Mwanangu amegongwa na Pikipiki

Lazima mtu awe na hasira kama za Galadudu na kuwapa hawa bodaboda funzo...hakikisha hiyo kesi inaenda mahakamani. Ameendesha kwa uzembe na kusababisha ajali kiasi cha kutishia maisha ya motto. Inampasa jela...ningejua hiyo hospitali ningeongea na Dr aandike ripoti nzuri ya kumtia mtu jela...wamezidi hawa nasi tunawachekea.
 
Last edited by a moderator:

Hiyo Baba yetu.....huwa naisali kila asubuhi na wakati wa kulala
 
Pole sana kaka yangu, shukuru Mungu mwanao anaendelea vizuri. Mi huku jana bodaboda kaua mtoto wa jirani yangu, hivi tunazika leo...........inauma sana jamani.

Ooh poleni sana Mungu amuweke mahali pema
 

...mkung'ute vilivyo kabla ya kumchukulia hatua za kisheria, maana akifika kituoni au baada ya hapo ukimbamiza itakula kwako....
 
Hiyo Baba yetu.....huwa naisali kila asubuhi na wakati wa kulala

Huonyeshi kuitii sala hii nawe wajiita ni mfuasi wake, umeigeuza hiyo sala kuwa ni wimbo kama wa bongo fleva sio?

Kwa kuwa bahati mbaya huongozana jiandae kuuona ukuu wa nguvu za Muumba wako.
 
eeeh hii kali yaani baba mtu mwanao kagongwa na pikipki jamii forum ndyo kimbilio jamani tumeisha, ni mtazamo tu bro, kuna mambo mengi ya msingi ya ku share na watu sio kila tukio la nyumbani kwako nasi tulijue.
 
eeeh hii kali yaani baba mtu mwanao kagongwa na pikipki jamii forum ndyo kimbilio jamani tumeisha, ni mtazamo tu bro, kuna mambo mengi ya msingi ya ku share na watu sio kila tukio la nyumbani kwako nasi tulijue.

Huo pia ni mtazamo wako mkuu sio mbaya
 
Galadudu pole mkuu ila mtoto akipona nadhani itabidi kuongeza uangalizi Mara dufu espcly wakati anaenda na kurudi shule kama sio mkubwa sana,mfundishe pia kuwa EXTRA CAREFUL awapo barabarani yaani bora beki3 au wewe/wife awe anamescort kama shule haiko mbali sana.Pole
 
Pole sana kwa ajali hiyo ya mwanao, hakuna mwenye leseni halali na kama aliipata hajui utaratibu na nidhamu za kuendesha, msamehe bure ila iachie serikali imhukumu
 
Pole sana

Pikipiki ni majanga

Nilishuhudia mmoja alimwingiza abiria wake chini ya uvungu wa prado (yeye mwenyewe aliruka) kwa kujifanya ana haraka kupita wakati magari yamesimama kumpisha aliyekuwa anatokea barabara nyingine
 
Nampa pole mzazi. Lakini ni kwa vipi hawa bodaboda hawafuati kabisa alama.za barabarani hata mbele ya polisi? Mimi hawa huwa wananikera sana kwa kweli.
 

Kumbe basi boda boda wengi hawana leseni ndo maana wanafanya vituko barabarani. Nina wasiwasi kama nyingi ya hizo pikipiki siyo za askari polisi.
 
Juzi maeneo ya sokoine university bodaboda kawagonga wanafunz 3 was drs3mmoja akafariki papohapo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…