Mwanamume kumuachisha kazi mukewe!!!!

Mwanamume kumuachisha kazi mukewe!!!!

Hahahaha hureee .mshauri amrudishe au kumtafutia kaz nzur bas .maana inaelekea utasikilizwa..
 
Mrembo, hapo pa red! Siyo kweli kuwa ni "from no where", huyo ni mume kwa hiyo unajua anakotokea labda na sababu za kukuachisha kazi. Kama unafanya kazi na hela zako hazisaidii "mwili mmoja" basi ukae unipikie ugali maana ndio kuoa!

Hata ziwe za from somewhere kazi siachi ng'oooooo, labda kwa ridhaa yangu mwenyewe
 
sasa unakuta mishahara yenyewe ndo laki 4 sijui tano, si bora ukae nyumbani uwape watoto malezi bora ya mzazi kuliko kuwa busy for nothing unamwacha kwa yaya!..kama unapata kila kitu, tengeneza mradi binafsi utakuwa more flexible..au kama shule ipo vizuri kichwani tafuta kazi itakayokupa uhuru kiasi
 
Maisha ya kuachishana kazi yalikuwa enzi hizo
na huyo mwanaume anaekuachisha kazi hana akili mukichwa
maisha yenyewe mafupi akifa leo au kesho unastrive vipi.............

Hivi ni kwa nn nyie wanawake huwa mnattua hv? Hakuna mwanmke ambaye anaishi bila kufikiria kwanza mmewe ashakufa. Kwa nn hufikirii kama ukifa wewe? unakuta kila mnachofanya mwanamke kazi yake ni kuchukua tahadhari tu kwa kuwaza mwanaume akifa!
Analazimisha mfunge ndoa ili ukifa asisumbuliwe
Analazimisha mjenge haraka hata ukifa awe tayari kwake
Anashauri mfungue biashara ili ukifa asipate shida

yaani kila kitu mnajiaandaa tu tukifa????
 
kweli hata me ningepata mume tajiri regardkess nina phd ningependa nikae home nilee watoto lakini niwe na kabiashara kadogo kakuweka mind busy
 
mie mke wangu lazima aache kazi akae home aalee mtoto full time sio miezi mitatu. hapo anakaa nje mwaka lea mtoto ndio unarudi kazini. unataka mtoto kazi unaacha kwa mwaka mzima ule watoto then later ndio unaweza rudi job. hiyo ya kumuachisha moja kwa moja sio kabisa
 
Wengi huachisha wake zao kazi ili wawanyanyase....
lakini vp kwa wale wanaoachisha kazi ili wawape deal ya kusimamia biashara zao ambazo kipato chake ni mara 10 ya mshahara wa awali
 
una pesa?siwezi kukutafuta sababu we sio husband material

pesa nasaka sasa wee umejuaje mie sio husband material jamani...mie mbona wewe mwenyewe utafurahi nakwambia...ndoa yetu itajaa furaha....ila ukitaka kuolewa na mie ujue kabisa naraka unizalie watoto wawili wakike
 
helo kumbe yule muke mwenzangu angekuwa mboss mkubwa tu TPA mume alivomuoa.
Akamuachisha kazi.
Wanaume kwa nini mnawaachisha wake zenu kazi?
Na wewe mudada kwa nini mume akuachishe kazi?
Wadada msikubali muwachishwe kazi.
Mie tokea nifahamu kuwa aliachiswa kazi namuhurumia na ninampenda mke mwenzangu.
Ile tabia ya kumfungia mume wake nimeacha.

Unajua Mwanamke ameumbwa kumsaidia Mwanaume, Yaani mwanaume atakula kwa jasho na mwanamke atazaa kwa uchungu,sio maneno yangu ni ya bible,hata nchi za jiarabu mwanamke hafanyi kazi,ni mwanamume.....
Baada ya vita vya pili vya dunia 1945,kulianza kutokea uhaba wa wafanyakazi ulaya,hivyo,kuanza kwa wanawake kufanya kazi.....Thats why Hata hapa TZ, wanawake wameanza kufanya kazi baaada ya 1945.BUT Hali ya kiuchumi imebadilika,wanawake wanafanya kazi ili ku balance mambo.JE? Wataweza pia kubalance staha,kuvumilia,kumheshimu mumewe hata kama anamzidi kipato?
Najiuliza kwanini vitabu havikusema mwanamke atatafuta kwa jasho?au bible inatakiwa pia kubadilishwa?au bible inamkandamiza mwanamke?Nini majukumu ya mwanamke?nafikiri tukijua majukumu ya kila mmoja ktk familia ndo msingi wa Upendo na kuvumiliana.Maisha yamebadilika ya kiuchumi,je je kiroho/imani inabidi tubadilike pia,Kipi kinaweza kumuongoza mwenzie?
"NAPENDA MAISHA MAZURI ILA SIPENDI KUDHARAULIWA HATA KAMA SINA KITU"
 
aisee unacho nichekesha kila leo ni kuigiza ujui kiswahili.kumbe hadi leo huna mume wako.lakini kumuachisha mke kazi si suluhu ya kitu chochote ni unyanyasaji tuu.
 
Hata ziwe za from somewhere kazi siachi ng'oooooo, labda kwa ridhaa yangu mwenyewe

mrembo, kwangu mimi nilivyo mkoloni, ndoa itaisha. Kila mmoja na lwake! Nami sipendi mke aache kazi, lakini kama haina kujenga Nyumba yetu, utaacha au ndoa itakufa! Najua una wajibu mkubwa kwa wazazi wako, wamekusomesha etc, tukubaliane tuendeje. Lakini ukileta jeuri ya wanawake wenye fedha, basi ndoa! CCM siyo mama yangu!- alisema Nyerere-
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom