Frank Wanjiru
JF-Expert Member
- Apr 12, 2012
- 21,873
- 38,810
Wimbo unaitwa Ajali utunzi wa TX Moshi WilliamMabe mabe mabe mabe mabela. Hapo ni kwenye korasi ya wimbo wa msondo ni baada ya gitaa la said mabela kucharazwa kweli kweli
Wimbo unaitwa Ajali utunzi wa TX Moshi WilliamMabe mabe mabe mabe mabela. Hapo ni kwenye korasi ya wimbo wa msondo ni baada ya gitaa la said mabela kucharazwa kweli kweli
Gwiji wa muziki wa dansi na Kiongozi wa bendi ya Msondo Ngoma, Saidi Mabera amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Jumanne Septemba 29, baada ya kuugua kwa zaidi ya miezi miwili. Mazishi yatafanyika leo saa 10 jioni nyumbani kwake Goba.
Msiba upo Nyumbani kwake Tegeta A maeneo ya Goba jijini Dar es Salaam.
===
SAID MABERA WA MSONDO NGOMA AFARIKI DUNIA
GWIJI wa ukung'utaji gitaa la solo hapa nchini na kiongozi wa bendi ya Msondo Ngoma, Said Mabera amefariki dunia jana saa 6 za usiku.
Mabera ambaye ameitumikia Msondo Ngoma tangu mwaka 1973 bila kuhama hata mara moja, amefariki baada ya kuugua kwa zaidi ya miezi miwili.
Mtoto wa marehemu, Mabera Said amesema kuwa msiba uko nyumbani kwao Goba jijini Dar es Salaam na mazishi yatafanyika leo saa 10 alasiri huko huko Goba.
R.I.PGwiji wa muziki wa dansi na Kiongozi wa bendi ya Msondo Ngoma, Saidi Mabera amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Jumanne Septemba 29, baada ya kuugua kwa zaidi ya miezi miwili. Mazishi yatafanyika leo saa 10 jioni nyumbani kwake Goba.
Msiba upo Nyumbani kwake Tegeta A maeneo ya Goba jijini Dar es Salaam.
===
SAID MABERA WA MSONDO NGOMA AFARIKI DUNIA
GWIJI wa ukung'utaji gitaa la solo hapa nchini na kiongozi wa bendi ya Msondo Ngoma, Said Mabera amefariki dunia jana saa 6 za usiku.
Mabera ambaye ameitumikia Msondo Ngoma tangu mwaka 1973 bila kuhama hata mara moja, amefariki baada ya kuugua kwa zaidi ya miezi miwili.
Mtoto wa marehemu, Mabera Said amesema kuwa msiba uko nyumbani kwao Goba jijini Dar es Salaam na mazishi yatafanyika leo saa 10 alasiri huko huko Goba.
Inatia uchungu sana.Nitakwenda na naani msondo ngooma, nitacheza na nani magoma kitakita.
Kalale mahali pema .
Athumani Momba,
Selemani Mbwembwe,
Maina,
TX Moshi William,
Muhidin Maalim Ngurumo na leo
Said Mabera.
Nitakwenda na naani msondo ngooma, nitacheza na nani magoma kitakita.
Kalale mahali pema .
Athumani Momba,
Selemani Mbwembwe,
Maina,
TX Moshi William,
Muhidin Maalim Ngurumo na leo
Said Mabera.
Ishaq Kibene alikua mfadhili au mwanamuziki?Malizia na Isiaka Kibene.
Mtunzi na mpiga gitaa la solo mahili sana Mabera!!!! Mungu amlaze pema. Amefariki akiwa na umri gani? Tangu Enzi za Nuta Jazz nyimbo kama Nidhamu ya Kazi, Mpenzi Zarina, Nisingekukimbia Mpenzi na vibao vingine vingi Enzi hizo tutamkumbuka sana Said Mabera na wengine waliotangulia mbele za haki.
Pole sana kwa familia na taasisi na bendi ya Msondo Ngoma.
MfadhiliIshaq Kibene alikua mfadhili au mwanamuziki?