Mwanangu ana kimeo, napaswa kufanya nini?

mapipando

JF-Expert Member
Jun 8, 2015
2,921
3,549
Habari wakuu,

Naomba niende kwenye mada, mwanangu ana umri wa miaka minne,juzi ndio tumegundua kuna kinyama kimening'inia kwenye koo (kimeo).

Na hili wazo la kumchunguza lilikuja baada ya kuwa na hali ya kukohoa mara kwa mara licha ya kuwa huwa tunampa dawa za kifua na kikohozi.

Nimejaribu kuzungumza na baadhi ya jamaa zangu juu ya tatizo hili na wao kusema kwamba huwa kuna watu wanakata kienyeji sasa mimi nimeamua kulileta hapa ili kupata ushauri.

Natanguliza shukrani zangu.
 
Hosiptali ipi wanakata kimeo?
Duh mkuu, mm nilikua naishi dar hapa tandika mbona wanafanya sana hivyo?? Hata mkoa niliokua naishi wanafanya sana kukata hivyo vitu, hio inatokea kwa watoto wadogo ila sio wote, mm nashkuru haikunitokea hio sote tuliozaliwa hme family nilipomuuliza bimkubwa aliniambia haikutokea tunashkuru ila watoto wa jirani nimeshuhudia wengi wanaenda kukatwa ni dakika 1 moja tu wala haina tabu kukata hio

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Baada ya kukata inachukua muda gani mtoto kupona na vipi kuhusu aina ya vyakula anavyopaswa kupewa na kutokupewa?
 
Kinapona haraka sana muda mfupi, mikate iliochanganywa na chai yaani iliovurugika milaini isiwe moto, uji nk , ukienda watakufahanisha vizuri vyakula
 
Duh mkuu, mm nilikua naishi dar hapa tandika mbona wanafanya sana hivyo?? Hata mkoa niliokua naishi wanafanya sana kukata hivyo vitu, hio inatokea kwa watoto wadogo ila sio wote, mm nashkuru haikunitokea hio sote tuliozaliwa hme family nilipomuuliza bimkubwa aliniambia haikutokea tunashkuru ila watoto wa jirani nimeshuhudia wengi wanaenda kukatwa ni dakika 1 moja tu wala haina tabu kukata hio

Sent using Jamii Forums mobile app
hakuna asiezaliwa na kilimi or kimeo ni vile unakuta hakimsumbui akiwa mdogo ila baadhi yao huja kusumbuliwa ukubwani na wengi huwa wanakata watoto wakiwa angali n wadogo wakiwa hata hawajitambui mimi nikiwa miongoni
 
Baada ya kukata inachukua muda gani mtoto kupona na vipi kuhusu aina ya vyakula anavyopaswa kupewa na kutokupewa?
inategemea na umri wa mtoto ila kama nikuanzia miaka mitano hakikisha unampa vitu vya motomoto chai ya tangawizi ni the best(vitu vyamoto vinapochoma hapo ndio kupona kwake) na hakikisha unamfunika maskio baridi isipenye
 
Mkuu kimeo ni anatomy ya kawaida ya binadamu......kuwa kikubwa sio shida au ugonjwa....ni marachache sana utaenda kwa daktari kwa ajili ya kukata kimeo....
Kikohozi cha mara kwa mara kwa watoto ni kawaida kwani kinga zao hazipo imara kukabiliana na vijidudu pale vitakapojitokeza.....
Kwahiyo mpeleke mtoto akatibiwe kikohozi na sio kukata kimeo.....
 
Habari wakuu,

Naomba niende kwenye mada, mwanangu ana umri wa miaka minne,juzi ndio tumegundua kuna kinyama kimening'inia kwenye koo (kimeo).

Na hili wazo la kumchunguza lilikuja baada ya kuwa na hali ya kukohoa mara kwa mara licha ya kuwa huwa tunampa dawa za kifua na kikohozi.

Nimejaribu kuzungumza na baadhi ya jamaa zangu juu ya tatizo hili na wao kusema kwamba huwa kuna watu wanakata kienyeji sasa mimi nimeamua kulileta hapa ili kupata ushauri.

Natanguliza shukrani zangu.
Very sad, kuna mdogo wangu kipindi tupo wadogo ilisemekana anahichokidude, wakampeleka kwa wataalam wakienyej wakakikata & sjui walikosea nini, mpaka leobwanamdogo hawaezi kuongea, uwezo wake pia wa kukontral ulimi wake ni mdogo na mara nyingi hua anajiumaulimi wakati wa kula. Udende unaflow mda wowote nahawezikuzuia.

Nahis kuna nerve waliikata wakati wanafanya hii huduma.

Jitahidi sana kuwaepuka hawa wanaojiita wataalam wa kienyeji. Wataharibu.
 
Mpe mtoto dawa ya minyoo kwanza kabla ya kumpeleka hospital kukata hiko kimeo. Ninaishi Dar sijawahi kuwakata vimeo watoto wangu. Kuna mmoja alionesha hizo dalili za kukohoa watu wakanishauri akakate kimeo lakini nilipoenda hospital walimpa dawa za minyoo na wakanisisitiza niwr na tendency ya kumpatia dawa za minyoo kwa interval inayoshauriwa kitaalamu ili kuepuka haya matatizo.
 
Mkuu kimeo ni anatomy ya kawaida ya binadamu......kuwa kikubwa sio shida au ugonjwa....ni marachache sana utaenda kwa daktari kwa ajili ya kukata kimeo....
Kikohozi cha mara kwa mara kwa watoto ni kawaida kwani kinga zao hazipo imara kukabiliana na vijidudu pale vitakapojitokeza.....
Kwahiyo mpeleke mtoto akatibiwe kikohozi na sio kukata kimeo.....
Hapa ndo najaribu kuwaza kwamba kimeo kinasababisha vipi hali hii ya kukohoa.

Ninachofahamu kukohoa kikohozi ni njia moja wapo ambayo njia ya hewa inatoa ute ute mzito uliokueko katika njia hiyo ya hewa kutokana na maambukizi mbali mbali.

Sijajua mpaka sasa kimeo kina mahusiano gani na tatizo aliloleta mdau hapa.
 
mkuu kama ulivyo sema......hakuna uhusiano hapo.....
kikohozi kikatibiwe mtu akijichanganya mtoto atakatwa kimeo kwa kutumia vifaa unsterile mwishowe aambukizwe magonjwa ya hatari
 
Very sad, kuna mdogo wangu kipindi tupo wadogo ilisemekana anahichokidude, wakampeleka kwa wataalam wakienyej wakakikata & sjui walikosea nini, mpaka leobwanamdogo hawaezi kuongea, uwezo wake pia wa kukontral ulimi wake ni mdogo na mara nyingi hua anajiumaulimi wakati wa kula. Udende unaflow mda wowote nahawezikuzuia.

Nahis kuna nerve waliikata wakati wanafanya hii huduma.

Jitahidi sana kuwaepuka hawa wanaojiita wataalam wa kienyeji. Wataharibu.
Kuna kimeo na udata. Huyo hakukata kimeo.
 
Tafuta specialist wa E.N.T yaani Masikio, Koona Pua

Wapo wengi tu kwenye mahospitali ya dar.
 
Mkuu dawa ni kukikata hicho kimeo! Kesi yako inafanana na ya mwanangu,ushauri niliopewa ilikuwa kumpeleka kwa mtaalamu wa kazi hiyo mtaani.
Nashukuru mara baada ya kukikata mwanangu haikumchukua zaidi ya siku kama mbili mwanangu akapona kabisa.
Sina hakika kama hospitali wanatoa huduma hiyo!
 
Kimeo kinakuwaje mkuu ?
 
Habari wakuu,

Naomba niende kwenye mada, mwanangu ana umri wa miaka minne,juzi ndio tumegundua kuna kinyama kimening'inia kwenye koo (kimeo).

Na hili wazo la kumchunguza lilikuja baada ya kuwa na hali ya kukohoa mara kwa mara licha ya kuwa huwa tunampa dawa za kifua na kikohozi.

Nimejaribu kuzungumza na baadhi ya jamaa zangu juu ya tatizo hili na wao kusema kwamba huwa kuna watu wanakata kienyeji sasa mimi nimeamua kulileta hapa ili kupata ushauri.

Natanguliza shukrani zangu.
Kwani kikohozi chake kikavu au kinatoa makohozi ?
 
Very sad, kuna mdogo wangu kipindi tupo wadogo ilisemekana anahichokidude, wakampeleka kwa wataalam wakienyej wakakikata & sjui walikosea nini, mpaka leobwanamdogo hawaezi kuongea, uwezo wake pia wa kukontral ulimi wake ni mdogo na mara nyingi hua anajiumaulimi wakati wa kula. Udende unaflow mda wowote nahawezikuzuia.

Nahis kuna nerve waliikata wakati wanafanya hii huduma.

Jitahidi sana kuwaepuka hawa wanaojiita wataalam wa kienyeji. Wataharibu.
Huyu aliyemkata hakuwa mtaalamu!
 
Back
Top Bottom