Wana jamvi tujadili hii Nukuu ndogo tu iliyoandikwa na Mwananchi kuhusu ufisadi TAMISEMI
"Tumelazimika tena leo katika kipindi kisichozidi wiki mbili kuzungumzia ufisadi unaoendelea kuitafuna Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi). Mwishoni mwa mwezi uliopita, tulichapisha habari za kushtusha kwamba Sh644 milioni kati ya Sh35 bilioni zilizotolewa na wahisani kutoka nchi sita za Magharibi kugharimia awamu ya pili ya Mpango wa Maboresho ya Serikali za Mitaa (LGRP) zimetafunwa na mafisadi wizarani humo.
Tulisema nchi hizo sita za Sweden, Finland, The Netherlands, Ireland, Japan na Ujerumani kwa pamoja zimeitaka rasmi Serikali ya Tanzania kurejesha fedha hizo ambazo zilitumiwa vibaya na mafisadi katika wizara hiyo. Nchi hizo zimesema kila nchi itawasilisha barua ya madai serikalini na kwamba zinasikitishwa na hali hiyo iliyojitokeza kwa sababu kundi linaloumizwa ni la wananchi maskini."
Nchi hii ni yetu sote, namna hii ya ulaji haiwezi kamwe kuleta ustawi wa jamii yetu, watu wachache ambao wamejichukulia madaraka na uhalali wa kutafuna fedha za wananchi pasipo mashaka hawawezi kuvumilika kamwe.
katika mlolongo huu wa ulaji TAMISEMI WAPO wakurugenzi wa halmashauri ambao wamediriki hata kuwahamisha Internal Auditors ambao ni Waaminifu na ambao wamekuwa wakiwabana kwa hoja mbalimbali, wengine hata kufanyiwa timimg na kuibiwa laptop za kazini , na kushtakiwa polisi kwa wizi wa laptop na hatimaye mahakamani. Utashangaa kuona hata taratibu za kiutumishi kuhusu upoteaji wa laptop hazijafatwa wakati hiyo laptop ni less than 1million,wakati pengine Auditor huyu amehoji hoja nyingi kuhusu matumizi mabovu ya mamilioni ya Tsh pasipo action za kueleweka.
Haingii akilini kuona Mkurugenzi anapewa uhamisho, halafu anafanya makeke yake nadani ya miezi miwili tangu kuhamishwa anarudishwa kituo hicho hicho. this is the shame for the Tamisemi!!! Ni wakati wa kuondoa hawa ma internal auditor kuwajibika kwa Wakurugenzi, inabidi wawajibike kwa Chief Internal Auditor au RAS ( ingawa hapa ninawasiwasi pia maana kamfumo haka ka chama hiki cha CCM ni ulaji ulaji tu)
Asalaam Aleikum! Bwana Yesu Asifiwe!

- Mimi nasema ni wakati wa Wabunge wetu tuliowachagua wenyewe pasipo shuruti kwenda mbele zaidi na kuacha ushabiki wa vyama kufanya maamuzi magumu ya hawa MM katika TAMISEMI
- Pili niwakati wa Wananchi wa TZ wapenda maendeleo kuanza kufikiria mfumo mbadala mwaka 2015
Asalaam Aleikum! Bwana Yesu Asifiwe!