TANZIA Mwanamuziki mkongwe, Said Mabera afariki dunia

Rubawa

JF-Expert Member
Dec 25, 2015
2,055
3,239
Gwiji wa muziki wa dansi na Kiongozi wa bendi ya Msondo Ngoma, Saidi Mabera amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Jumanne Septemba 29, baada ya kuugua kwa zaidi ya miezi miwili. Mazishi yatafanyika leo saa 10 jioni nyumbani kwake Goba.

Msiba upo Nyumbani kwake Tegeta A maeneo ya Goba jijini Dar es Salaam.

mabela++pic.jpg

===
SAID MABERA WA MSONDO NGOMA AFARIKI DUNIA

GWIJI wa ukung'utaji gitaa la solo hapa nchini na kiongozi wa bendi ya Msondo Ngoma, Said Mabera amefariki dunia jana saa 6 za usiku.

Mabera ambaye ameitumikia Msondo Ngoma tangu mwaka 1973 bila kuhama hata mara moja, amefariki baada ya kuugua kwa zaidi ya miezi miwili.

Mtoto wa marehemu, Mabera Said amesema kuwa msiba uko nyumbani kwao Goba jijini Dar es Salaam na mazishi yatafanyika leo saa 10 alasiri huko huko Goba.
 
Nitakwenda na naani msondo ngooma, nitacheza na nani magoma kitakita.
Kalale mahali pema .
Athumani Momba,
Selemani Mbwembwe,
Maina,
TX Moshi William,
Muhidin Maalim Ngurumo na leo
Said Mabera.
Wote hao waliotajwa wameshalala na hawataamka tena hadi kiyama. Ardhi imekula watu.

Hakika sisi sote ni wa Mungu na Kwake Yeye ndio marejeo yetu. Mwenyezi Mungu Amrehemu Mzee Said Mabela
 
Back
Top Bottom