TANZIA Mwanamuziki mkongwe, Said Mabera afariki dunia

Ametutoka alfajiri ya kuamkia leo kwa Maradhi ya muda mfupi

Alikuwa Kiongozi wa bendi ya Msondo Ngoma na atapumzishwa leo saa 10 Maeneo ya Goba
FB_IMG_16013733483627361.jpg
 
Mungu ndio ajuaye siri ya kifo,Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema!
 
Jana usiku tulikua tunaangalia wimbi wa msondo ngoma unaitwa kwenye penzi hapa kosi tenzi. Yule jamaa mfupi kibonge na Mzee Mabera tulimjadili kua ndio mkongwe aliyebaki. Kumbe ndio ulikua usiku wake wa mwisho. Apumze kwa amani kwakweli.
 
Nitakwenda na naani msondo ngooma, nitacheza na nani magoma kitakita.
Kalale mahali pema .
Athumani Momba,
Selemani Mbwembwe,
Maina,
TX Moshi William,
Muhidin Maalim Ngurumo na leo
Said Mabera.
Bila kunsahau Suleyman Mwanyiro (Computer) . Duu kweli dunia ni mapito!! Pumzika kwa amani mzee Mabela!
 
Baraza la Sanaa,tunaomba muhifadhi kumbukumbu za Wanamuziki wa miaka ya enzi hizo.
Maana miziki ya zamani ilikuwa na maneno yenye vionjo ambavyo mpaka leo havijafikiwa.
Tena ingesaidia wasanii wa sasa wapate pa kuanzia,na kuacha kuiga miziki ya NAIJERIA.
"Kuna bendi mmoja ilishawahi imba wimbo wenye "kuomba pawepo na jela ya mapenzi"(Hii jela ingekuwepo wapenzi wa kizazi hiki wengi wapelekwa kwenye jela hii.
 
'Dally Kimoko Virus' anamaliza sana 'Wanamuziki' na sasa baada Kumaliza 'Kupukutisha' hawa wa Msondo zamu ya FM Academia na Twanga yaja.
Sio kweli mkuu jamaa umri ulienda sana pia feg na konyagi alipiga sana nilimuona last timu pale dar safari pak buza
 
Jana usiku tulikua tunaangalia wimbi wa msondo ngoma unaitwa kwenye penzi hapa kosi tenzi. Yule jamaa mfupi kibonge na Mzee Mabera tulimjadili kua ndio mkongwe aliyebaki. Kumbe ndio ulikua usiku wake wa mwisho. Apumze kwa amani kwakweli.
Penye penzi hapakosi tenzi, wakale walisema na huwezi kula muwa bila kukuta fundo. Huu wimbo unaniacha hoi saana. Wewe utakua mpenzi wa msondo mwenzangu. Najua utakua unakunywa safari na Ni mshabiki wa timu kongwe. Dar es Salaam Young Africans.
 
Msondo ngoma kuna jamaa walikuaga wanaimbaga "Mabela, Mabela, Mabela, Mabela" jamaa analikung'uta gitaa...
 
R.I.P mabera. Sema tune ya gitaa lake litapotea ila ukitaka ujue muziki ama melody ya muziki wa msondo ipo katika vidole vya Abdul Ridhiwani Pangamawe huyu alifundishwa gitaa na Kassimu Mbwana Mponda. Na kinanda alifundishwa na Waziri Ally. Kweli msondo itapata pigo ila melody ya kihuni katika gitaaa bado ipo katika vidole vya solo attack Tanzania. Msikilize kwenye Kalunde na ndugu hatuelewani.
Kweli kabisa, Ridhiwani Mpangamawe ndio anaebeba ladha halisi ya Msondo.
 
Back
Top Bottom