Daby
JF-Expert Member
- Oct 26, 2014
- 34,961
- 80,197
hahaha pole mkuu.Mtu mzima kuamua kumtukana mwenzie hivyo hadharani lazima kunajambo, inawezekana yapo mengi zaidi ya hilo....
By the way, wakati mwingine wanawake mnakera tena sana, mi mwenyewe iliisha nitokea ya hivyo, nimejibana mtoto wa kiume angalau wife asipate dhahama ya kukaa masaa 14 kwenye basi, nikamega nusu ya mshahara nikamkatia tiketi ya ndege siku yenyewe inafika anajizungusha ndanii, namkumbusha muda una enda yeye hata hashtuki ndio anaanza nakufua, akachelewa shuttle....roho ikaniuma kweli, mtoto wa kiume nikajikaza na mihasira yangu nikawasha gari nimpele airport( hapo ni Arusha mpaka KIA) alipoona nimewasha gari na yeye akaamua kubadili tena nguo, nikazima gari, nimepiga simu mtu hatoki, kuingia ndani ndio kwanza anapanga begi limejaa balaa, nikamsaidia kulifunga, tumeondoka mpaka KIA watu wana board, ananiambia kasahau wallet na ina ticket tena akaanza kunilaumu mimi ndio nimemuwahisha mpaka kasahau, nikaidowload ticket nikampa...kule matangazo ndio yanazidi yeye ndio kwanza yuko kwenye kioo cha anarekebisha nywele...uvumilivu ulikwisha tho iam not proud of lakini nilimpa mabanzi mawili naona akili yake ikarudi, na ninashukuru hajawahi kuniuliza kwa nini nilimpa mabanzi na tangu siku hiyo kama anataka ndege atumie mshahara wake.......kwa hiyo haya mambo wakati mwingine wanawake mnatuuzi mno. Ingawa sitetei lakini inawezekana jamaa uvumilivu umefika mwisho, wenzenu roho zetu ndogo mjue!
ndicho nilieleza huko nyuma.
wanawake wanajijua wenyewe.
Atakuambia mwenyewe nimepata email ya wateja madagascar wanahitaji mzigo. Anahitajika mtu aende.
mnashauriana aende yeye anakubali kabisa na mnabook ticket. Zinabaki siku tano anakuambia sijisikii kwenda. sababu ni nini sijiskii kwenda wewe nenda.
anakuja anabadilika tena anaamua kuondoka. siku ya kuondoka anaanza mizengwe. hajaandaa chochote. Nusu saa imebaki ndiyo anaanza kujipanga.
Lazima ukasirike kama hauna break matusi hayakukauki.

