"Mwanasiasa huyu bwana!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

"Mwanasiasa huyu bwana!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Thanda, Apr 6, 2012.

 1. Thanda

  Thanda JF-Expert Member

  #1
  Apr 6, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 1,915
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mwanasiasa huyu Bwana!!
  Masikini, fukara,tajiri mkwasi kijana wa jana, umri wake wangu, hana wasiwasi,wala upesi, katika maamuzi yake.
  Hana dini, wala kabila, si mbaguzi, bali mpevu,mkomavu, shupavu, nguli wa sera,kapera, hana mwanzo wala mwisho,

  Mwanasiasa huyu Bwana!!
  Hodari, daktari, mjuzi wa habari, profesa mwingi wa pesa, mwanasheria mrengo wa kulia,fundi muhunzi,seremala hana Hila, mwalimu mhitimu, mtafiti mdhibiti,mchapa kazi, kwa dhahiri mshairi, mwanasiasa!!

  Mwanasiasa huyu Bwana!!
  Mwanasiasa huyu nguli,si fedhuli,mkomavu,shupavu, mvumilivu, mnyenyekevu,mkakamavu
  Mzamili, mzamivu mpevu katika sera huwajua wapiga kura wake,
  Mtunzi wa katiba, mwelewa, anaijua, anaipenda, anaisoma, huwaita wapiga kura wake, huketi kula nao na kuwaambia"Leteni hoja zenu matatizo yenu msiyoyaweza, nami nitayatatua" pia huongeza..mtakula mtalala pasi na shaka.

  Mwanasiasa huyu Bwana!!
  Mikutano yake hadharani maadui zake uwandani,hawana la kumfanya, anajua yote,anaona yote, yuko kila mahali, Usiku na mchana, hachoki. huwaambia adui zake " mnanipinga huku nina kinga,katiba mwaijua,kanuni ziko wazi hizo Zinanilinda"mwanasiasa huyu hujua matatizo ya watu wake, kama vile maji hai, umeme,hewa safi,naye huwapa bure Bila tozo.

  Mwanasiasa huyu Bwana!!
  Rais, Makamu, Waziri, Mbunge,Diwani, Msuluhishi,Amiri Jeshi aliye mcheshi, mpatanishi, vyama vyote vyake, watu Wote wake, kila kitu chake, masikini mwenye kutajirisha wengi, tajiri mwenye kufilisi wengi"mkinikataa nami Nawakataa" huu ndio wake msisitizo.

  Mwanasiasa huyu Bwana!!
  Jeuri, mkali, mpole, smart, mtanashati, usafiri wake Punda si farasi,mkokoteni, baiskeli magari ya kifahari NO.huwaasa Wapiga kura zake kuwa safi mbali na hila, ufisadi, udhalimu,uonevu wizi na uchakachuzi,huwapa uhuru wa maamuzi

  Mwanasiasa huyu Bwana!!
  Nguvu zake za asili, mwanzo wake hauna mwisho, makini, hajulikani katokea wapi, msomi asiyekumbukwa, falsafa Zake huria, serikali yake ina nguvu, jeshi lake lina nguvu halina ufukara,papara, wala Mikwara...Anaheshimika,anapendwa,anasifika kwa amani,upendo,ukarimu,anasomesha wengi, bure!! Anatibu bure!! Anasamehe wafungwa bure!! wenye shida mbali mbali huwasaidia kwa fedha za mfuko wa jimbo lake bure!!

  Mwanasiasa huyu Bwana!!
  Mwaminifu, mtiifu, mwadilifu,namsifu, si mimi wala wewe ni yeye mwenye mvuto, hatozi kodi wala ushuru
  Kura zetu tumpigie,ukweli wake tuusikie,kadi yangu imani yangu nitaitumia kupata haki yangu, Sishawishiki,sihongeki,sishauriki kura zangu kutompa.

  Mwanasiasa huyu Bwana, we acha tu, Namkubali!!
   
 2. Borakufa

  Borakufa JF-Expert Member

  #2
  Apr 6, 2012
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 1,503
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Sawa malenga wetu
   
 3. Thanda

  Thanda JF-Expert Member

  #3
  Apr 6, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 1,915
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  nashukuru sana
   
Loading...