Mwananchi Communications inatumika na Rwanda?

Mwananchi Communications inatumika na Rwanda?

jMali

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2010
Posts
8,412
Reaction score
5,013
New times Rwanda ni gazeti linalomilikiwa na idara ya usalama wa taifa ya Rwanda. Ukiacha kazi ya kuipigia "promo" (pr) serikali ya RPF, vile vile linatumika kuchafua wapinzani wa rais kagame na kuhalalisha mauaji yao. Hata kwenye website yao, sehemu ya kuwahusu wamiliki inasomeka "its being updated" toka 2011! Lakini ukweli wa nani anamiliki na kuendesha new times Rwanda unapatikana kwenye chapisho hili ambalo waandishi wake ndio hawa wanaowindwa na kuuwawa kiajabu ajabu katika nchi ambazo wanaishi in political exile, kama vile Col. Karegeya etc.

"The RPF owns the daily newspaper, The New Times . However, The New Times is managed by the
intelligence services rather than Tri -Star Investments, the RPF's flag -ship holding company."

Source: Rwanda briefing, footnote page 25. Walioandika hii ni waliokuwa viongozi wa juu wa RPF, hivyo wanajua kiundani nani hasa anaendesha gazeti hili la "chama".

Inasikitisha kuona gazeti mahiri kama citizen likitumika na idara ya usalama wa taifa ya Rwanda kumchafua mpinzani paul rusesabagina, mmoja wa waanzilishi wa chama cha RNC anayeishi ukimbizini marekani. Citizen imechapisha makala toka new times Rwanda kama ilivyo hapa.Revealed: The other side of Hotel Rwanda - National - thecitizen.co.tz.

Haishangazi kuona Rwanda inatumia magazeti ya nje kupiga propaganda zake, wamekuwa wakifanya hivyo muda mrefu. Kinachoshangaza ni jinsi Mwananchi communications ilivyojishusha hadhi kwa kutumika na serikali ya Rwanda namna hii! Nilitegemea kama hili lingetokea Tanzania, basi ni kampuni nyingine ya habari ndio ingetumika, lakini sio Mwananchi ambayo inasifika kwa weledi wake. Je tutegemee nini tena toka Mwananchi communications? Makala zingine toka new times dhidi ya theogene rudasingwa, david himbara, na wapinzani wengine?
"Since 2009, the RPF has worked with American and British PR specialists whose primary task is to drown out the voices of foreign critics and bury evidence of the RPF's human rights abuses under rosy language about political stability, economic growth, and the stated intention of helping the poor."

Source: Rwanda’s Twitter-Gate: The Disinformation Campaign of Africa’s Digital President â€" By Susan Thomson | African Arguments

Richard mgamba na waandishi wa aina yake:

Mhariri wa sasa wa citizen, Richard mgamba aliwahi kuwasafisha M23 (ambayo ripoti ya UN mwaka huu imeweka wazi kuwa walikuwa ni askari wa Rwanda) enzi zile akiwa IPP, aliwezeshwa kufika mpaka msituni na kufanya mahojiano na kiongozi wa waasi sultani makenga, kilichofuatia ni makala iliyojaa propaganda zile zile unazoweza kuzipata toka serikali ya Rwanda leo hii, kama ku-discredit reports za UN dhidi ya Rwanda, kuwapamba waasi wa M23 kuwa ni wapigania uhuru n.k makala hii hapa. Home
Leo hii amehamia citizen na tunaanza kuona articles kwenye magazeti ya Citizen, toka kwa wenzake kama Andrew mwenda wa Uganda. Na sasa kama haitoshi citizen sasa imeanza ku-source makala toka new times Rwanda! Na hivyo kimsingi kutumika kama mouthpeace ya kagame in Tanzania. Aibu hii ya Citizen ni pigo kwa tasnia ya habari nchini.

Nyuma yake nahisi kuna mambo kama haya ya mwandishi mwenzie Andrew mwenda wa uganda:

source:Andrew Mwenda is on Kagame's payroll and unethical journalist | Ugandans-At-Heart

Mtu huyu Andrew mwenda naye makala zake zimekuwa zikichapishwa na gazeti la citizen hivi karibuni kama "Citizen correspondent".
 
Uuuummh Juma Pinto and Jambo Leo newspaper?Natania,Byeeee!!!!
 
Bdo sana kuamini ulichokiandika kwani ktk magazeti yanayoaminika sana kwa kutoa habari za uhakika ni mwananchi wapo vizuri na hawapendelei upande wowote ule kisiasa hapa tz au hata nje ya tz....
 
Huyu mwandishi anataka citizen waandike propaganda kama habari Leo?
 
Huyu mwandishi anataka citizen waandike propaganda kama habari Leo?

Msihangaike na hii interahamwe jmali,yeye sikuzote anataka news ambazo ziko negative kwa rwanda,hapendi postive news kwa serikali ya pk,pole sana jmali,mwaka huu utachizi.
 
Bdo sana kuamini ulichokiandika kwani ktk magazeti yanayoaminika sana kwa kutoa habari za uhakika ni mwananchi wapo vizuri na hawapendelei upande wowote ule kisiasa hapa tz au hata nje ya tz....

hicho ndicho kinachosikitisha, heshima yao imeshuka vibaya mno kwa kuingiliwa na hawa mamluki.
 
Huyu mwandishi anataka citizen waandike propaganda kama habari Leo?

we hujaelewa thread kabisa, swala ni kwamba citizen haijaandika bali imekopi na kupaste habari za propaganda toka gazeti la Rwanda linalomilikiwa na Usalama wa taifa wa Rwanda! Yani kwa maneno mengine ni mfano gazeti la kenya linaloheshimika kukopi-paste habari za hilo habari leo.
 
jMali unatia huruma ndugu yangu. You are so immersed in your hatred for Kagame that you refuse to be rational. Mbona This Day walipo-copy uongo kuhusu Kagame majuzi hukulalamika? Acha double standards.
 
Mtu huyu Richard Mgamba. Alikuwa mwandishi wa mtaani huko Mwanza. Aliwahi kuruka ukuta pale ukumbi wa Ghandi akikimbia PCB wakiwa na mwenzake marehemu Vunjabei. Mgamba ambaye mara ni Mkurya mara Mhaya mara Mkenya? Mgamba wa minofu ya samaki, mapanki na M-23. Mgamba na maandamano ya mapanki Mwanza! Ilifika mahali baadhi ya wadadisi wakahoji nani anatuma taarifa za Tanzania kwa serikali ya Kagame? Ukweli habari zinazohaririwa ama kuandikwa na Mgamba ni zaidi ya habari, nyuma ya pazia kuna jambo. Ila hamko sahihi kudai hiyo ndo sera ya Mwananchi Communcations kama kampuni, mnatuonea sana. Hiyo ni sera ya tumbo la Mgamba. Ipo siku mtamjua mtu huyu.
 
Mkuu naona ulikuwa unamaanisha kumwambia jMali. Mimi sioni hatia juu ya gazeti la Mwananchi.
 
jMali unatia huruma ndugu yangu. You are so immersed in your hatred for Kagame that you refuse to be rational. Mbona This Day walipo-copy uongo kuhusu Kagame majuzi hukulalamika? Acha double standards.

wewe kwanini unashindwa kuuleta? lete hiyo habari na sema kwa nini iko biased, don't assume watu wanasoma kila gazeti. si unaona mimi nimeleta kila kitu? na wewe fanya hivyo!
 
wewe kwanini unashindwa kuuleta? lete hiyo habari na sema kwa nini iko biased, don't assume watu wanasoma kila gazeti. si unaona mimi nimeleta kila kitu? na wewe fanya hivyo!

Unlike you, I do not dignify cheap propaganda neither do I wish to waste time and space inundating JF with lengthy quotes that only further the enemy's cause. JF is for great thinkers; people who can discern matters and think for themselves and not plagiarizers who can't think for themselves and rely on biased source to form their opinion.
 
Binafsi jamaa huyu nilisha mshitukia siku nyingi tu, tangu yupo IPP: I hope vyombo vinavyo husika vitamuweka kwenye darubini kali. Mwenda wa Uganda huyo anajulika yupo kwenye payroll ya nani, watu weledi hapa walishtoa kivuli(phocopy) ya malipo yaliyo idhinishwa na Serikali ya Rwanda kumlipa Mwenda!!! Huyu wa Tanzania ndiye tunapaswa kumfatilia kwa karibu sana, sitaona hajabu kama naye hajanasa kwenye intricated web ya PK'S goodies JAR na kugeuzwa his MASTER'S VOICE!!! PK ana AKILI sana, anajua vilivyo kuwachezea/kuwatumia binadamu wenye njaa kali kifedha na kuwageuza his Babie Dolls - wanapewa Govt handouts/script wanazichapisha kwenye media RAW bila ya kutafakali kwa udani malengo ya G.O.R, kibaya zaidi hata editors hawa hoji chochote!! Alafu waadishi wa namna hiyo wanajipachika majina ya kubuni tu ili wapate credibility wanazuga watu eti "INVESTIGATIVE JOURNALISM" my foot!
 
Mkuu naona ulikuwa unamaanisha kumwambia jMali. Mimi sioni hatia juu ya gazeti la Mwananchi.

Ni kweli gazeti la Mwananchi alina hatia lakini kwa nini wasiwe makini na wadishi wenye utata kidogo, jaribu kusoma makala zake za nyuma alipo kuwa IPP - jamaa huyu ana an hidden AGENDA si bure.
 
Unlike you, I do not dignify cheap propaganda neither do I wish to waste time and space inundating JF with lengthy quotes that only further the enemy's cause. JF is for great thinkers; people who can discern matters and think for themselves and not plagiarizers who can't think for themselves and rely on biased source to form their opinion.

If you claim something why don't you back it up? sasa tutaaminije kuwa kweli This day ina matatizo na kagame bila ushahidi? mimi nimetuhumu na nimetoa the exact article i have a problem with, nimetoa historia ya mhusika with links, wewe sio tu unataka kuhamisha mjadala, bali unafanya hivyo pasipo kutaka kuulizwa chochote!
 
Back
Top Bottom