Mchengerwa: Ubadhilifu unaotajwa Mitandaoni Kufanyika Tamisemi ulitokea Kati ya Mwaka 2017 hadi 2021 na Wahusika wako mahakamani!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,000
142,027
Waziri wa Tamisemi mh Mchengerwa amesema Wizi unaotajwa Kufanyika Tamisemi ulitokea kuanzia 2017 hadi 2021

My take: Jafo aliupiga mchache

====
"Mh. Rais naomba nikuthibitishie, hakuta wakati ambapo ofisi yako TAMISEMI imefanya kazi kubwa ya kushughulika na Kero za wananchi kama wakati huu, naomba nikuthibitishie watendaji wamefanya kazi kubwa na kazi nzuri sana, lakini sisi chini ya ofisi yako tumeendelea kuhakikisha kwamba tunasimamia nidhamu, uwajibikaji, na pale pote ambapo kumetokea na changamoto hakuna wakati ambapo tumechukua hatua kali hasa kwa watumishi wazembe, wala rushwa lakini kwa wale ambao wanafanya kazi kwa mazoea kama wakati huu tangu uliponiteua katika nafasi hii October 2023.

"Kumekuwa na taarifa nyingi baadhi ya watu wakiandika mtandaoni hasa eneo kuhusu hili la ubadhirifu, Mh. Rais naomba nikuthibitishie taarifa nyingi ambazo zimeandikwa sasa katika mitandao ya kijamii ni matukio ambayo yalitokea katika kipindi cha mwaka 2017-2021.

Naomba nikuthibitishie watendaji wote ambao wamekuwa wakitajwa kushiriki katika shuguli mbalimbali za ubadhirifu, nilipoingia katika nafasi hii tulichukua hatua kali kuwasimamisha kazi hatua za kinidhamu na wngi wao wapo mahakamani na kesi zao zinaendelea mahakani.

Na sisi tumeshawaeleza watendaji wote hatustasita kuendelea kuchukua haatua kali za kinidhamu dhidi ya watendaji wenye utendaji wa kimazoa na kukwamisha utekelezaji wa shughuli mbalimbali ambazo Mh. Rais unadhamiria kuhakikisha kwamba Watanzania wanapatiwa huduma bora katika maeneo yetu.."
- Mchengerwa

 
20240119_163744.jpg

Wewe mkwe nyamaza
 
Back
Top Bottom