TANZIA Mwanamuziki mkongwe, Said Mabera afariki dunia

Penye penzi hapakosi tenzi, wakale walisema na huwezi kula muwa bila kukuta fundo. Huu wimbo unaniacha hoi saana. Wewe utakua mpenzi wa msondo mwenzangu. Najua utakua unakunywa safari na Ni mshabiki wa timu kongwe. Dar es Salaam Young Africans.
Hahaaa
 
Sio kweli mkuu jamaa umri ulienda sana pia feg na konyagi alipiga sana nilimuona last timu pale dar safari pak buza

Sitaki na usinilazimishe nikaanza kuzitoa 'Siri' za Watu, ila pengine ulibakia Wewe tu pekee kutokujua kuwa Wanamuziki hao wengi walishajiwakia.
 
Mabe mabe mabe mabe mabela. Hapo ni kwenye korasi ya wimbo wa msondo ni baada ya gitaa la said mabela kucharazwa kweli kweli
 
Gwiji wa muziki wa dansi na Kiongozi wa bendi ya Msondo Ngoma, Saidi Mabera amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Jumanne Septemba 29, baada ya kuugua kwa zaidi ya miezi miwili. Mazishi yatafanyika leo saa 10 jioni nyumbani kwake Goba.

Msiba upo Nyumbani kwake Tegeta A maeneo ya Goba jijini Dar es Salaam.

===
SAID MABERA WA MSONDO NGOMA AFARIKI DUNIA

GWIJI wa ukung'utaji gitaa la solo hapa nchini na kiongozi wa bendi ya Msondo Ngoma, Said Mabera amefariki dunia jana saa 6 za usiku.

Mabera ambaye ameitumikia Msondo Ngoma tangu mwaka 1973 bila kuhama hata mara moja, amefariki baada ya kuugua kwa zaidi ya miezi miwili.

Mtoto wa marehemu, Mabera Said amesema kuwa msiba uko nyumbani kwao Goba jijini Dar es Salaam na mazishi yatafanyika leo saa 10 alasiri huko huko Goba.
Da....nimesikitika sana kuondoka kwa gwiji la muziki ujanani mwangu.
RIP Mabela.
 
Back
Top Bottom