Mwananchi: UFISADI WAITAFUNA TAMISEMI

Shembago

JF-Expert Member
Aug 20, 2011
332
50
Wana jamvi tujadili hii Nukuu ndogo tu iliyoandikwa na Mwananchi kuhusu ufisadi TAMISEMI

"Tumelazimika tena leo katika kipindi kisichozidi wiki mbili kuzungumzia ufisadi unaoendelea kuitafuna Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi). Mwishoni mwa mwezi uliopita, tulichapisha habari za kushtusha kwamba Sh644 milioni kati ya Sh35 bilioni zilizotolewa na wahisani kutoka nchi sita za Magharibi kugharimia awamu ya pili ya Mpango wa Maboresho ya Serikali za Mitaa (LGRP) zimetafunwa na mafisadi wizarani humo.

Tulisema nchi hizo sita za Sweden, Finland, The Netherlands, Ireland, Japan na Ujerumani kwa pamoja zimeitaka rasmi Serikali ya Tanzania kurejesha fedha hizo ambazo zilitumiwa vibaya na mafisadi katika wizara hiyo. Nchi hizo zimesema kila nchi itawasilisha barua ya madai serikalini na kwamba zinasikitishwa na hali hiyo iliyojitokeza kwa sababu kundi linaloumizwa ni la wananchi maskini."

Nchi hii ni yetu sote, namna hii ya ulaji haiwezi kamwe kuleta ustawi wa jamii yetu, watu wachache ambao wamejichukulia madaraka na uhalali wa kutafuna fedha za wananchi pasipo mashaka hawawezi kuvumilika kamwe.

katika mlolongo huu wa ulaji TAMISEMI WAPO wakurugenzi wa halmashauri ambao wamediriki hata kuwahamisha Internal Auditors ambao ni Waaminifu na ambao wamekuwa wakiwabana kwa hoja mbalimbali, wengine hata kufanyiwa timimg na kuibiwa laptop za kazini , na kushtakiwa polisi kwa wizi wa laptop na hatimaye mahakamani. Utashangaa kuona hata taratibu za kiutumishi kuhusu upoteaji wa laptop hazijafatwa wakati hiyo laptop ni less than 1million,wakati pengine Auditor huyu amehoji hoja nyingi kuhusu matumizi mabovu ya mamilioni ya Tsh pasipo action za kueleweka.

Haingii akilini kuona Mkurugenzi anapewa uhamisho, halafu anafanya makeke yake nadani ya miezi miwili tangu kuhamishwa anarudishwa kituo hicho hicho. this is the shame for the Tamisemi!!! Ni wakati wa kuondoa hawa ma internal auditor kuwajibika kwa Wakurugenzi, inabidi wawajibike kwa Chief Internal Auditor au RAS ( ingawa hapa ninawasiwasi pia maana kamfumo haka ka chama hiki cha CCM ni ulaji ulaji tu)

  1. Mimi nasema ni wakati wa Wabunge wetu tuliowachagua wenyewe pasipo shuruti kwenda mbele zaidi na kuacha ushabiki wa vyama kufanya maamuzi magumu ya hawa MM katika TAMISEMI
  2. Pili niwakati wa Wananchi wa TZ wapenda maendeleo kuanza kufikiria mfumo mbadala mwaka 2015

Asalaam Aleikum! Bwana Yesu Asifiwe!

Wabunge wameendelea kuwang'ang'ania kooni Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, (Tamisemi), Hawa Ghasia wakiwataka wasisubiri kutimuliwa bali wapumzike nyadhifa zao kistaarabu kwa kushindwa kuwajibika.

"Inatakiwa kabla ya Mkutano huu wa Bunge kumalizika, mawaziri kadhaa hapa hawastahili kuwapo kwa kushindwa kuwajibika katika nafasi zao na hivyo kusababisha ufisadi na ubadhirifu kwa fedha za umma," alisema Mbunge wa Muhambwe, Felix Mkosamali (NCCR-Mageuzi), wakati akichangia mjadala wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa, Kamati ya Bunge ya Bajeti na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali jana.

"Huwezi kila mwaka wabunge wanakulalamikia waziri kuhusu rushwa katika wizara yako halafu hakuna hatua zozote zinazochuliwa kudhibiti hali hiyo…unastahili kuondolewa.

Alisema hata wafadhili waliotoa fedha zao Tamisemi kiasi cha Sh. milioni 600 na zikatafunwa wanamtaka Rais Jakaya Kikwete, amfukuze waziri kwa kushindwa kuwajibika.
"Sasa kama haya yote ya rushwa yanafanyika katika wizara yake, yeye (waziri) anafanya kazi gani, kwanini asipigiwe kura ya kutokuwa na imani naye.

"Spika unapaswa kuliongoza Bunge kumfukuza Waziri Mkuu kwa mujibu wa Ibara ya 52 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania…Waziri Mkuu anapaswa kupumzika kistaarabu sasa, Waziri Ghasi pia naye anapaswa kupumzika, lakini wakishindwa kufanya hivyo wenyewe hawa wote ni kupiga nje, kufukuza tu," alisema.

Mbunge wa Viti Maalum, Pauline Gekul, (Chadema), alisema ni vizuri Waziri Mkuu Pinda akaondoka mapema na mawaziri wake, lakini akaonya kwamba siyo vizuri kuwaondoa hao kwani hakutakuwa na wengine wenye nafuu kwa sababu ya mfumo uliowaweka madarakani ni huo huo, hivyo unapaswa kuondolewa.

"Hata tukiwaondoa hawa, tatizo linabaki pale pale, mfumo. Hawa wote hawafai, wananuka rushwa.…Dawa yao ni Watanzania kuwaondoa kwenye masanduku ya kura za uchaguzi," alisema.

Alisema kwa mfano, vitabu 2,546 vya makusanyo ya kodi mbalimbali katika halmashauri havijareshwa na ni fedha kiasi gani ambazo zimekusanywa kupitia vitabu hivyo, lakini kila wakati serikali inasema chakula hakitoshi kwani sungura mwenyewe ni mdogo.

"Hivi ni kweli Watanzania waangalie tu fedha zao zinavyoliwa…tatizo siyo kwamba fedha zetu ni chache ila ni chama ambacho kimekufa ganzi…kwanini waziri asiwajibike.

Lakini alisema, "haya yote yanavumilika ila wapo baadhi yetu ambao wameamua kuichagua CCM, sasa ni vema wakafanya maamuzi magumu…nchi yetu siyo maskini kiasi hicho, lakini siyo vizuri kuwaondoa hawa, tatizo ni mfumo wenyewe."

Baada ya Pauline kumaliza kujadili kamati hizo, Mnadhimu Mkuu wa Bunge, William Lukuvi, ambaye ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) alisimama na kusema, "nimemsikiliza mheshimiwa kwa muda mrefu, sikupenda kumkatisha nilitaka amalize kwanza mchango wake, lakini mchango wake wote umejaa matusi na lugha ya kuudhi, tunataka afute kauli yake."

Hata hivyo, Mbunge wa Nyamagana, Ezekia Wenje, (Chadema), aliposimama na alimtetea Pauline akisema katika mchango wake hakutoa matusi yoyote ingawa maneno yake yanachoma sana kwa upande mmoja wa CCM.

"Lukuvi ni mwongo na athibitishe na siyo vizuri kwa mzee kama yeye kutoa uongo bungeni," alisema na kutaka mwongozo wa Naibu Spika Job Ndugai, ambaye hata hivyo aliahidi kutolea ufafanuzi/majibu mwishoni mwa kikao hicho, lakini hakuweza kufanya hivyo.

Mbunge wa Mufindi Kaskazini, Mahmood Mgimwa, (CCM), alikiri kwamba kuna udhaifu na ubadhirifu serikalini na akataka hatua za msingi za kumaliza tatizo hilo zichukuliwe.

"Ni kweli kwenye matumizi mabaya ya fedha, Serikali ya CCM tunalalamikiwa," alisema.

CHANZO: NIPASHE
 
Wana jamvi tujadili hii Nukuu ndogo tu iliyoandikwa na Mwananchi kuhusu ufisadi TAMISEMI

"Tumelazimika tena leo katika kipindi kisichozidi wiki mbili kuzungumzia ufisadi unaoendelea kuitafuna Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi). Mwishoni mwa mwezi uliopita, tulichapisha habari za kushtusha kwamba Sh644 milioni kati ya Sh35 bilioni zilizotolewa na wahisani kutoka nchi sita za Magharibi kugharimia awamu ya pili ya Mpango wa Maboresho ya Serikali za Mitaa (LGRP) zimetafunwa na mafisadi wizarani humo.

Tulisema nchi hizo sita za Sweden, Finland, The Netherlands, Ireland, Japan na Ujerumani kwa pamoja zimeitaka rasmi Serikali ya Tanzania kurejesha fedha hizo ambazo zilitumiwa vibaya na mafisadi katika wizara hiyo. Nchi hizo zimesema kila nchi itawasilisha barua ya madai serikalini na kwamba zinasikitishwa na hali hiyo iliyojitokeza kwa sababu kundi linaloumizwa ni la wananchi maskini."

Nchi hii ni yetu sote, namna hii ya ulaji haiwezi kamwe kuleta ustawi wa jamii yetu, watu wachache ambao wamejichukulia madaraka na uhalali wa kutafuna fedha za wananchi pasipo mashaka hawawezi kuvumilika kamwe.

katika mlolongo huu wa ulaji TAMISEMI WAPO wakurugenzi wa halmashauri ambao wamediriki hata kuwahamisha Internal Auditors ambao ni Waaminifu na ambao wamekuwa wakiwabana kwa hoja mbalimbali, wengine hata kufanyiwa timimg na kuibiwa laptop za kazini , na kushtakiwa polisi kwa wizi wa laptop na hatimaye mahakamani. Utashangaa kuona hata taratibu za kiutumishi kuhusu upoteaji wa laptop hazijafatwa wakati hiyo laptop ni less than 1million,wakati pengine Auditor huyu amehoji hoja nyingi kuhusu matumizi mabovu ya mamilioni ya Tsh pasipo action za kueleweka.

Haingii akilini kuona Mkurugenzi anapewa uhamisho, halafu anafanya makeke yake nadani ya miezi miwili tangu kuhamishwa anarudishwa kituo hicho hicho. this is the shame for the Tamisemi!!! Ni wakati wa kuondoa hawa ma internal auditor kuwajibika kwa Wakurugenzi, inabidi wawajibike kwa Chief Internal Auditor au RAS ( ingawa hapa ninawasiwasi pia maana kamfumo haka ka chama hiki cha CCM ni ulaji ulaji tu)

  1. Mimi nasema ni wakati wa Wabunge wetu tuliowachagua wenyewe pasipo shuruti kwenda mbele zaidi na kuacha ushabiki wa vyama kufanya maamuzi magumu ya hawa MM katika TAMISEMI
  2. Pili niwakati wa Wananchi wa TZ wapenda maendeleo kuanza kufikiria mfumo mbadala mwaka 2015

Asalaam Aleikum! Bwana Yesu Asifiwe!

Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (Laac), imeilipua Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) kwa madai ya kuwa sehemu ya Mtandao wa Ufisadi serikalini.

Tamisemi inaongozwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Hawa Ghasia anayesaidiana na manaibu waziri wawili, Aggrey Mwanry na Majaliwa Kassim Majaliwa.

Halikadhalika kamati hiyo ya Bunge imesema, zipo dalili za wazi za kuwapo kwa mtandao wa kutisha wa kifisadi unawashirikisha baadhi ya watendaji wa halmashauri nchini, hazina na Tamisemi.

Tuhuma hizo zilitolewa Bungeni jana na Mwenyekiti wa Laac,Rajab Mbarouk wakati akiwasilisha taarifa ya hoja za kamati kuhusu hesabu zilizokaguliwa kwa mwaka wa fedha unaoishia Juni 30,2012.

Alisema bado kuna ubadhirifu,ufisadi na utovu wa nidhamu wa hali ya juu wa matumizi ya fedha za umma kutokana na Tamisemi kutosimamia ama yenyewe kuhusika moja kwa moja na ufisadi huo.

"Mfano mwaka 2011/12, Sh1.6 bilioni zilitumika nje ya bajeti iliyoidhinishwa katika halmashauri 38 na Sh2.6 bilioni zilihamishwa kutoka akaunti moja kwenda nyingine bila kurudishwa,"alisema.

Kamati hiyo imebaini kwamba upo mtindo wa Serikali kutuma kwa halmashauri kiasi kikubwa cha fedha kuliko kiasi cha fedha kilichoidhinishwa na Bunge katika fungu husika wakati wa upitishaji bajeti.

Kamati hiyo imetolea mfano wa Sh2 bilioni zilizotumwa Halmashauri ya Jiji la Tanga na Sh500 milioni zilizotumwa katika Halmashauri ya Mji wa Korogwe ikiwa ni zaidi ya kiasi kilichoidhinishwa na Bunge.

"Kitendo hiki ambacho kinafanyika kwa ushirikiano wa hali ya juu wa Hazina,Tamisemi na Halmashauri kinaashiria kuwapo mtandao wa kutisha wa kifisadi baina ya mamlaka hizo,"alisema.

Kamati hiyo imeituhumu pia Tamisemi inayoongozwa na Waziri Hawa Ghasia, kuwahamisha haraka watumishi wanaotuhumiwa kufanya ubadhirifu kutoka hamashauri moja kwenda nyingine.

"Kamati imebaini kwamba Tamisemi imekuwa ikitumia mtindo huu kuwalinda watumishi mafisadi ndani ya halmashauri na kuifanya kamati iamini Tamisemi ni sehemu ya mtandao huu,"imesema.

Mwenyekiti wa kamati hiyo alisema kwa makusudi,Tamisemi imekuwa ikieneza saratani hiyo ya ufisadi kwenye halmashauri nyingi iwezekanavyo na kuitaka Serikali kuachana na mtindo huo.

Kamati ya Bunge ya Bajeti, imeishauri Serikali kupunguza matumizi na kuongeza ukusanyaji mapato ili miradi ya maendeleo igharamiwe kwa asilimia 35 ya bajeti ya Serikali.

Akiwasilisha ripoti ya kamati hiyo Bungeni jana, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Andrew Chenge alisema kwa utaratibu wa sasa hakuna uwiano sawia kati ya matumizi ya kawaida na matumizi ya maendeleo.

Chenge ambaye pia ni Mbunge wa Bariad Magharibi(CCM) alisema, mwenendo wa deni la taifa si wa kuridhisha kutokana na kuongezeka kwa mikopo ya masharti ya kibiashara na malimbikizo ya riba.
 
Wana jamvi tujadili hii Nukuu ndogo tu iliyoandikwa na Mwananchi kuhusu ufisadi TAMISEMI

"Tumelazimika tena leo katika kipindi kisichozidi wiki mbili kuzungumzia ufisadi unaoendelea kuitafuna Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi). Mwishoni mwa mwezi uliopita, tulichapisha habari za kushtusha kwamba Sh644 milioni kati ya Sh35 bilioni zilizotolewa na wahisani kutoka nchi sita za Magharibi kugharimia awamu ya pili ya Mpango wa Maboresho ya Serikali za Mitaa (LGRP) zimetafunwa na mafisadi wizarani humo.

Tulisema nchi hizo sita za Sweden, Finland, The Netherlands, Ireland, Japan na Ujerumani kwa pamoja zimeitaka rasmi Serikali ya Tanzania kurejesha fedha hizo ambazo zilitumiwa vibaya na mafisadi katika wizara hiyo. Nchi hizo zimesema kila nchi itawasilisha barua ya madai serikalini na kwamba zinasikitishwa na hali hiyo iliyojitokeza kwa sababu kundi linaloumizwa ni la wananchi maskini."

Nchi hii ni yetu sote, namna hii ya ulaji haiwezi kamwe kuleta ustawi wa jamii yetu, watu wachache ambao wamejichukulia madaraka na uhalali wa kutafuna fedha za wananchi pasipo mashaka hawawezi kuvumilika kamwe.

katika mlolongo huu wa ulaji TAMISEMI WAPO wakurugenzi wa halmashauri ambao wamediriki hata kuwahamisha Internal Auditors ambao ni Waaminifu na ambao wamekuwa wakiwabana kwa hoja mbalimbali, wengine hata kufanyiwa timimg na kuibiwa laptop za kazini , na kushtakiwa polisi kwa wizi wa laptop na hatimaye mahakamani. Utashangaa kuona hata taratibu za kiutumishi kuhusu upoteaji wa laptop hazijafatwa wakati hiyo laptop ni less than 1million,wakati pengine Auditor huyu amehoji hoja nyingi kuhusu matumizi mabovu ya mamilioni ya Tsh pasipo action za kueleweka.

Haingii akilini kuona Mkurugenzi anapewa uhamisho, halafu anafanya makeke yake nadani ya miezi miwili tangu kuhamishwa anarudishwa kituo hicho hicho. this is the shame for the Tamisemi!!! Ni wakati wa kuondoa hawa ma internal auditor kuwajibika kwa Wakurugenzi, inabidi wawajibike kwa Chief Internal Auditor au RAS ( ingawa hapa ninawasiwasi pia maana kamfumo haka ka chama hiki cha CCM ni ulaji ulaji tu)

  1. Mimi nasema ni wakati wa Wabunge wetu tuliowachagua wenyewe pasipo shuruti kwenda mbele zaidi na kuacha ushabiki wa vyama kufanya maamuzi magumu ya hawa MM katika TAMISEMI
  2. Pili niwakati wa Wananchi wa TZ wapenda maendeleo kuanza kufikiria mfumo mbadala mwaka 2015

Asalaam Aleikum! Bwana Yesu Asifiwe!

Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (Laac), imeilipua Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) kwa madai ya kuwa sehemu ya Mtandao wa Ufisadi serikalini.

Tamisemi inaongozwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Hawa Ghasia anayesaidiana na manaibu waziri wawili, Aggrey Mwanry na Majaliwa Kassim Majaliwa.

Halikadhalika kamati hiyo ya Bunge imesema, zipo dalili za wazi za kuwapo kwa mtandao wa kutisha wa kifisadi unawashirikisha baadhi ya watendaji wa halmashauri nchini, hazina na Tamisemi.

Tuhuma hizo zilitolewa Bungeni jana na Mwenyekiti wa Laac,Rajab Mbarouk wakati akiwasilisha taarifa ya hoja za kamati kuhusu hesabu zilizokaguliwa kwa mwaka wa fedha unaoishia Juni 30,2012.

Alisema bado kuna ubadhirifu,ufisadi na utovu wa nidhamu wa hali ya juu wa matumizi ya fedha za umma kutokana na Tamisemi kutosimamia ama yenyewe kuhusika moja kwa moja na ufisadi huo.

“Mfano mwaka 2011/12, Sh1.6 bilioni zilitumika nje ya bajeti iliyoidhinishwa katika halmashauri 38 na Sh2.6 bilioni zilihamishwa kutoka akaunti moja kwenda nyingine bila kurudishwa,”alisema.

Kamati hiyo imebaini kwamba upo mtindo wa Serikali kutuma kwa halmashauri kiasi kikubwa cha fedha kuliko kiasi cha fedha kilichoidhinishwa na Bunge katika fungu husika wakati wa upitishaji bajeti.

Kamati hiyo imetolea mfano wa Sh2 bilioni zilizotumwa Halmashauri ya Jiji la Tanga na Sh500 milioni zilizotumwa katika Halmashauri ya Mji wa Korogwe ikiwa ni zaidi ya kiasi kilichoidhinishwa na Bunge.

“Kitendo hiki ambacho kinafanyika kwa ushirikiano wa hali ya juu wa Hazina,Tamisemi na Halmashauri kinaashiria kuwapo mtandao wa kutisha wa kifisadi baina ya mamlaka hizo,”alisema.

Kamati hiyo imeituhumu pia Tamisemi inayoongozwa na Waziri Hawa Ghasia, kuwahamisha haraka watumishi wanaotuhumiwa kufanya ubadhirifu kutoka hamashauri moja kwenda nyingine.

“Kamati imebaini kwamba Tamisemi imekuwa ikitumia mtindo huu kuwalinda watumishi mafisadi ndani ya halmashauri na kuifanya kamati iamini Tamisemi ni sehemu ya mtandao huu,”imesema.

Mwenyekiti wa kamati hiyo alisema kwa makusudi,Tamisemi imekuwa ikieneza saratani hiyo ya ufisadi kwenye halmashauri nyingi iwezekanavyo na kuitaka Serikali kuachana na mtindo huo.

Kamati ya Bunge ya Bajeti, imeishauri Serikali kupunguza matumizi na kuongeza ukusanyaji mapato ili miradi ya maendeleo igharamiwe kwa asilimia 35 ya bajeti ya Serikali.

Akiwasilisha ripoti ya kamati hiyo Bungeni jana, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Andrew Chenge alisema kwa utaratibu wa sasa hakuna uwiano sawia kati ya matumizi ya kawaida na matumizi ya maendeleo.

Chenge ambaye pia ni Mbunge wa Bariad Magharibi(CCM) alisema, mwenendo wa deni la taifa si wa kuridhisha kutokana na kuongezeka kwa mikopo ya masharti ya kibiashara na malimbikizo ya riba.
 
Tamisemi wanakera sana, mfano mdogo Mkuranga, idara ya mipango ina wachumi 6, wawili wana experince ya more than 8 yrs, lakini cha ajabu idara inaongozwa na afisa maendeleo ya jamii II anaekaimu mwaka wa nne huu sasa haipendzi kwa kweli na inatia uchungu
 
Back
Top Bottom