi hivi na mwanamke akiwa ameshikilia kiuno anachonga ile mbaya. Nikasogea karibu ili nijue kulikoni. nilivyosogea nikasikia huyo mdada akimsema jamaa mmoja ambaye alikuwa kimya kama kanyeshewa mvua.

Huyu dada nikamsikia akisema kuwa "nimekuita hapa ili umuone mume wangu kwa sababu ulidhani mimi ni mtu wa kiivyo, fedha zako ulizokuwa unanipa kwa ajili ya chipsi sema nikiasi gani ili mume wangu akurudishie" pembeni palikuwa na mwanaume amekaa ametulia ambaye inadaiwa ndiyo mume wa huyo dada. Jinsi kisa kilivyokuwa ni kwamba huyu jamaa alikuwa akimtokea huyu dada ambaye kazi yake anauza duka la dawa (pharmacy).

Sasa huyu jamaa alikuwa akienda mara kwa mara kwa huyu dada na kutoa ofa mbalimbali ikiwamo ya kumnunulia chipsi na soda. Sasa huyu dada alivyokuwa anasumbuliwa akamwambia huyu jamaa wakutane mahali fulani ambapo wataongea zaidi. sasa huyu jamaa alipofika hapo ndiyo kizazaa hiki kikaanza.

Kwanza huyu mdada alimtambulisha jamaa kwa mume wake. Halafu akamwambia nilikuona unanisumbua sana kila napokueleza nimeolewa ulikuwa haunielewi sasa huyu hapa ni mume wangu.

Ongea sasa yote uliyokuwa unaniambia mbele ya mume wangu" jamaa alivyoambiwa hivyo akawa anajichekeshachekesha tu, jamaa akasema nilikuwa sina nia mbaya kama unavyodhani bali mambo ya kawaida tu.

Mume wa jamaa akawa anamuangalia tu bila kusema kitu, jamaa alivyoona mambo yanakuwa mabaya akaamua kuondoka huku mdada akimtupia maneno ya kashfa kuwa "kama amezoea kuzoa zoa siyo hapa, mimi nina mume wangu na ninajiheshimu" Jamaa nilimuona akiondoka huku akiongea mwenyewe kwa maneno ambayo sikuyaelewa.

Nami nikaondoka huku yule mdada na mtu aliyedai ni mume wake wakicheka. Sasa nikajiuliza huyu ni mume wake kweli au wa kuchonga ili kumuumbua jamaa? kama alijua ana mume kwanini alikuwa anakula vya watu?
 
Huyo sio mumewe...na kama ni mumewe hana akili..ni liboya fulani hivi maana mwanaume mwenye akili hawezi kukubali upuuzi huo.....ina maana huyo dada hawezi kusema hapana yeye mwenyewe hadi mumemwe ndo amsaidie kukataa?
 
hata mimi nilishangaa sana

Wooooi huyo dada na mumewe hawajielewi
Nb: kama ni kweli ni mumewe na pia kama hii story ni kweli
 
Wooooi huyo dada na mumewe hawajielewi
Nb: kama ni kweli ni mumewe na pia kama hii story ni kweli
Kujua kama kweli ni mume halisi mimi sikujua kwani hata mm nilikuwa najiuliza...lakini kuhusu hii story ni ya kweli kabisa nimeishuhudia mm mwenyewe

Huyo sio mumewe...na kama ni mumewe hana akili..ni liboya fulani hivi maana mwanaume mwenye akili hawezi kukubali upuuzi huo.....ina maana huyo dada hawezi kusema hapana yeye mwenyewe hadi mumemwe ndo amsaidie kukataa?

Mim ndio maana nashangaaga akili za wengine japokuwa hata zangu inawezekana wakazishangaaa huyu hapishani sana na yule anaetoa namba ya mumewe
 
Huyo sio mumewe...na kama ni mumewe hana akili..ni liboya fulani hivi maana mwanaume mwenye akili hawezi kukubali upuuzi huo.....ina maana huyo dada hawezi kusema hapana yeye mwenyewe hadi mumemwe ndo amsaidie kukataa?

hilo jamaa zezeta kweli.. Na hakuna mwanamke mbaya kama yule anayekuambia wanaume waliomtongoza wakat aliowakubalia na kugegeda hakuambii na hujamkuta bikra... Ningekuwa mm ili tuelewane ningemwambia aniambie hata waliomgegeda vingnevyo notice tu
 
Mwanamke kama huyu lazima nimle tena mchana kweupe.ni mrahisi sana maana hajitambui
 
Huyo sio mumewe...na kama ni mumewe hana akili..ni liboya fulani hivi maana mwanaume mwenye akili hawezi kukubali upuuzi huo.....ina maana huyo dada hawezi kusema hapana yeye mwenyewe hadi mumemwe ndo amsaidie kukataa?

wanaume wa uswahilini wanaweza khantwe
 
Huyo dada amejitengenezea mazingira magumu. Watoto wa kihuni wanaweza kufanya yao, huwezi jua jamaa alikuwa anawaza nini kichwani baada ya hiyo aibu. Dada hajielewi huyo.
 
Back
Top Bottom