Daisy Llilies
JF-Expert Member
- Apr 19, 2019
- 1,017
- 2,163
Mtoto wa kike wewe, pichu unafua kwenye washing machine, huna haya? Zile safari zako za mwezi pia utarun washing machine kila siku? Pichu ifue kwa mikono, uanike sehemu itakayo pata jua na hewa. Pichu nzuri ni za cotton. Kuna wale wenye pichu rangi kwa kusafiria lakini za kila siku ni nyeupe. Hata pichu za cream pia huwa zinapendeza.
Kwa wale mnaoishi kwenye vyumba vya kupanga, si vibaya kuweka khanga juu baada ya kuanika pichu kwenye kamba. Mtoto wa kike kuloweka pichu mmh, hiyo mikono ina kazi gani? kuna wale wasio na haya anamuachia dada amfulie mpaka pichu.