Mwanasheria mkuu ampinga Dk Hoseah

mpigauzi

JF-Expert Member
Jul 17, 2012
275
71
NI KUHUSU SHERIA KUIKWAZA TAKUKURU KUWASHTAKI VIGOGO WA UFISADI

Kizitto Noya | Mwananchi | Monday, 20 August 2012

MWANASHERIA Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema amesema Sheria ya Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa (Takukuru), ni nzuri na kwamba haipaswi kufanyiwa mabadiliko kama ambavyo imekuwa ikidaiwa.

Jaji Werema aliliambia gazeti hili jana kuwa haoni haja ya sheria hiyo kufanyiwa mabadiliko sasa kwa kuwa haina tatizo na ipo kutekeleza misingi ya utawala wa Sheria.

"Mimi nakubaliana na Sheria hii ya (Takukuru) kwamba iendelee kuwapo. Hakuna haja ya kuifanyia mabadiliko sasa. Ni nzuri kwa kuwa inazingatia misingi ya utawala wa sheria," alisema Jaji Werema.

Kauli ya Jaji Werema inapingana na ile iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dk Edward Hoseah kwamba sheria hiyo imekuwa ikiwakwaza kuwashughulikia wala rushwa wakubwa, kwani majalada ya kesi zilizokwishafanyiwa uchunguzi yamekwama kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka (DPP).

Wiki iliyopita Dk Hoseah alilalamikia sheria hiyo, hasa kifungu cha 37 na 57 akisisitiza kuwa ni mbovu kwa kuwa vinamzuia kuwafikisha watuhumiwa wa rushwa kubwa mahakamani. "Tusaidieni sheria hii ibadilishwe ili iweze kuturuhusu kufanikisha kupambana na rushwa nchini," alisisitiza Dk Hoseah.

Hata hivyo, jana Werema alipinga dhana hiyo na kusema kwamba siyo sahihi kuipa Takukuru mamlaka yote; kutuhumu, kupeleleza na kushtaki kwa kuwa kufanya hivyo ni kinyume na demokrasia, Katiba na utawala wa sheria.

Kumrundikia mtu au taasisi moja mamlaka zote hizo, ni kinyume na misingi ya utawala bora, alisema.

"Haiwezekani mtu (Dk Hoseah) akawa na mamlaka ya kupeleleza na kushtaki, halafu Mahakama ikiwaachia huru watuhumiwa, atasema siyo mimi ni kosa la Mahakama, We can't do that! (hatuwezi kufanya hivyo)," alisema Werema na kuongeza:

"Mimi nakubaliana na kitu kimoja, kila mamlaka iwe na kigingi. Iwe Mamlaka ya Rais, Bunge au Mahakama, lazima kuwe na chombo cha ku-check and balance," alisema Jaji Werema.

Kauli hiyo ya Jaji Werema imekuja siku chache tangu Mkurugenzi wa Mashtaka, (DPP) Eliezer Felishi kukiri kwamba kazi ya kuwafikisha watuhumiwa hao mahakamani ni yake, lakini kesi nyingi zinakwama.

DPP Feleshi alisema ucheleweshaji wa kesi za rushwa kupelekwa mahakamani, unatokana na kukosekana kwa ushahidi wa kutosha. "Ikifikia hapo, nalazimika kuyarudisha mafaili hayo kwa Takukuru," alisema.

"Mimi nafanya kazi kwa kufuata sheria na taratibu zilizowekwa na Serikali. Siwezi kufanya kazi kwa sababu mtu fulani ametaka nifanye. Jambo hilo linaweza kuniletea matatizo baadaye," alisema na kuongeza:

"Kutokana na hali hiyo, siwezi kupeleka mahakamani jalada ambalo halijakamilika. Sheria inanipa siku 60 niwe nimepeleka kesi mahakamani, lakini kama ushahidi haupo cha kufanya ni kurudisha Takukuru faili."

Madai ya Dk Hoseah
Awali Dk Hoseah alisema anajua matarajio ya wananchi ni makubwa kwa Takukuru, lakini sheria imewafunga mkono kwa kuwa hawawezi kuchukua uamuzi dhidi ya kesi kubwa za ufisadi bila ushauri wa DPP.

"Sina mamlaka ya kumpeleka mtuhumiwa wa rushwa kubwa mahakamani. Uwezo wangu ni kupeleka walarushwa ndogondogo tu na kwamba kazi yangu ni kuchunguza tu," alisema Dk Hoseah na kuongeza;

"Sheria yetu imetufunga mikono kwa kuwa kumpeleka mtu mahakamani siyo uamuzi wangu, bali ya DPP."

Awali Dk Hoseah alisema sheria hiyo katika kifungu cha 57 inamzuia kuwapeleka mahakamani watuhuhumiwa wakubwa wa rushwa, mpaka awafikishe kwa Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP).

Kifungu hicho cha 57 (1) kinasema kuwa shtaka lolote la kosa lililoelezwa kwenye Sheria ya Takukuru lazima lifunguliwe kwa ruhusa ya maandishi kutoka kwa DPP. Kifungu cha 57 (2) kinamtaka DPP ndani ya siku 60 kutoa au kukataa ruhusa ya kushtakiwa.

Dk Hoseah alisema, hiyo ni moja ya changamoto zinazoikabili taasisi yake na kwamba wananchi wasubiri mabadiliko ya kiutendaji kama sheria itabadilika na kumruhusu kufanya hivyo.

Maelezo ya Dk Hoseah yanaungwa mkono na sehemu ya taarifa ya awali ya Mpango wa Nchi za Afrika wa Kujitathmini (APRM) ambayo inaeleza kwamba kikwazo cha ufanisi katika vita ya rushwa nchini Tanzania ni sheria inayowazuia Takukuru ipate kibali cha DPP kabla ya kufungua kesi kubwa za rushwa.

"Ni wala rushwa wadogo wadogo tu ndiyo wanaoweza kushtakiwa na Takukuru, lakini makosa makubwa ya rushwa yanayohusu viongozi au watu wa karibu na viongozi wakubwa ni mara chache sana kufunguliwa kesi mahakamani," inasema sehemu ya taarifa hiyo na kuongeza:

"Mfumo huu ni kama unainyima mamlaka ya kiutendaji Takukuru na kimsingi, unakandamiza juhudi za chombo hiki kupambana na rushwa".

Hii siyo mara ya kwanza kwa ofisi hizi mbili kuvutana kuhusu udhaifu katika sheria ya Takukuru, lakini mara zote Serikali imekuwa ikisisitiza kwamba lazima mashtaka kwa watuhumiwa wakubwa wa rushwa wapate yapate kibali cha DPP kabla ya kufikishwa mahakamani.

~~~~~~~~~~~~~~~~~

Huyu ndiyo AG wetu. Hapa anatetea uozo, kiujumla Hosea yuko sahihi kwani kesi za rushwa bila ridhaa ya DPP, TAKUKURU hawawezi peleka mahakamani.

Hawa ndo majaji wetu
 
Werema hapo anawalinda wala rushwa waendelee kupeta tu. Kwanza Lissu Alisema huyu ana upofu wa sheria.
 
i hate kukubaliana na Hosea kwa maana naamini ki kiongozi mmoja dhaifu sana lakini kwa hili yuko sahihi kwanini viongozi wengi wana mamlaka lakini hawana mamlaka kamili kwani mfumo mbaya wa uongozi unawafanya viongozi hata kama wana nia ya kweli ya kuwashugulikia waalifu wasiweze kufanya hivyo kwa maana kuna sheria mbili zinazoshugulikia maskini na kuna za vigogo.

soultion:
Taasisi zote zinazoshugulikia haki za raia hazipaswi kusimamiwa na wanasiasa kama kuwateua wawateue na kuthibitishwa na bunge na kupewa mamlaka kamili bila kuingiliwa na mtu na hata aliyemteua asiwe na mamlaka naye si ya kumtumia na wala kumfukuza kazi.
 
Kupatikana kwa mtu kama Jaji Werema, ni moja ya udhaifu mkubwa uliopo kwenye KATIBA yetu. Kwanini asiruhusu swala hili lijadiliwe BUNGENI ambapo sheria hutungwa, kwanini yeye alazimishe iwepo hivyohivyo wakati imeshindwa kutekelezeka na muhusika wa TAKUKURU analalamika hilo. Wananchi tunapata mashaka sana sababu tunaona MAFISADI wanaendelea kufisadi bila ya kuchukuliwa hatua, tukiuliza tunaambiwa tupeleke vithibitisho wakati vingine vipo wazi kabisa.
 
Kama swala ni checks and balances kwa nini iwe rushwa kubwa tu? Hapa naona swala ni kulindana tu. Si inaeleweka kuwa chombo cha kutafsiri sheria ni Mahakama, ikiwa kesi itakuwa haina ushahidi mtuhumiwa si ataachiwa? DPP sasa amekuwa mahakama na kama ni mahakama kwa nini kesi ipelekwe mahakamani.

This is a double handling of the same issue. Kutafuta kichaka cha kufichia madhambi. Hivi DPP anakaguliwa na nani? Shauri likienda kwa DPP kuna uwezekano wa kukata rufaa.

CORRUPTION=TECHNICAL POWER+ DISCRETION+AUTHORITY - TRANSPERANCY. The DPP fits into this equestion therefore is position which fuels corruption it cannot sit the same table with ant corruption
 
Ninashangaa anaposema 'rushwa kubwa na ndogondogo'. Ina maana kuna cut off point na ningependa hilo nalo liwekwe wazi tuelewe rushwa kubwa ni nini na rushwa ndogo ni ipi.

Pia kama sheria ni ili itusaidie kwenye mambo ya check and balance, mbona sio raia wote wanapewa treatment sawa? Ina maana wala rushwa 'ndogondogo' hawahitaji checking and balancing?

CHADEMA na vyama vingine vya upinzani tunawaomba sana mkaliwakilishe hili swala Bungeni liwe reviewed. Nina hakika wamo hata wabunge wa CCM ambao hawapendi mambo kama haya.
 
Basi kama ni hivo takukuru ifungwe.. Sioni point ya wai kukamata watu alafu dpp hafanyi chochote... Ndio yake nayosema kua vyombo nyeti kama hivi viko chini ya serikali afu bado mnataka kuwashtaki watu hao hao haiwezekani
 
Tatizo la jaji Warema ni udhaifu wake katika kufanya mabadiliko ya kisheria Dr. Edward G. Hoseah yuko sahihi mapungufu ya kuwafikisha vigogo mahakamani yanakwamishwa na sheria ilipopo UTENDAJI WA TAKUKURU JAMANII NI IMARA SANA NA NI MAKINI Dr Hoseah ni kiungo na ni kichwa
 
Werema hana hata aibu. Sioni hata anachotetea hapa. Hizo checks and balance mbona hazizingatiwi kwa rushwa ndogo ndogo

Kama vipi PCCB bora ivunjwe tu. PCCB lazima wajione wanyonge wanapopeleleza rushwa kubwa kwasababu hiyo sheria peke yake ya kutaka DPP ndo apeleke mahakamani mashitaka ya kesi kubwa za rushwa, inadhihirisha DPP amewekwa hapo kuwalinda mafisadi

Ndo maana PCCB wataishia kuwakamata afisa mtendaji wa kijiji hawataweza hata kuwakamata polisi kwasababu public prosecutor wa mahakama ya wilaya naye lazima atazame maslahi yake

Na kwa wala rushwa kubwa ngazi ya taifa DPP ndo atawakingia kifua mafisadi
 
Wakati wadau tukidai katiba mpya, Mh Welema aliweka bayana msimamo wake wa kupinga katiba mpya. Dr. Hosea ametoa mawazo yake kuhusu sheria ya kuwashitaki Mafisadi Papa, Jaji Welema anaipinga nia hii nzuri ya kuondoa bureaucracy serikalini.

Wana JF naomba majibu ya swali langu please
 
Werema amenyoosha maelezo, though inaweza kuonekana anawakingia kifua lakini ukweli unabaki palepale, haiwezekani ukatuhumu, ukapeleleza na kushtaki bila mtu mwingine kucheki kama ni majungu, visasi au kweli kuna kosa in terms of ushahidi, haiwezekani.

Jiulize hao Pccb wanaong'ang'ania kufutwa kipengele cha conset ya Dpp wameshinda kesi ngapi? ukicompare na walizoshindwa? na zile za disign ya Liyumba? Sometimes watu tunakuwa mashabiki zaidi.

Sheria iko poa tatizo labda ni dhamira tu, Hosea aache visingizio na siku zote serikali huwa ina kauli moja na msimamo 1
 
Wameshachanganyikiwa!wanapigana chenga wao kwa wao,mwisho wa siku watajifunga wenyewe!waacheni!
 
Ninashangaa anaposema 'rushwa kubwa na ndogondogo'. Ina maana kuna cut off point na ningependa hilo nalo liwekwe wazi tuelewe rushwa kubwa ni nini na rushwa ndogo ni ipi.

Pia kama sheria ni ili itusaidie kwenye mambo ya check and balance, mbona sio raia wote wanapewa treatment sawa? Ina maana wala rushwa 'ndogondogo' hawahitaji checking and balancing?

CHADEMA na vyama vingine vya upinzani tunawaomba sana mkaliwakilishe hili swala Bungeni liwe reviewed. Nina hakika wamo hata wabunge wa CCM ambao hawapendi mambo kama haya.

Mkuu hapa huelewi nini rushwa kubwa ni ile ambayo GAMBAZ wakikamatwa nayo, hapo consent ya DPP ni lazima. Lakini mimi na wewe tukikamatwa ni rushwa ndogo, HAPA HATUHITAJI CONSENT YA DPP
 
Nimefuatilia sana umakini wa AG na kugundua hapaendi ama ni mwoga wa mabadiliko.HAPENDI LAWAMA AU KUZOMEWA NA MWAJIRI WAKE,ANAPENDA MWAJIRI WAKE AWE MBELE NA YEYE AWE MSHAURI WAKE2.
 
Mwanasheria Mkuu ampinga Dk Hoseah Send to a friend
Monday, 20 August 2012 08:35

0000000000000000000jajiweremaorij.jpg
Jaji Werema.

NI KUHUSU SHERIA KUIKWAZA TAKUKURU KUWASHTAKI VIGOGO WA UFISADI
Kizitto Noya
MWANASHERIA Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema amesema Sheria ya Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa (Takukuru), ni nzuri na kwamba haipaswi kufanyiwa mabadiliko kama ambavyo imekuwa ikidaiwa.

Jaji Werema aliliambia gazeti hili jana kuwa haoni haja ya sheria hiyo kufanyiwa mabadiliko sasa kwa kuwa haina tatizo na ipo kutekeleza misingi ya utawala wa Sheria.

"Mimi nakubaliana na Sheria hii ya (Takukuru) kwamba iendelee kuwapo. Hakuna haja ya kuifanyia mabadiliko sasa. Ni nzuri kwa kuwa inazingatia misingi ya utawala wa sheria," alisema Jaji Werema.

Kauli ya Jaji Werema inapingana na ile iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dk Edward Hoseah kwamba sheria hiyo imekuwa ikiwakwaza kuwashughulikia wala rushwa wakubwa, kwani majalada ya kesi zilizokwishafanyiwa uchunguzi yamekwama kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka (DPP).

Wiki iliyopita Dk Hoseah alilalamikia sheria hiyo, hasa kifungu cha 37 na 57 akisisitiza kuwa ni mbovu kwa kuwa vinamzuia kuwafikisha watuhumiwa wa rushwa kubwa mahakamani. “Tusaidieni sheria hii ibadilishwe ili iweze kuturuhusu kufanikisha kupambana na rushwa nchini,” alisisitiza Dk Hoseah.

Hata hivyo, jana Werema alipinga dhana hiyo na kusema kwamba siyo sahihi kuipa Takukuru mamlaka yote; kutuhumu, kupeleleza na kushtaki kwa kuwa kufanya hivyo ni kinyume na demokrasia, Katiba na utawala wa sheria.

Kumrundikia mtu au taasisi moja mamlaka zote hizo, ni kinyume na misingi ya utawala bora, alisema.

"Haiwezekani mtu (Dk Hoseah) akawa na mamlaka ya kupeleleza na kushtaki, halafu Mahakama ikiwaachia huru watuhumiwa, atasema siyo mimi ni kosa la Mahakama, We can't do that! (hatuwezi kufanya hivyo)," alisema Werema na kuongeza:

"Mimi nakubaliana na kitu kimoja, kila mamlaka iwe na kigingi. Iwe Mamlaka ya Rais, Bunge au Mahakama, lazima kuwe na chombo cha ku-check and balance," alisema Jaji Werema.

Kauli hiyo ya Jaji Werema imekuja siku chache tangu Mkurugenzi wa Mashtaka, (DPP) Eliezer Felishi kukiri kwamba kazi ya kuwafikisha watuhumiwa hao mahakamani ni yake, lakini kesi nyingi zinakwama.

DPP Feleshi alisema ucheleweshaji wa kesi za rushwa kupelekwa mahakamani, unatokana na kukosekana kwa ushahidi wa kutosha. "Ikifikia hapo, nalazimika kuyarudisha mafaili hayo kwa Takukuru," alisema.

"Mimi nafanya kazi kwa kufuata sheria na taratibu zilizowekwa na Serikali. Siwezi kufanya kazi kwa sababu mtu fulani ametaka nifanye. Jambo hilo linaweza kuniletea matatizo baadaye," alisema na kuongeza:

"Kutokana na hali hiyo, siwezi kupeleka mahakamani jalada ambalo halijakamilika. Sheria inanipa siku 60 niwe nimepeleka kesi mahakamani, lakini kama ushahidi haupo cha kufanya ni kurudisha Takukuru faili.”

Madai ya Dk Hoseah
Awali Dk Hoseah alisema anajua matarajio ya wananchi ni makubwa kwa Takukuru, lakini sheria imewafunga mkono kwa kuwa hawawezi kuchukua uamuzi dhidi ya kesi kubwa za ufisadi bila ushauri wa DPP.

“Sina mamlaka ya kumpeleka mtuhumiwa wa rushwa kubwa mahakamani. Uwezo wangu ni kupeleka walarushwa ndogondogo tu na kwamba kazi yangu ni kuchunguza tu,” alisema Dk Hoseah na kuongeza;

“Sheria yetu imetufunga mikono kwa kuwa kumpeleka mtu mahakamani siyo uamuzi wangu, bali ya DPP.”

Awali Dk Hoseah alisema sheria hiyo katika kifungu cha 57 inamzuia kuwapeleka mahakamani watuhuhumiwa wakubwa wa rushwa, mpaka awafikishe kwa Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP).

Kifungu hicho cha 57 (1) kinasema kuwa shtaka lolote la kosa lililoelezwa kwenye Sheria ya Takukuru lazima lifunguliwe kwa ruhusa ya maandishi kutoka kwa DPP. Kifungu cha 57 (2) kinamtaka DPP ndani ya siku 60 kutoa au kukataa ruhusa ya kushtakiwa.

Dk Hoseah alisema, hiyo ni moja ya changamoto zinazoikabili taasisi yake na kwamba wananchi wasubiri mabadiliko ya kiutendaji kama sheria itabadilika na kumruhusu kufanya hivyo.

Maelezo ya Dk Hoseah yanaungwa mkono na sehemu ya taarifa ya awali ya Mpango wa Nchi za Afrika wa Kujitathmini (APRM) ambayo inaeleza kwamba kikwazo cha ufanisi katika vita ya rushwa nchini Tanzania ni sheria inayowazuia Takukuru ipate kibali cha DPP kabla ya kufungua kesi kubwa za rushwa.

“Ni wala rushwa wadogo wadogo tu ndiyo wanaoweza kushtakiwa na Takukuru, lakini makosa makubwa ya rushwa yanayohusu viongozi au watu wa karibu na viongozi wakubwa ni mara chache sana kufunguliwa kesi mahakamani,” inasema sehemu ya taarifa hiyo na kuongeza:

“Mfumo huu ni kama unainyima mamlaka ya kiutendaji Takukuru na kimsingi, unakandamiza juhudi za chombo hiki kupambana na rushwa”.

Hii siyo mara ya kwanza kwa ofisi hizi mbili kuvutana kuhusu udhaifu katika sheria ya Takukuru, lakini mara zote Serikali imekuwa ikisisitiza kwamba lazima mashtaka kwa watuhumiwa wakubwa wa rushwa wapate yapate kibali cha DPP kabla ya kufikishwa mahakamani.

My take: Hivi kama kesi kubwa za rushwa lazima zipate kibali cha DPP, kwa nini TAKUKURU iruhusiwe kuwapeleka wala rushwa wadogo mahakamani bila kupata kibali toka kw Bwana DPP? Isitoshe kama TAKUKURU hawaruhusiwi KUTUHUMU, KUKAMATA, KUPELELEZA na KUSHTAKI... kwa nini POLICE wanafanya hivyo? Hivi waendesha mashtaka wa TAKUKURU na wa POLICE ni wapi ambao ni wanasheria (GRADUATES with LLB/LLM)?? Hivi Hosea kama Mwanasheria (PHD Holder) Kweli hawezi kujua au hana wataalamu wa kujua kuwa USHAHIDI uliopo unajitosheleza???

Hii ndiyo JMT kila kitu ni danganya toto. Inashangaza kumshitaki aliyeomba rushwa ya sh 10,000 lakini unashindwa kumshitaki aliyehongwa usd 1,000,000. Huku ni kulindana kwa viongozi wa magamba.
 
huyu si ndio alisema katiba ya jamhuri iko vizuri kabisa haiitaji kutengezwa upya.? Nchi ya vituko,rais kituko,pm kituko,madam spika kituko,AG kituko.!!
 
Mkuu hapa huelewi nini rushwa kubwa ni ile ambayo GAMBAZ wakikamatwa nayo, hapo consent ya DPP ni lazima. Lakini mimi na wewe tukikamatwa ni rushwa ndogo, HAPA HATUHITAJI CONSENT YA DPP

Haswaaaaaa,umenena mkuu
 
Back
Top Bottom