Mwanamume kumuachisha kazi mukewe!!!!

Mwanamume kumuachisha kazi mukewe!!!!

Zahra White,.............. ndivyo mke mwenzio alivyokwambia? Kuwa aliachishwa kazi na mumewe? Pengine alivolunteer yeye mwenyewe!
 
Last edited by a moderator:
mrembo, kwangu mimi nilivyo mkoloni, ndoa itaisha. Kila mmoja na lwake! Nami sipendi mke aache kazi, lakini kama haina kujenga Nyumba yetu, utaacha au ndoa itakufa! Najua una wajibu mkubwa kwa wazazi wako, wamekusomesha etc, tukubaliane tuendeje. Lakini ukileta jeuri ya wanawake wenye fedha, basi ndoa! CCM siyo mama yangu!- alisema Nyerere-

Na ndio maana kuna kipindi cha urafiki kabla ya ndoa, ya nini kuolewa na mwanaume jeuri kama Idd Amini??
 
itategemea kuachishwa kazi nini mbadala wake...sio waachishwa unashinda home unapauka hadi ueleweki
 
Binafsi nliachakazi mwenyewe, vile ilikuwa mbali na makazi ya mumewangu. Tukakubaliana akantaftia mtaji wa biashara yangu. Sio tu kukaa home unakua mmbea bali unapata muda wa kutosha kuhudumia mume na watoto. Nafurahi mume arudipo ale nlompikia, akute nmemuandalia mazingira safi, room inanukia udi.
 
Na ndio maana kuna kipindi cha urafiki kabla ya ndoa, ya nini kuolewa na mwanaume jeuri kama Idd Amini??

Kwetu hakuna urafiki kamwe kati ya msichana na mvulana. Wazazi ndio wanafanya kila kitu. Huu uhuni na umalaya wa leo ndio unaleta haya matatizo unayoyasema kuwa hutaacha kazi. Mnakutana ofisini, barabarani, shuleni mnabebana na nyege basi mwisho ni huo. Pole kama nimetumia lugha kali!
 
Hahahahaha naona una hasira kufananishwa na Idd Amin Dada...pole mkuu, ndio JF hii bwana.
 
Hahahahaha naona una hasira kufananishwa na Idd Amin Dada...pole mkuu, ndio JF hii bwana.

Wala sio hilo la Amin, Amin actually watu wa kagera walikuwa wanampenda maana wao wana afiliation sana na "abaganda" wanajiona wanashabihiana sana na waganda-abaganda kuliko Tanzania. Anyway tunaheshimu mipaka ya wakoloni na tuitunze. Mrembo wala sina hasira, kwani wanaohamasisha polisi kupiga raia mbona hatuwachukii. Nasema kubebana kwa vizazi vya leo kwa sababu ya nyege kunanikera sana!
 
Ndo hatima mliyochagua na ndio mmeamua kuitembeza dunia kwa style ya genye.....sasa tufanyeje sie?
 
Mrembo, hapo pa red! Siyo kweli kuwa ni "from no where", huyo ni mume kwa hiyo unajua anakotokea labda na sababu za kukuachisha kazi. Kama unafanya kazi na hela zako hazisaidii "mwili mmoja" basi ukae unipikie ugali maana ndio kuoa!

watu wengine viatu kweli mi hata kwa dawa sikai nyumbani mzazi wangu anashindia bamia kutwa kunisomesha ili niwe na maisha mazuri then uniambie nisifanye kazi patachimbika,hata kama nalipwa 20tsh ni si haba.kwanza kukaa nyumbani ni majungu tu,umbea na unampa mkeo nafasi ya kutafutwa na wengine maana mawazo yake yatakuwa finyu hana atakacho waza zaidi ya 6*6 na ukitetereka kidogo tu wenzako wanakusaidia.
 
helo kumbe yule muke mwenzangu angekuwa mboss mkubwa tu TPA mume alivomuoa.
Akamuachisha kazi.
Wanaume kwa nini mnawaachisha wake zenu kazi?
Na wewe mudada kwa nini mume akuachishe kazi?
Wadada msikubali muwachishwe kazi.
Mie tokea nifahamu kuwa aliachiswa kazi namuhurumia na ninampenda mke mwenzangu.
Ile tabia ya kumfungia mume wake nimeacha.

Zahra; Naomba kuuliza issue hapa ni ipi. Ni mama kuwa mahali kama MWAJIRIWA au kuachishwa ni kwamba mume ANAMFUNGIA VYANZO vyote vya mapato? Kwa sababu sidhani kama ni sahihi kuchukulia kazi kwa maana ya wale walio kwenye ajira peke yao. Kwangu mimi mama mwenye biashara hata ya kuchoma vitumbua na kuiuzia hoteli jirani kwa ujumla ana kazi pia. Sasa hapa MUME kamuachisha mkewe kwa maana kazi IPI? Ni case hiyo ya TPA pekee unazungumzia?

OK; Kwanza nadhani ni haki Mume kujua mke wake anapataje kipato. Pia ni wajibu wake kuhakikisha kuwa mke anakuwa na chanzo cha kipato ambacho hakimzuii kufanya majukumu yake msingi kama mama na mke. Pia kama mume lazima awe makini kuwa shughuli za kipato za mama hazidhuru maisha yao kama wana ndoa, ila zinawaletea nafuu, upendo na tija na hata uwezo wa wao kuwajali na kuwasaidia ndugu zao wa pande zote. Ieleweke wazi kuwa jukumu la mume kwa mke na kaya yote liko paleplae bila kujali kipato cha mama

Ni desturi nzuri mume kujua mkewe ana vipaji gani na akamsaidia mama huyu kutumia kipaji chake ipasavyo. Akijenga msingi huu siku zote wataheshimiana (wengi anyway)Kwa hali yoyote mama mwenye kipato halingani na asiye nacho. Na a busy mind ni bora kuliko an idle one.

Sasa tukirudia mada yako ya kumwachisha kazi (hapa natafsiri kama ulilenga ajira maofisini/viwandani)vizuri ikaenda na NIA NJEMA. Na mlengwa akaijua hiyo NIA. Bila huo msingi patakosekana masikizano na mshikamano katika kupata njia mbadala ya kuyaweka sawa maisha ya familia husika.

Hilo la wewe kumuachia mumeo huru ili asikuachishe kazi kama huyo wa TPA huenda halitalipa. Alishakuzoea na kijiwivu chako. Sasa ukikiacha mbele ya safari mshikaji anaweza kukugeuzia kibao kuwa ka-notice tabia yako "ime-change" sana na "hakuelewi elewi". KISHA utasikia "Mama Latifa.......Hebu.......TULIZANA HAPA NYUMBANI KWANZA" Hakika mtoaji rizki ni M/Mungu pekee.

WEWE ISHI KAMA WEWE
 
Hivi ni kwa nn nyie wanawake huwa mnattua hv? Hakuna mwanmke ambaye anaishi bila kufikiria kwanza mmewe ashakufa. Kwa nn hufikirii kama ukifa wewe? unakuta kila mnachofanya mwanamke kazi yake ni kuchukua tahadhari tu kwa kuwaza mwanaume akifa!
Analazimisha mfunge ndoa ili ukifa asisumbuliwe
Analazimisha mjenge haraka hata ukifa awe tayari kwake
Anashauri mfungue biashara ili ukifa asipate shida

yaani kila kitu mnajiaandaa tu tukifa????

Ushasikia mtoto karithi mali toka kwa mama?au kesi mahakamani baba mjane kadhulumiwa mali?ni sababu mkifa ndo kizazaa kinaanza.hasa cha mali so lazima mwanamke achukue tahadhari.mbona mambo mengine mnapenda kufanyiwa hamlalamiki?kupikiwa,kufuliwa etc si mnasema ni kazi ya mwanamke.kufa ndo hamtaki?heh!
 
mie mke wangu lazima aache kazi akae home aalee mtoto full time sio miezi mitatu. hapo anakaa nje mwaka lea mtoto ndio unarudi kazini. unataka mtoto kazi unaacha kwa mwaka mzima ule watoto then later ndio unaweza rudi job. hiyo ya kumuachisha moja kwa moja sio kabisa

Heeeh!kama sijamtambulisha houseboy wetu kama babake mzazi.coz ndo tunashinda nae home,wewe ukiwa kazini...I don't get this ya mwanaume kudhani his part ni kumpa mwanamke ujauzito tu,malezi ni juu ya mkewe.uafrika kazi jamani!!!hivi hamjifunzi kwa wenzenu walivyo responsible?ndomana unakuta mtoto anasema my dad is my role model..huku hukuti hizo mambo!unaweza niachisha kazi na bado nkawa mguu na njia kwa mashosty.utanifunga kamba??hebu kuweni rational.mwanamke anajua majukumu yake,si lazima umfanye punda wako!
 
watu wengine viatu kweli mi hata kwa dawa sikai nyumbani mzazi wangu anashindia bamia kutwa kunisomesha ili niwe na maisha mazuri then uniambie nisifanye kazi patachimbika,hata kama nalipwa 20tsh ni si haba.kwanza kukaa nyumbani ni majungu tu,umbea na unampa mkeo nafasi ya kutafutwa na wengine maana mawazo yake yatakuwa finyu hana atakacho waza zaidi ya 6*6 na ukitetereka kidogo tu wenzako wanakusaidia.

Sawa dada, wala hakuna anayekukataza. Kama hutaki si basi rudi kwenu nami nirudi kwetu! Ndio uhuru kama walionao wazungu! Kwa wazungu Mke na mume wote ni sawa kuishi kwao ni mkataba, AFRIKA BADO! Inabidi tukubaliane hiyo kazi yako unaifanyaje!
 
Akikubali kunipa pesa sawa na mshahara wangu kila mwisho wa mwezi na marupurupu huenda nikamfikiria.
Ila kama hataki ajue kbs kuwa akina Kimbweka watamsaidia kunilea na kunitunza hapa mjini.

Halafu kumbuka leo ijumaa na mimi nakuhusu mpaka jumapili ndiyo nakuachia........................!
 
Na mke kumwachisha kazi mmewe je?
 
heee
atakubali atakupa mwezi wa kwanza na wapili..kajitahidi sana wa tatu..baada ya hapo mama sahau..
kuna mtu ishamtokea hiyo
Akikubali kunipa pesa sawa na mshahara wangu kila mwisho wa mwezi na marupurupu huenda nikamfikiria.
Ila kama hataki ajue kbs kuwa akina Kimbweka watamsaidia kunilea na kunitunza hapa mjini.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom