Mwanamume Malaya - Je ungekuwa wewe ungefanyaje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanamume Malaya - Je ungekuwa wewe ungefanyaje?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Theodora, Dec 25, 2009.

 1. Theodora

  Theodora JF-Expert Member

  #1
  Dec 25, 2009
  Joined: Dec 20, 2009
  Messages: 522
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Nimekuwa kwenye relationship ya up and down na nimeteswa kinoma. Tumezaa mtoto na huyu mwanamume lakini alivyosikia mi mja mzito akaanza kuwatongoza wanawake wengine na nikasikia anafunga ndoa. Dunia ajabu, familia ya yule dada walipata ukweli na wakamkataa. Baadaye akaanza kurudi kwangu lakini hata hamjali mtoto, hana kazi na nilikuwa namsaidia kwa kile kidogo ninachopata na ukumbuke kulea nahangaika mwenywe na ndugu zangu.

  Sasa cha ajabu ni umalaya wake ambao hauna mpaka - yaani hana aibu. Sasa hivi bila aibu kaanza kutoka na dada nafanya naye kazi na kashampa uja uzito! Nimechanganyikiwa lakini wadau what would u do if you were me? Udhaifu wangu na kila siku najuta ni wema wangu - na hata mama aliniambia una roho nzuri lakini walimwengu wabaya kuwa makini.

  My baby girl is wonderful and so special... na huwa nauliza why do good people suffer so?
   
 2. Rah_sputin

  Rah_sputin Member

  #2
  Dec 25, 2009
  Joined: Nov 3, 2009
  Messages: 83
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pole sana.
  Wadada wengi hujikuta kwenye hali kama yako.Wanaume bahati mbaya sana hawana ile ya kuangalia walikotoka na waelekeako.So ladies, be careful before kukubali kula tunda na mbegu zake.
   
 3. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #3
  Dec 25, 2009
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,035
  Trophy Points: 280
  Cha muhimu chunga asikuletee ngoma maana anaonekana hajatulia huyu
   
 4. kitalolo

  kitalolo JF-Expert Member

  #4
  Dec 25, 2009
  Joined: Dec 4, 2006
  Messages: 1,846
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  una bahati hujafunga naye ndoa achana naye anza maisha mengine na ujitahidi usahau baada ya muda mambo yatakuwa mazuri lakini ukiendelea kungangania hapo utajuta maisha yako yote yaliyobaki, na usishangae mambo yako yakiwa mazuri akakutafyuta ili akuharibie tena usirudi nyuma mama songa mbele, najua ninachukushauri hii ni kutokana na uzoefu kidogo nili nao nahii uwaathiri watu wengi kama unataka kuondoka na hiyo hali jitahidi uwe wewe usiogope kwamba marafiki na ndugu wanasema nini ishi kama utakavyo na uwe huru . natamani ungelijua neno ninalokuambia, wanawake wengi wanateseka kwaajili ya kuishi maishi ya kulazimisha kuishi na mtu mwache tafuta maisha yako mlee mtoto wako
   
 5. Annina

  Annina JF-Expert Member

  #5
  Dec 25, 2009
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 437
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mwambie Mungu asante kwa kuwa una afya njema na kazi inayokuwezesha kulea mtoto wako. Usikate tamaa, mungu anakupenda na yupo pamoja nawe,ujifunze kutokana na mahusiano haya na usonge mbele - unaweza kuishi bila yeye, amini hivyo!
   
 6. U

  Ujengelele JF-Expert Member

  #6
  Dec 26, 2009
  Joined: Jan 14, 2008
  Messages: 1,256
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuchanganyikiwa katika hali kama hii ni lazima, lakini tu usiendelee kupoteza muda wako na huyu mpumbavu ambaye ameshakuonyesha kwamba hakujali na wala hana msaada wowote katika malezi ya mtoto wenu. Usimpe nafasi nyingine yoyote ile ya kuendelea kukutesa kwa namna moja au nyingine.
   
 7. Papizo

  Papizo JF-Expert Member

  #7
  Dec 26, 2009
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 4,611
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180
  Kama vipi angalia maisha yako yanakwendaje...Siwezi kumpa mwanamke damu yangu alafu hata kama kwa bahati mbaya then kajifungua nisijali...Nadhani huyo mwanaume ni mchafuzi tu na hajui alifanyalo......Check life yako na achana na huyo ambaye hajui wapi anaelekea zaidi kichwani mwake anajua mapenzi tu basi.......
   
 8. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #8
  Dec 26, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  its very funny.....
  kwamba mwanaume hana kazi na bado amewpiga mimba
  wanawake wawili......

  this guy is my hero....
  kwa jinsi ilivyo ngumu kupata mwanamke
  wa kukujali ukiwa huna kazi.
  he is stupid yes,but he is impressive also.
   
 9. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #9
  Dec 26, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180

  Nimeielewa post yako vyema, lakini nina neno fupi sana juu ya mkasa hu....nI KWAMBA HUYU JAMAAA ATAKUJA KUKUTAFUTA.
  Na bahati mbaya ni kwamba naogopa atakuwa amechelewa..

  sHIKA NENO HILI, na utaja kunieleza....Nimemaliza.
   
 10. Theodora

  Theodora JF-Expert Member

  #10
  Dec 26, 2009
  Joined: Dec 20, 2009
  Messages: 522
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Thanks all, kwa advice nzuri na Mungu awabariki. One day at a time, nadhani waliopitia life kama yangu wataelewa nikisema unapotamani all the pain to go away lakini in life its step by step. Ahsanteni
   
 11. M

  Mtu B JF-Expert Member

  #11
  Dec 27, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 921
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Nakupa pole sana. Lakini kwa uzoefu wangu, wanawake wa namna yako hukutana tena na mwanaume mwingine, labda na mwingine pia, nao huwatenda hayohayo, wanazalishwa na kutelekezwa. Na jamaa akiwa na shida anakurudia unamtunza kama mtoto, na shida yake ikiisha anaishia. Na kuendelea.

  Ujumbe: Chunga sana. Usitoe kitu yako hovyo. Umeshaumwa na nyoka, liwe funzo. Tulia na mwanao, hata akija mwanaume mwingine weka stricter terms kuliko, kwamba chovyachovya marufuku, hapo utaheshimika. Lakini ukizubaa ukijifanya una huruma kwa wanaume, au ati 'roho nzuri' ndio kuwapa kitu yako wakuombapo, utajuta kuwafahamu.
   
 12. L

  Lampart Senior Member

  #12
  Dec 27, 2009
  Joined: Sep 18, 2009
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Nd. Mtu B,
  I say, hii ni advice au matusi???
   
 13. S

  Shingo Senior Member

  #13
  Dec 27, 2009
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 127
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mwanamke au mwanaume hatakiwi kumhurumia mwenzie when it comes to establishing relationship; hilo ni kosa namba moja. Mahusiano yanatakiwa yaanze kutokana na mutual respect si kuhurumiana.

  Huyu mwanaume tayari unamwita malaya - sifa mbaya kabisa na ni neno zito kulitumia. Ikiwa hiyo ndo description yake, je imeanza leo au alikuwa hivyo wakati mnaanza mahusiano. Kama imeanza leo, haiwezekani ukawa sababu? Kama alikuwa nayo toka mwanzo, kwa nini hatimaye ulimkabali hadi kuzaa naye?

  Pengine inawezekana matatizo yapo. Lakini wakati tunapotaka kutatua matatizo inabidi tujiangalie wenyewe kwa undani zaidi ili kusaidia kuepuka matatizo kabla hayajaja au kuweza kuona alama za awali mapema na kuzitafsiri mapema na kutoa maamuzi kabla ya maumivu.

  Ukisema huyu ni malaya, unajiweka wapi wewe kuwa umeolewa na malaya?
   
 14. L

  Lampart Senior Member

  #14
  Dec 28, 2009
  Joined: Sep 18, 2009
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu Shingo,
  Inamaana unamuona huyu mwana-JF wetu ni malaya kwasababu kakubali kuolewa na malaya?
  I am sure husemi hivyo!!!
  Labda sijakufahamu, kwani kiswahili chenu cha watu wa pwani kwasisi kutoka Bara ni kigumu sana!!!
   
 15. Abunwasi

  Abunwasi JF-Expert Member

  #15
  Dec 28, 2009
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 3,166
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Ndani ya moyo wako unajua kuwa huyo jamaa hakupendi,hakuthamini ila anakutumia kwa faida yake. Mapenzi ni nipe nikupe sasa kama wewe umeamuwa kuwa mtumwa wa mapenzi ya upande mmoja endelea lakini bora nusu hasara kulika hasara kamili
   
 16. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #16
  Dec 28, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  huyo kijana ni MSHAMBA WA WANAWAKE!bado ana hulka za ujana za kupenda ngono kupindukia!ukiangalia kwa jicho la ziada kuhusu wanawake utagundua kitu kimoja interesting ni kwamba WANAWAKE NI WALE WALE!..TULIA NA ULIE NAE!
   
 17. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #17
  Dec 28, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Kama hujapima afya yako, nakushauri uende ukapime uone kama hujaathirika. Na majibu kama yatakuwa safi achana na huyo jamaa atakuharibia mambo yako na mtoto wako pia. Pili, nina imani litakuwa ni fundisho tosha kwako kujifanya mnawapenda majamaa mengine ambayo ni irresponsible kazi yao ni kuchovya anakuburudisha unampa na tujisenti then anakula kona, hayo mambo ni ya kizamani sana. Angalia sasa amekuzalisha hatunzi mtoto na huyo mwingine ameshamchapa mimba mtakuwa wengi sana na watoto wenu watawalaumu nyie mama zao kwa kuzaa na baba asiyewajibika!!! Good day.
   
 18. Theodora

  Theodora JF-Expert Member

  #18
  Jan 7, 2010
  Joined: Dec 20, 2009
  Messages: 522
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  All, nashukuru for advice which made sense. Mtu B na Shingo ur perception of somebody you dont know the character is spiteful and because mi ni mwanamke. I pray that what happened to me does not happen to people u love and care about then u will tel me kama wao ni malaya.
   
 19. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #19
  Jan 8, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  dada huyo mbona ni malaya mzoefu ..labda unampenda kama moyo wako au ?kama maneno yote hayo yana ukweli piga moyo konde uendelee na maisha yako na mwanao ,mzazi mwenzio anafanya ngono zembe Y ,inavyoonekana hana mapenzi na wewe ,anakufata wewe kwa vile anajua una mstiri ..
  chukua hatua mapema kabla hujajuta baadae
   
 20. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #20
  Jan 8, 2010
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  mie magonjwa ya waziwazi ndio cyawezi, huyo mkaka hakuheshimu bwana, sasa ndio nini hivi kutembea mpaka na unaofanya nao kazi? kidogo muwege na roho ngumu...ninavyojijua huyu ungekuta nimeshamsahau kabisa.
   
Loading...