Mwanamke ninayeishi nae hataki nikamwone mwanangu

Mwanamke ninayeishi nae hataki nikamwone mwanangu

Ni bora kuanza upya kuliko kuendelea na mahusiano mabovu, ukiendekeza kuvumilia eti kisa Mali utakufa kabla ya siku na hizo Mali zitaliwa na waume wenza so kama mapenzi yameisha kimbia... Vitu vinatafutwa na happiness matters the most
 
umejuaje mkuu kipindi flan mawazo yalonizidi nikawa ni mtu wa tungi sana siku moja niliuzika sana nikawa napiga konyagi na dragon energy ilifika usiku mapigo ya moyo yalizidi kuwahi hospital pressure ilikuwa juu 180/90 ila nashukuru nilipata nafuu siku hizi nimeacha kabisa pombe
haya mambo yanaumiza sana moyo
ila badili avatar kabla hujaenda mbeya kumwona mtoto
 
mfano: mlivyokaa miaka 4 iwe hujazaa akapewa mimba na jamaa mwingine mtoto alivyofikisha mwaka lijamaa likamchukua je ungemsamehe aendelee kuwa mkeo kama yeye alivyofanya??

akuage sasa anasafir kwenda kumuona mtoto mkoani nyumbani kwa kidume ambacho hakijaoa! ungemruhusu kwa furaha?? jiweke kwenye hyo nafasi na ujue utavyojisikia nayeye hivyohivyo. wanaume ni wabinafsi aisei
 
Kwanini umshirikishe mwanamke kila kitu unachofanya? Kwa wakiristo - kama ibrahim angemshirikisha sara kuhusu kumtoa sadaka Isaka hivi unafikiri pangetosha?

Unatakiwa uishi na mwanamkr kwa akili bhana. Si kila kitu unamwambia mkeo, wanawake wanaroho mbaya sana, ukiendelea hivyo na tabia ya kuanika kila kitu utakuja juta. Jumapili njema!!
 
Nenda kaone damu yako kaka, usiwe mnyonge. Hana uwezo wa kukulaan huyo kwani hana Baraka.
 
Mwanaume lazima uwe na msimamo, kuyumbishwa yumbishwa ndo kunakofanya udharaulike

Ikiwezekana mbebe mwenda naye, akaone mwanao
 
Mwanaume hukutakiwa kuuliza swali hili...kwani ulipoonda Mbeya na kutia mimba ulimuaga?
 
Wiki ya pasaka nina likizo na nilikua nimepanga nisafiri mbeya kwenda kumwona mtoto niliezaa na mwanamke mwingine.

Kwani kipindi naishi na huyu nilie nae tulikaa Muda bila kupata mtoto nilitoka nje ya mkoa nikiwa mbeya nilifanikiwa kumpa huyu binti ujauzito tukianya mengi bc tuu tuyaache mtoto kazaliwa nikalea nilipo mueleza huyu binti nina mtoto ilikua ugomvi si wa kitoto alidiriki kumwita mbwa aliapa hataki kumwona wala kumsikia iliniuma sana. sijawahi enda mpaka leo

Sasa jana nimemgusia kwenye likizo ya easter naenda mbeya imetokea ugomvi adi kunilaani nikienda sitofika imeniuma kwa nn hataki nikamwone mwanangu nimewaza ikiwezekana nimfukuze tuu maana miaka mi4 hana mtoto mm naumia nikiwaza mfukuza nina miradi, viwanja, duka, si itakuwa kugawana? nifanyeje next weak niende mbeya kumwona mtoto huku kashanitishia?

Ushauri naomba kama Huna ushauri ukae kimia usilete matusi nipo seriaz... plzzzz
Kama ana wivu azae ka toto ya yeye tena ikibidi huyo mwanamke wa mbeya, muhamishie hapo nyumbani kabisa
 
kweli mfumo dume ni hatari kwa maisha ya wanawake wa kiafrika. Unajiita mume huku hujui, huthamini wala kujali hisia za mkeo? Ye aliandika barua kwa Mungu kuomba akose mtoto? Ungejua jua ye kakusaliti kwa ajili ya udhaifu ulio nao usingeumia? mkeo ana maumivu sana moyoni kwa kukosa mtoto, alitegemea uwe faraja yake na mhangaike pamoja kutafuta suluhu na tiba. Badala yake umeenda kumfanyia unyama na kujeruhi moyo wake. halafu humpendi ila unaishi naye tu kwa kuhofia kugawana mali!!!! Natamani ningemfahamu mke wako. Nenda tu Mbeya Baba na njiani upate ajali UFE ili mkeo aishi kwa amani na tatizo lake la kukosa mtoto.
 
Unataka akuchekee ukienda pasha kiporo huko baba haumaniki jua hivyo ulishaharibu,wanaume wa cku hizi ni shidaaah hilo nalo mpk uombe ushauri,kujiongeza nimeshindwa..eti Mali unawazia umefikia hadi huko?you are not trustworthy basi tu umesema tusitukane
 
Tafuta mbinu za kutaifisha mali zako ki u janja zitafutie madalali uza halafu cheza dili
Umpe kidogo tu ukifanikiwa mtimue huyo dem atakuja kukuua wewee
 
Niseme machache: kwanza mkuu umekosea sana tena mnoo kwa jambo ulilofanya ni laziiima aumie, hilo unapaswa kulitambua.Hvyo jarbu kwenda nae kwa busara na hekima nyingi.
Pili, kumuona mtt ni jambo la muhimu tena sanaaa, sasa nashauri nenda kamuone mtoto, ila sasa usiende kipindi cha pasaka kama ulivyosema mwanzo maana yy lazma ataumia.
Acha pasaka ipite kaa nae nyumbani mfurahie siku kuu, alafu baada ya mda kidogo tafuta (safari danganya hata unaenda tunduma huko) kamuone mwanao hata wik nzima.

Hiyo utalinda na kuheshimu hisia zake na wewe utakuwa umetendea haki moyo wako.

NB: Sio kila jambo umwambie mkeo mengine mdanganye danganye tuu huwa kauongo kidogo wana enjoy pia✌️
 
Yaani wanaume mmekosa ubavu siku hizi.
dahhh mmnaitia huruma. Huyo mwanamke si mke wako.
ni mchumba tu wa mika minne.

Wewe umeshindwa kabisa kuona kipi muhimu kati ya
huyo mwanamke na mwanao. huyo mtoto anamuhitaji babayake.
Acha kumpa huyo mdada asie na upendo kipaumbele. Nenda kamuone mwanao.

Eti anakwambia hutafika salama na we kweli unaogopa kwani ye MUNGU??
Ndio maana hakupi heshma maana umekosa mabavu mbele yake.
Nijuacho kuhusu sisi wanawake ukituachia kimoja kimoja imekula kwako.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom