Mwanasheria halmashauri Arusha,atishwa na kasi ya chadema,aomba uhamisho | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanasheria halmashauri Arusha,atishwa na kasi ya chadema,aomba uhamisho

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Mwan mpambanaji, May 2, 2011.

 1. M

  Mwan mpambanaji JF-Expert Member

  #1
  May 2, 2011
  Joined: Apr 3, 2008
  Messages: 468
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Katika hali inayoonyesha kuogopa kasi ya madiwani wa chadema,mwanasheria wa halmashauri ya Arusha Bw Paul Mugasha,ameomba kuhamishwa ghafla,na sasa ataripoti Mwanga kwenye kituo kipya cha kazi.Hivi karibuni diwani mmoja wa chadema wa kata ya Levolosi alimweleza mwanasheria huyo kama mtu hatari kwa halmashauri na akasisitiza kuwa lazima ashughulikiwe kwa kuisababishia halmashauri hasara ya mamilion ya fedha.
  Huyu mwanasheria ameingia mikataba mingi ya kifisadi,ukiwamo ule wa soko la kilombero uliovunjwa kwa shinikizo kubwa kutoka kwa diwani huyo wa chadema kata ya Levolosi.mkataba mwingine ni wa car park kati ya Halmashauri na Kilimanjaro printers eneo la stend kuu ya mabasi ,unaokusanywa kwa masaa 24,ilihali halmashauri haipati mgao huo.Kampuni hii ilitishia kumshitaki diwani wa kata ya Levolosi Mh Nanyaro,kwa kuwakataza kukusanya ushuru eneo la stend ya Loliondo,katika sakata hili ndio huyu diwani akamweleza mwanasheria ufisadi wake na kwamba umefika mwisho.
   
 2. M

  Msharika JF-Expert Member

  #2
  May 2, 2011
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 936
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mchawi anakimbia anapogundua tunguli zimeishiwa nguvu. Big up diwani wetu, kwani amekimbilia mwanga ndio hatuwezi kumfuatilia aletwe arusha kwenye kesi. My Godness. Yahani hata hela ya wagonjwa wa Loliondo anakula?:help:
   
 3. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #3
  May 2, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Hata angeenda Mikoa ya kusini atafuatwa hukohuko,acha hapa Mwanga ya pua na mdomo. Lazima awajibishwe! Huu ni wkt wa UKOMBOZI!!
   
 4. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #4
  May 2, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Kama amesababisha ubadhirifu wowote hata huko alikokimbilia tutaenda kumnyofoa tu.
   
 5. nsimba

  nsimba JF-Expert Member

  #5
  May 2, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  hana anachokimbia, tutampata tu.
   
 6. T

  The GreatMwai Member

  #6
  May 2, 2011
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu ashughulikiwe ipasavyo kwa gharama yoyote ile. Heko diwani umeonesha kwamba unachukia ufisadi kwa kiwango cha juu sana songa mbele mpaka kielweke. Natamani angekuwa Manispaa ya Kinondoni huyu diwani maana ndo kuna ufisadi mkubwa kama huu wa kumlinda mkurugenzi kwa shilingi takriban milioni 90 na kuandaa uchaguzi wa CCM kwa zaidi ya shilingi milioni 40 huku hospitali ya Mwananyamala ikikosa dawa.
   
 7. N

  Ngandema Bwila JF-Expert Member

  #7
  May 2, 2011
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 1,000
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Du Kweli huyu mwanasheria anajua anachokifanya, amekimbilia Mwanga kule madiwani wote CCM, Wazee wakuungamkono hoja 100/100.
   
 8. Chepii

  Chepii Senior Member

  #8
  May 2, 2011
  Joined: Mar 7, 2011
  Messages: 102
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Hongera diwani kwa kazi nzuri nyota njema honekana asubuhi, Kero ya Parking Fee ktk Halmashauri ya Arusha imezidi kampuni zakukatsha ushuru wa Parking zimekua nyingi kila moja inatoza ushuru bilakuitambua nyingine pia wanatoza ushuru mpaka nje ya mji kwenye maeneo ya watu binafsi, chakusikitisha zaidi ni majina ya kampuni hizo ktk soko la kilombero kunakampuni moja inaitwa Piga Dili! ikiinia tu ktk soko hilo utakutana nao mlangoni.
   
Loading...