Mkuu punguza hasira, usije 'jinunulia' murder case.Wamenigongea mtoto wangu asubuhi hii anavuka kwenda shule akiwa kwenye Zebra, magari yote yamesimama lakini yeye akajifanya ana haraka sana akaunga na baada ya kumgonga akataka kukimbia.
Sasa hapa tupo Hospitali, tukitoka hapa huyo jamaa nitamshughulikia mi mwenyewe, nna hasira nae sana.
Inawezekana ikawa huyo boda boda akawa miongoni ya wale boda boda waliotoka Mbarali na kusafiri kilomita 600 kwenda Dom, kwa lengo la kumshawishi mzee wa mamvi agombee Urais, na si ajabu akawa miongoni ya waliomchangia EL ile laki 6 ya kwenda kuchukulia fomu ya kugombea Urais.unataka kumshugulikia mpiga kura wa Lowassa...Bodaboda Republic
pole mkuu.. ila ukimkamata umpige tu, basi watakuja bodaboda 100 hapo kwako kuandamana bora umsamehe tu
Ndg zangu wana Jf mi nawashukuru wote mliomuombea mwanangu apate ahueni, ametibiwa......ndg wa aliyemgonga nao wamekuja, kwa kuwa hakuumia sana mtoto nimewaambia wanirudishie tu gharama zangu zote nilizotumia.
Kasheshe iliyopo sasa..... Kumbe aliyemgonga mtoto siyo anaetambuliwa kwa tajiri, yeye alipewa deiwaka tu na kibaya zaidi hana leseni, na yule anaetambulika kwa tajiri (aliyetoa deiwaka) nae pia hana leseni...... Kwa hiyo wote wamewekwa ndani kituo cha police kumsubiri mmiliki wa pikipiki
Mkuu punguza hasira, usije 'jinunulia' murder case.
Tumia taratibu za kawaida za kisheria, ingekuwa vyema uripoti tukio hilo kwenye Police Station ilyo jirani na hilo tukio lilipotokea.