Mwananyamala hospitali jijini Dar mnavyowafanyia Wagonjwa si sahihi. Serikali mulika manesi wa hii hospitali

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,149
Na bahati kuna fani hata ukiaribu unajua pa kurekebisha

Unapokuwa nesi hii ni wito umebeba maisha ya watu

Nini kimetokea

Tulipeleka mgonjwa Mwanayamala siku nne zilizopita akaonekana anahitajika kusafishwa vidonda mguuni. Wakaandika madawa na vya kusafishia tukanunua vya 26000

Mchana ule wakamsafisha wakisema na kesho wanamsafisha..Tulipofika hospitali tulikutana na aibu. Daktari anasema vifaa havipo vya kumsafishia tukasema mbona tumenunua jana tukambiwa vitatosha na leo

Akaitwa nesi akakiri walipokea baada nesi mmoja anaomba msamaha vilitumika kwa wagonjwa wengine wanahisi walijichanganya

Anyway vidonda vimeanza toa harufu tukanunua vifaa vingine wakapewaa wamsafishe asbh yake ajasafishwa mchana tukaforce aondolewe maana hata baadhi ya manesi wengine walikuwa wanashauri pale atakufa kwa hao manesi wa shift hii mtamsahau mgonjwa wenu

Tulipowambia tunamhamishia hospitali nyingine wakaona aibu wakaja kumsafisha juujuu. Wakati wanaombwa vifaa vilivyobakia inapokelewa bandage moja tu...

Wakaulizwa zingine ziko wapi tulizonunua manesi wodi 5 surgical again bila haya wanasema wametumia jana usiku kuna mgonjwa atarudisha waliishiwa usiku

Ndugu zangu mnaopeleka wagonjwa pale jihadharani saba hasa hii wodi

1. Wanauza vifaa vya mgonjwa wako

2. Bla haya kama ujawapa hela mgonjwa wako hata dawa ulizonunua apewi wala chakula kama muda umepita

3. Nashauri uongozi kuhimiza awa manurse wavae majina na namba kabisa iwe visible mtu kujua nani amehusika na tukio fulani

4. Nashauri kuwepo na usimamizi maalum.Wodi 5 surgical wagonjwa wengi wanateseka manurse wanawaangalia.Wakati mwingine inabidi uwaonbe jaman mgonjwa yule anaomba msaada wanasema kwani atumsikii??

5. Nashauri mruhusu wagonjwa waliohoi wawepo msimamizi mmoja anaeshinda nae asubuhi mpaka asubuhi kuondoa manunguniko kwañn

Kuna mgonjwa tumekuta analalamika kwa ndugu zake jioni ajapewa chakula na chakula mchana ndugu walichelewa kidogo wakambiwa kiacheni tutampa yule mgonjwa hakupewa kabisa kabisa

Yapo matukio mengi. Mwanyamala serikali muangalie kuwahamisha hawa manesi wamezoea kazi

Kuna hili tukio lilinihuzunisha sana kabla ya wodi 5 mgonjwa alikuwa wodi moja upande wa kulia sikumbuki namba...Akaja mgonjwa mmoja manurse wakambiana huyu afikishi masamanne..Mkimbizieni oxygen

Mkaka wa watu akapewa oxygen siku ya kwanza huyo ya pili huyo yatatu huyoo akatolewa oxygen manurse awaamini wakanza ambiana kha yale masaa yamegeuka siku mungu apangiwi...Hataree sana sanaa

Kama unamgonjwa unajua yuko hoi ushauri tu peleka luganzila ama muhimbili

Lugalo wamempokea mgonjwa wanashanga vile vidonda na bahati kulikuwa na madaktari bingwa wakamsaidia wakandika na ripoti hali waliompokea nayo na kusema watawakilisha huko juu kupata maelekezo zaidi...

Manurse Mungu awasamehe sana hata kama mtakuja hapo bado heshimuni uhai wa mungu alietupa na nyie kuwepo hapo

Mbona hamna upendo kama manurse wenzenu wa Lugalo??

Tunatoa shukran nzima kwa wauguzi na madk wote wa lugalo waliompokea wapendwa wale watu wana Mungu wana hofu ya mungu...

Nimekaa masaa machache wanakuja wagonjwa kwenye gari wanawakimbilia na kutoa dir wapeleken pale wako nyuma na kumsaidia mgonjwa mmoja mmoja

Mungu awabariki sana saba uongozi mzima wa lugaloo hosp
 
P didy katika ubora wako! Ujumbe umefika lakini.
Kuna kijana wangu alizaliwa pale M,nyamala,mama yake hakupenda kabisa alikua matawi kataka Private. Mi nikamwambia tunaenda pale buku 50 tu utahudumiwa km Princess.
Na kweli mpaka leo hasahau,nilimfikisha usiku wa manane tunaambiwa hamna kitanda alale chini nikamvuta huyo nurse pembeni piga buku 50 enzi hizo balaa.baasi akasema subiri karekebisha kitanda na mashuka saafi kabisa kamchukua mgonjwa akanambia kaka we kalale ntakupigia simu mtoto akizaliwa.na kweli sa mbili and ndo anapiga kaka mfate mwanao umepata kidume na vigelegele anapiga.
Nyie acheni pesa hizi. Nilivyofika nikamlamba na buku 20 ingine akafie mbele.
Private ningepigwa km milioni hivi na maybe operation isiyotakiwa
 
Dah!
Tatizo la Ma Doctors na Nesi wa Mwananyamala kuchukua Rushwa, kunyanyapaa Wagonjwa halijaanza leo na bado hazijafanyika Tatuzi sahihi za kumaliza tatizo.

Kuna haja ya Wizara au Mamlaka ya Mkoa kulisimamia hili kidete, watu wengi wamepoteza maisha pale kwa Tamaa za watu.

Pia Wangewashurutisha Manesi wavae ile Beji yenye jina lake na Level yake, ili iwe rahisi kum report Nesi ambaye amekiuka Sheria, kuliko hii ya kusema Nesi toka Wodi no. 5....Manesi no wengi.

Kama kuna vitu Mkuu wa Mkoa Makonda angejaribu kushughurikia yeye mwemyewe na vingempa credit moja kwa moja basi ni huduma za Manesi kwa Government Hospitals hizi
 
P didy katika ubora wako! Ujumbe umefika lakini.
Kuna kijana wangu alizaliwa pale M,nyamala,mama yake hakupenda kabisa alikua matawi kataka Private. Mi nikamwambia tunaenda pale buku 50 tu utahudumiwa km Princess.
Na kweli mpaka leo hasahau,nilimfikisha usiku wa manane tunaambiwa hamna kitanda alale chini nikamvuta huyo nurse pembeni piga buku 50 enzi hizo balaa.baasi akasema subiri karekebisha kitanda na mashuka saafi kabisa kamchukua mgonjwa akanambia kaka we kalale ntakupigia simu mtoto akizaliwa.na kweli sa mbili and ndo anapiga kaka mfate mwanao umepata kidume na vigelegele anapiga.
Nyie acheni pesa hizi. Nilivyofika nikamlamba na buku 20 ingine akafie mbele.
Private ningepigwa km milioni hivi na maybe operation isiyotakiwa
Hiyo ni kawaida hospitali za serikali ukiwa na laki unazalishwa Kama malkia.
 
P didy katika ubora wako! Ujumbe umefika lakini.
Kuna kijana wangu alizaliwa pale M,nyamala,mama yake hakupenda kabisa alikua matawi kataka Private. Mi nikamwambia tunaenda pale buku 50 tu utahudumiwa km Princess.
Na kweli mpaka leo hasahau,nilimfikisha usiku wa manane tunaambiwa hamna kitanda alale chini nikamvuta huyo nurse pembeni piga buku 50 enzi hizo balaa.baasi akasema subiri karekebisha kitanda na mashuka saafi kabisa kamchukua mgonjwa akanambia kaka we kalale ntakupigia simu mtoto akizaliwa.na kweli sa mbili and ndo anapiga kaka mfate mwanao umepata kidume na vigelegele anapiga.
Nyie acheni pesa hizi. Nilivyofika nikamlamba na buku 20 ingine akafie mbele.
Private ningepigwa km milioni hivi na maybe operation isiyotakiwa
Akafie mbele haha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aisee poleni wahanga.Kiukweli sekta ya afya ina changamoto nyingi sana.
Hata wanafunzi wanaomaliza vyuo wanakuwa na moyo mzuri na ari ya kuisaidia jamii lakini akifika wodini anakuta mfumo umeoza ni rushwa! rushwa! rushwa!.
Ingewezekana ilitakiwa kila wodi wanapandikiza shushushu mmoja kama mgonjwa.watanaswa wengi na wataisha watakaobaki watatia adabu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana kwa yaliokukuta mana ni mazito kwa sana mkuu na naamini wahusika wanapita hapa Jf na naamini watalifanyia kazi. Pia naunga mkono ushauri uliotolewa na Mjumbbe mmoja wapo kua ni heri kungewekwa hata shushushu hata mmoja katika kila wodi ili awe anaweka mambo sawa na watu waanze kuthamini hospitali za serikali.

Ushauri kwa Manesi wenye tabia hizi kama mnaona kazi hamuitaki au mmeichoka basi andikeni barua ya kuacha kazi na waingie watu wengine kazin
 
Hii hospitali ya Mwananyamala kwa kweli huwa naiogopa sana yaani mara mia niende machakani kuliko pale, yaani toka enzi hizo ni ya matukio naiogopa vibaya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Issue sensitive kama hizi mkuu wa mkoa wala Waziri wa Afya hawezi kutatua ila ingekuwa ni swala la masifa wangeingilia kati ili wapate Kiki.!

Jamani ndugu zetu wanakufa hapo,serikali kimyaaa au kwa vile ndugu zenu mnatibia Agakhan?
Nidhamu 0,upendo 0.Hadi walinzi wanajiona kama Miungu pale.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna kisa.
Kuna wakati nikarejea Dar nikakutana na jirani yangu mdada. Nikamuuliza habari ya Watoto akaniambia alimpoteza Mtoto wake Mwananyamala Hospital. Mtoto wake alikuwa na tatizo la sickle cell, na linafahamika muda mrefu.

Siku moja kabla hajafariki alizidiwa na kupelekwa Mwananyamala Hos, wakafuata taratibu zote ikiwemo kuongezewa damu.

Wakaambiwa kuna baadhi ya dawa zinahitajika kununuliwa, wakati anarudi anakuta wameondoa 'drip' ya damu. Kwa maneno mengine hajawekewa kiwango cha damu kinachotakiwa.

Nesi/daktari wakasema haina tatizo japo kulikuwa na mashaka makubwa. Mama mtu kaenda nje kufuatilia baadhi ya dawa. Ile anaingia anakuta pazia limezungushiwa Mtoto kafariki. Alifanya vurugu kubwa sana.

Nawaasa wahudumu wa afya, kama unaona hauna huo wito tafuta kazi nyingine. Uhai una thamani kubwa sana. Kuna baadhi wakiona hata mgonjwa kafa kwa uzembe wao wala hawashtuki.

Wafikirie pia wao wanapofiwa maumivu wanayoyapata.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana kwa yaliyokukuta mkuu,2014 november nilimpoteza baba yangu mdogo hapo Mwananyamala hospital na unachokisema hapa naweza kuafikiana na wewe bila shaka yoyote,why nasema hivi?

Alipelekwa pale kama mgonjwa wa dharura,kitu ambacho nilifanikiwa kupata receipt ni ile kadi ya mgonjwa tu pale reception ila madawa yote biashala nilifanya na nurses kama chinga anavyouza bidhaa pale mtaa wa Congo,alipopelekwa wodini yakawa yale yale wakataka drip me nikauliza nikalipie wapi?wakacheka huku wakigongeshana viganja vya mikono wapo "hehehee huyu anataka kumsahau mtu hapa",nikiangalia faza anaumwa ikabidi nikubali nipigiwe hisabu kisha mmoja wao huku amepinda kiuno akakinga mkono nimpe pesa sikuwa na namna maana hata doctor anaemuangalia mgonjwa wangu yupo pale na sioni hata akikemea.

Akilini najiambia labda karatasi zangu nitapewa baadae mgonjwa akikaa sawa,siku ya pili asubuhi nilipoamkia pale nakuta mzee hajawekewa drip kumuuliza dawa umepewa anasema hapana nikenda kuwaambia ndo wakaenda kutafuta drip sasa sijui walizifuata store au vipi maana jana jioni wakati naondoka pale niliziacha kwenye meza ya kitanda cha mgonjwa wangu,kufupisha story tu nikwamba mzee alifariki ikabidi niwadai hela zangu maana dawa nilizonunua zote hakupewa hata kidogo na hela zenyewe hazikurudi hata cent.

Mortuary ndo nilikutana na balaa,wale jamaa kumbe wanaangalia kwanza ubini wa mtu maana nilipoenda kuhakikisha kama amehifadhiwa vizuri jamaa mmoja {alinikera mpaka jina namkumbuka somebody Athuman,mpare huyu jamaa} ananiambia najua huyu kwa asili atasafirishwa nimeshamchoma sindano na yupo kwenye jokofu tayari wakafungua kweli nikaona kisha akaniambia utalipa kiasi sikumbuki ila nilipouliza nikalipie wapi akamwambia mwenzake mtoe huyo {akimtaja jina} muweke huyo mwengine hapo chini huyu anataka apeleke puto kwao duh!kidogo jamaa nimkunje shati,hapa napo niliacha 77,500/= sikuwahi kuona risit yoyote!

Kwa ufupi wengi wanaofanya kazi pale hawana huruma na hawana wito wa kazi yao.

Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk
 
Back
Top Bottom