Mwanangu yupo njia panda athibitishe wapi kati ya UDSM na UDOM

Mwanangu yupo njia panda athibitishe wapi kati ya UDSM na UDOM

Angechaguliwa finance udsm ningeshauri aende udsm ila tourim mmmh!! Bora aende udom maana hata akienda udsm akitaka kuchange kozi hawatamkubalia... All in all mpe nafasi achague anapopenda kutoka moyon... Usije ukamchagulia au ukamlazimisha asome kozi bila yeye kuipenda...
Kuna ndugu yangu mmoja alimazaga kipindi hicho akachaguliwa udsm education na tumaini iringa law akaenda yudizimu kinachompata sasa anajuta
 
Mimi binafsi nilitaka aende Udsm lakini sijaridhika na hiyo program ila yeye anataka aende Udom hataki mahangaiko ya kupanga nje ya chuo.
Mpe anachopenda mkuu!! Ila mwambie kabisa kwa hii serikali ya vi wonder aanze kuwaza jinsi ya kujiajiri tokea akiwa chuoni na akiweza kama akimaliza aanze kuisaka CPA mapema!!
 
namshauri UDOM kwa sababu zifuatazo
1.Bcom Finance iko poa kwenye ajira hata kujiajiri
2.Ada ya UDOM ni nafuu kulinganisha na UDSM
3. uhakika wa kupata histel maana kuna hostel za kutosha.
3. Chuo kimeimprove sana toka kuanzishwa kwake na sasa kipo kwenye peak kiasi ha kuleta ushindani kwa vyuo vikongwe.
 
Mwambie aende UDSM

Kile chuo ukisoma pale na changamoto za mji zinakufanya uwe mahiri ata kujenge hoja suala la ajira sio big dili , big dili akasome afaulu vizuri atachaguwa cha kufanya.mwemyewe.
 
Nashukuru kwa ushauri wako wenye ufafanuzi
 
Mwambie aende UDSM

Kile chuo ukisoma pale na changamoto za mji zinakufanya uwe mahiri ata kujenge hoja suala la ajira sio big dili , big dili akasome afaulu vizuri atachaguwa cha kufanya.mwemyewe.
Ni kweli lakini duh program yenyewe siilewi vizuri.
 
Ni kweli lakini duh program yenyewe siilewi vizuri.
Swala ambalo watu wengine wanashindwa kukushauri ni je huyo mwanao anapendelea nn na alisoma nini? Hamna kitu kibaya kama Mtoto kupushiwa kuingia kwe kitu asichokipenda?
 
Mimi binafsi nilitaka aende Udsm lakini sijaridhika na hiyo program ila yeye anataka aende Udom hataki mahangaiko ya kupanga nje ya chuo.
Ni program mbili tofauti, aende akafanye kile roho yake inapenda. Tunawaelekeza vijana lakini uamuzi wa mwisho uwe wao wanakuwa na ownership na kile watakacho kwenda kufanya.
 
Boss...Tourism iko poa na hata finance iko poa ila katika labour market BCom Finance ina comparative high labour market power ukicompare na BCom Tourisms so in my side aende BCom Finance ... Pili cost analysis ya hio miji vyuo vilipo yan DSM na DOM ts better aende DOM akasome hio BCom Finance.
Mi nafikri angalie interest aliyonayo kwenye fani na prospects ya kozi kuliko unafuu wa gharama.
 
Mwanangu yupo kwenye kundi la multiple admission kwenye vyuo hivyo, kwa UDSM amechaguliwa B. com in Tourism and Hospitality Management na anatakiwa athibitishe tar. 10/Oct. na UDOM amechaguliwa B. Com in Finance,na anatakiwa athibitishe tifikapo tar. 08/Oct sasa wapi bora aka confirm?
Wenye ufahamu hizo program nahitaji ushauri unaomsaidia huyo mwanangu
Ni bora akasome Bcom Finance. Utalii ataishia kuja kubebea watalii mabegi wakati wanapandisha mlima Kilimanjaro. Nimesoma Bcom ya UDSM so naelewa vizuri what to be a Bcom graduate is...
 
mwambie aende udsm ila akifika abadili hiyo kozi
 
Licha ya kwamba Udsm is among of the best university in Africa hiyo hospitality atajuta sio nzuri aende finance udom otherwise kama ataenda Udsm halafu abadilishe course ahamie finance hili nalo linategemea wakimkubalia athithubutu kusoma hospitality take care naijua vizuri udsm
 
Nashukuru kwa wote waliochangia na kutoa ushauri. nimezingatia yote mlioshauri na kuyafanyia kazi.
 
Back
Top Bottom