mgogoone
JF-Expert Member
- Dec 28, 2015
- 2,900
- 2,097
Wana jamvi Hongera za siku kuu
Olympic iliyofanyika Mexico City Mwaka 1968 ilituletea mashujaa wengi ambao waliwakilisha nchi zao Kwa kufanya vizuri katika mashindano Hayo.Watu wengi hawakumbuki Nani alishida nini au alifanya vizuri kuliko wote.mtu anayekumbukwa na ambaye hajapata ushindi ni mwanariadha MTanzania John Steven Akwari ambaye mpaka Leo anahamasisha watu Kwa UJASIRI NA WAJIBU WA KIBINAFSI KWA TAIFA LAKE kote isipokuwa Tanzania.John S.Akwari
Alitenguka mguu wakati wa mashindano alifungwa bandeji Na akaendelea kukimbia ilimchukua masaa manne kumaliza mbio za masafa marefu (Marathon).Uwanja wa watu laki ulibakia maelfu kadhaa.Alishangiliwa sana Kwa Ujasiri Na Uzalendo wa hali ya juu.Wanahabari walio bakia uwanjani wakamuuliza"Kwa nini unajihatarisha maisha yako wakati kila mtu anajuwa umeumia"?John Steven akajibu " sikutumwa Na nchi yangu mile 7000 kuja kuanza mashindano Ila nimetumwa kuja kumaliza" Hayo maneno mpaka Leo Hii watu wengi wanayatumia kuwaelimisha watu wasikate Tamaa Na maisha.
Je Kwa nini huyu Mzalendo haongelewi Kwa ujasiri wake? Anatuwakilisha Tanzania vizuri kabisa.Uzalendo,Ujasiri Na wajibu wa Kibinafsi umepotea nchi kwetu.
Je wewe unasemaje?