mwanamume ajifungua huko Biharamulo

mwanamume ajifungua huko Biharamulo

Kamakabuzi

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2007
Posts
2,904
Reaction score
1,364
Mwanaume mmoja ambaye jina halikuweza kupatikana mara moja, amejifungua mtoto wa kiume kwa operesheni huko Biharamulo.
Maelezo ya awali yanadai kwamba mwanaume huyo ambaye ana mke, alimpachika mimba binti ambaye haikujulikana kama ni mwanafunzi au la. Baada ya hapo alikataa katakata kuwa hahusiki na mimba hiyo, ndipo wazazi wa binti walipoamua kumkomesha wakaenda walikojua wao na mimba ikahamia kwa huyo mwanaume. Ameibeba miezi yote iliyokuwa imebaki na kujifungua. Mke wake ndiye ananyonyesha huyo mtoto.
Kama kuna wana JF walio biharamulo watujuze zaidi.
Je hii si inaweza kuwa suluhu ya wanaowatia mimba watoto wa shule?
 
pigeni picha au wekeni video watu waone,si zipo camera za simu na kila kitu? ripoti ya hospitali au madaktari waliofanya huo upasuaji si wapo?
mambo ya kila kitu kuwa tetesi inaboa wakati vifaa vya ku-prove vipo.
 
Hiki kisa hata Ze Comedy kipindi kile bado wapo EATV waliwahi kukitoa kuwa kilitokea huko Rukwa (Mpanda I guess) so naona mwana umebadilisha place na kuiweka B'mlo hapo...............
 
mtoa hoja alete ushahidi na siyo kutoa porojo tu
 
Wabongo kwa kupenda story za kichawi chawi, mbona hamuwarogi mafisadi basi :sick:
 
pigeni picha au wekeni video watu waone,si zipo camera za simu na kila kitu? ripoti ya hospitali au madaktari waliofanya huo upasuaji si wapo?
mambo ya kila kitu kuwa tetesi inaboa wakati vifaa vya ku-prove vipo.
Nimewaomba walio Biharamulo watujuze zaidi ikiwa ni pamoja na kutupatia picha. Au Biharamulo hakuna mwana JF?
Hii habari nimeipata kwa rafiki yangu aliye Biharamulo na ninamuamini. Nimemweleza atafute vielelezo anitumie ili niviweke hapa kwani yeye hajui kutumia computer lakini kwa simu anaweza kunitumia picha.
 
Hivi mpaji mimba na mpokeaji kwa nini wasiwe na adhabu sawa? Nionavyo mimi hii ni porojo!
 
Hiki kisa hata Ze Comedy kipindi kile bado wapo EATV waliwahi kukitoa kuwa kilitokea huko Rukwa (Mpanda I guess) so naona mwana umebadilisha place na kuiweka B'mlo hapo...............

Hii nilivyosikia ilikuwa true story naniliwahi kuonyeshwa kijiji hicho lakini jule jamaa inasemekana tumbo lilijaa na akawa na dalili zote za ujauzito lakini ilipofika wakati wa kujifungua alipata uchungu kawa walipotaka kutolewa mtoto walikuta tumbo limejaa maji na jamaa akafa hapo hapo. Hii ya huyu jamaa ni porojo tena ni uzushi katika kipindi hiki cha utandawazi tungefahamu tu hata hiyo mimba achilia mbali mtu kujifungua. Asitujaze ujinga anatakiwa awe na ushahidi wa kutosha (ambao haupo) kuleta habari kama hii.
 
Back
Top Bottom