Habari za jioni wapendwa, naomba ushauri mwanangu miaka mitatu anasumbuliwa na kikoozi anakooa anakuwa mpaka Kama anakakamaa wakati mwingine na kutapika, hosp wamepima kifua Kiko vizuri na Hana dalili za pumu Ila wanasema ana maambukizi kwenye Koo kapewa dozi zaidi ya mwezi lakini Bado tatizo linapungua na kurudi nikirudi hosp wanamuongezea dozi nyingine, washauri wa mtaani wanakwambia ni kimeo hicho na hosp wanasema ndio kipo lakini wao hawakati ni dozi mpaka kinaisha Naona mwanangu anapata shida anazidi kunyongonyea tu. USHAURI ndugu zangu nikakate au niendelee na dozi? Asante I sana