Mwanariadha wa Kenya Akatwa Miguu Baada ya Kuganda Kwenye Barafu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanariadha wa Kenya Akatwa Miguu Baada ya Kuganda Kwenye Barafu

Discussion in 'Sports' started by MziziMkavu, Dec 26, 2011.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Dec 26, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  [TABLE="width: 491"]
  [TR]
  [TD="colspan: 3"][/TD]
  [/TR]
  [TR="bgcolor: #E1E1E1"]
  [TD][​IMG]
  Marko Cheseto[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]


  Mwanariadha wa mbio ndefu toka nchini Kenya ambaye alipotea nchini Marekani wakati wa baridi kali na kupelekea miguu na mikono yake kuganda, amekatwa miguu yake yote miwili.


  Marko Cheseto mwenye umri wa miaka 28, alikutwa mbele ya hoteli huku viatu vyake vyepesi vya mazoezi vikiwa vimeganda kwenye miguu yake.

  Madaktari walishindwa kuvivua viatu hivyo kwa jinsi vilivyokuwa vimegandiana na ngozi ya miguu yake. Mikono yake pia ilikuwa imeganda sana.

  Cheseto alikuwa miongoni mwa wanariadha wa Kenya walioshiriki katika mbio za nyika na uwanjani katika chuo kikuu cha Alaska Anchorage UAA.

  Cheseto alikuwa mwanafunzi wa chuo hicho cha Alaska na alikuwa akishiriki mashindano kama mwanariadha wa chuo hicho.

  Cheseto alipotea jioni ya siku ya jumapili wakati huo theluji ilikuwa ikianza kuanguka taratibu.

  Cheseto alipatikana mapema siku ya Jumatano nje ya hoteli moja iliyopo karibu na chuo kikuu cha Alaska.

  Taarifa zilisema kuwa Cheseto ambaye alikuwa akisumbuliwa na stress za kujiua kwa rafiki yake wa karibu, alikuwa amevaa viatu vya michezo, koti jepesi na suruali ya jeans, lakini hakuwa na kofia au hata gloves za mikononi.

  Taarifa ya madaktari ilisema kuwa mikono ya Cheseto inatazamiwa kupata nafuu, lakini maeneo yake ya miguu ilipigwa na baridi kali mno na kulazimika kukatwa.

  Cheseto ataendelea kulazwa hospitali kwa matibabu zaidi.
   
 2. nachid

  nachid JF-Expert Member

  #2
  Dec 26, 2011
  Joined: Apr 14, 2011
  Messages: 898
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 45
  Mbona ize tu si wangemuweka kwenye oven kwa 2 hrs tu kwisha kabisa. NATANIA TU WANDUGU
   
Loading...