Serikali moja tu ndio Suluhu nchi hii asotaka ajinyonge!
Hii serikali moja ya aina ipi?
Serikali ya shirikisho ? Ambayo itafanya iwepo serikali ya Tanganyika na serikali ya Zanzibar kama serikali za majimbo halafu iwepo serikali ya shirikisho?
Au serikali moja kwa maana ya kuimeza Zanzibar na kuifanya ni sehemu(mkoa, wilaya) ya Tanganyika(Tanzania)? na kufuta dhana ya muungano wa nchi mbili wa baadhi ya mambo?
Rai yangu, turudishe Serikali ya Tanganyika na iendelee kuwepo serikali ya Zanzibar ili tujipe nafasi nzuri ya kupanga na kutafakari kuanzisha serikali ya Shirikisho la Afrika Mashariki.
Ni wazi tutakapofikiria shirikisho la Afrika mashariki hatutapenda serikali zetu zipotee na iwepo mamlaka moja tu, serikali ya Afrika Mashariki.
Tuache unafiki, tuone tatizo na tusijifanye wajanja kwani ujanja mwingi, mbele.......
Muungano wa nchi mbili (unaosemwa ni wa hiari) ambao hauainishi mipaka ya mamlaka ya wadau/wanachama wake kinagaubaga unafikia mahali unagonga ukuta kama huu wetu. Tabia ya wanasiasa wetu kuamini kuwa matumizi ya nguvu kuulinda/ kuulazimisha uwepo muungano inatujengea chuki na itatuletea maafa. Tabia ya wanasiasa wetu kufikiria kuwa kero zitajitatua zenyewe na tabia ya kuendelea kuficha uchafu chini ya zulia imetufikisha hapa tulipo leo.
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar(Tanzania)kama ulivyo sasa ni Muungano wa wanasiasa wajanja tu ambao wanatutengenezea bomu hatari. Wanasiasa hawa wamelea kero za muungano kwa miaka 48 na kutoa kauli za kisanii kuwa kero zitatuliwa,zitashughulikiwa, mwaka baada ya mwaka, huku wakiacha kero hizo kuongezeka.
Muungano huu ni kiini macho cha CCM cha kutaka kuendelea kutawala Tanzania. Hata hivyo kama ni wenye kuona mbele na mbali basi wangeelekeza juhudi zao katika kutatua hizo kero za muungano. Tatizo la CCM linaongezeka kwani kuna CCM ya Zanzibar ambayo ina msimamo wa akina Moyo, Raza nk na kuna CCM bara inayoamini katika kuleta serikali moja, Tatizo pia linaongezeka kutokana na kuwepo na sisa za vyama vingi na kila chama kikiwa na sera ya Muungano tofauti. CCM wamebakiwa na njia moja tu, kutumia mabavu/nguvu kuulinda muungano au wakubaliane na uhalisia wa sasa.Watatue kero za muungano.
Kuna wizara maalum ya Muungano(inashughulikia muungano, matatizo ya Muungano, kero za muungano), kazi yake ni nini? Kero ngapi imetatua? au nini kinakwamisha kutatua kero nyenginezo?
kwa bahati kila kitu hapa Tz ni siri. Kama hii wizara ingekuwa inabainisha kero za Muungano zilizopo baina ya Tanganyika(Bara) na Zanzibar na wananchi kuzielewa na vipi zinatatuliwa ingeepusha hizi jazba ambazo wengi wetu tumo tu, bendera kufata upepo.
Kila mtu anakubali kuwa Muungano una kero nyingi na sasa Muungano wenyewe unakuwa ni kero.
Kwa wale washabiki wa serikali moja,nchi moja,taifa moja ningeshauri wangefikiria hii kitu
onecountrytwosystems. Nafikiri Zanzibar watapata kupumua kama wanavyodai huku Tanganyika(Tanzania)tunajiandaa kuunda Shirikisho la kisiasa la Afrika Mashariki. Tunu yetu ya kuwa pamoja na ndugu zetu wa EAC katika nchi moja,serikali moja na taifa moja lenye nguvu itapata muda mzuri wa matayarisho ili tusirudie makosa ya muungano wa Tanzania.