Hatimaye nimemchukuwa mwanangu namlea japokuwa sijaoa

NYOTIENO JARIEKO

Senior Member
Apr 29, 2017
196
324
Nilimaliza form four 2012 kutokana na kuwa free nikajaribisha na mimi kuwa na dem ki utoto utoto. Eeeeee mara paap mimba, kama utani vile, lakini ndio ukweli.

Kipindi hicho binti ana miaka 18 mimi 19, kwa kweli bado tulikuwa watoto. Kibaya zaidi binti hana baba na ana wadogo zake kama 4 hivi mnavyojua maisha ya vijijini, na mama yake alikuwa anapika pombe (Gongo) kutunza familia.

Huyu binti alimaliza form 4 bahati mbaya alifeli kutokana na hali halisi ya kwao coz muda mwingi alikuwa anamsaidia mama yake kupika gongo ili wapate mahitaji ya kila siku. Nyumbani kwetu ilikuwa pia hovyo kipeasant peasant lakini tulikuwa angalau kulikoni wao coz mzee alikuwa analimalima na kupata vijiela vidogo vidogo vya kutupeleka St. Kayumba.

Ilichukua muda mfupi nikaenda A-level nikamwacha na mimba wa miezi 2, niliumia sana nikimwona binti anavyoteseka huku sina hata uwezo wa kumhudumia. HONGERENI WANAWAKE WANAOLEA MIMBA /WATOTO PEKE YAO MUNGU AWATANGULIE. Nilijaribu kuongea na mama yangu akipata chochote ampatie sana sana kipindi akikaribia kujifungua, japokuwa mama yake alinichukia kwa kilichotokea lakin maji tayari yalishamwagika hayazoeleki. Mama yake alisema mengi lkn haikusaidia mwisho wa siku akajifungua.

Alijifungua vizuri akaleta copy yangu (kabinti) baada ya mwaka moja akaolewa kijiji jirani, akaenda na mwanangu huko. Nilipoenda Advance sikuwahi kurudi home hadi nilipomaliza kutokana na umbali wa shule, na kutokuwa na nauli kwa hiyo likizo nilikuwa najichangaya kwenye vibarua kutafuta karo, hela ya kujikimu na kidogo kumtumia mzazi mwezangu anunue sabuni.

Niliporudi nilienda moja kwa moja kumwona mwanangu, bila hata kuogopa ni mke wa mtu. Hahaha nilikuwa na hamu ya kumwona damu yangu (Asee damu yako ni yako tu). Kabinti kangu aliponiona tu mbio kunipokea wakati huo tangu azaliwe hajawai kuniona. Nilifrahi siku huyo lakini nilimwonea huruma mzazi mwezangu, alichoka kulingana na hali ya maisha, tayair alikuwa na mtoto wa pili kipindi hicho na alikuwa mke wa tatu.

Tuliongea sana akanisimulia changamoto alizopitia hadi akaamua kuolewa mke wa tatu, wakati huo maisha bado yalikuwa hovyo koz ni mke wa tatu alafu ni mdogo ki umri kulingana na wanawake wengine wa huyo mumewe. Mumewe mkorofi anampiga sana (ana alama sana mwilini ya mapigo) kwa wenyeji wa mkoa wa Mara hapa mtanielewa. Kwa hayo mateso niliumia sana lkn sikuwa na jinsi.

Baada ya hapo niliendelea ku-struggle na maisha lakini nilikuwa namtumia hela kidogo kidogo nikipata kwa matunzo, akapewa masharti na mumewe hakuna kupokea matumizi ya mtoto na akanyang'anywa simu na kutishiwa kupingwa hadi avunjike vipande vipande akiendelea kupokea matumizi ya mtoto.

Niliwaza sana hilo swala nikaamua kumtumia mama yangu nguo na hela ya matumizi anampelekea kwa siri asije akapigwa kwa sababu yangu.

Kibaya zaidi mzazi mwezangu alikuwa anaumwa mara kwa mara, na maisha yake nayajua vizuri, nilimtumia taarifa kwamba naenda kuchukua mwanangu nikae naye. Nikaona ni muda sahihi wa kukaa na mwanangu coz nimeshapata kazi ili nimsomeshe.

Asee nilipofika kwa mzazi mwezangu haikuwa rahisi, mumewe hakutaka nimchukue mwanangu, yeye alishaanza kupigia mahesabu ya kumwoza akikua tu (kupata mahari) niliumia lkn mwisho wa siku nikakabidhiwa kabinti kangu, mamake alitaka anipe mtoto but huyo mmewe hakutaka kabisa. Hatua iliyobaki akiendelea kukataa ni kufuata sheria/kwa nguvu coz niliomba likizo kuchukua mwanangu kwa njia yoyote, namshukuru Mungu alikubali ki ustarabu mwishoni.

Nilipoenda kuchukua binti yangu ,nilimkuta mzazi mwezangu amekonda sana,hana raha, anaumwa huku akitumia dawa ya kienyeji bila hata kujua tatizo, tayari alikuwa na watoto watatu, baada ya kunikabidhi mtoto nilimshukuru kwa kulea mwanangu kwa sida. Nilimwambia huyu ni mtoto wetu naenda kumsomesha na kumwandalia future yake lakini ataendelea kuwa mtoto wetu na hata akifunga shule nitamleta akusalimie.

Kwa kweli kumtenga mama na mwanae ni kazi! Sijui aliwaza nini tena akajua labda nimeshaoa mke wangu atatesa mtoto. Alikuja kukubali baada ya kumwakikishia sijaoa naenda na mdogo wangu wa kike watakaa nae nikienda job, na huo ndio ukweli nilimchukuwa mwanangu na mdogo wangu wa kike coz sijaoa na mwanangu anateseka na mimi sipendi kumwongezea mama yangu mzigo wa kulea wajukuu, ni muda wake wa kupumzika, amehangaika kutulea sana kwa hiyo sikupenda nimwache kwa bi mkubwa.

Kabla sijaondoka na mtoto kwa mzazi mwezangu, kutokana na afya yake ilivyo niliongea naye kwa muda mfupi nikajua ana matatizo mengi pamoja na ya kiafya, nikamwambia amdanganye mumewe anavyoweza aje kwao nimpeleke hospitali akapime ajue ana matatizo gani kuliko kutumia dawa ya kienyeji bila kujua tatizo / ugonjwa. Alibahatika kuja kwao na watoto wake wawili wa huyo baba akaniambia amepewa likizo na mumewe aje asalimie mama yake, kwa kuwa bado nilikuwa kijijini kesho yake tukaenda hospitali acheki afya.

Akapatwa na uvimbe kwenye uzazi, kwa ushauri wa madokta akasahuriwa afanyiwe upasuaji yaondolewe yakiachwa yataleta matatizo pamoja na cancer badae. Aliponiuliza kama naweza kusimamia matibabu yake nikamjibu ndio lengo langu ili upone, lkn itakubidi uombe ruhusa kwa mumeo, tukakubaliana na doctor tukapangiwa terehe ya upasuaji, malipo ya kwanza nikatoa siku hiyo hiyo.

Mama yake alimwelezea mumewe kuwa mke wake ana uvimbe kwenye mfuko wa uzazi itabidi afanyiwe upasuaji. Mumewe alimjibu mama yake "KAMA ANA PESA YA KUHARIBU HUKO HOSPITALI ATOE LKN YEYE HANA PESA YA KUHARIBU" Duh! Mungu atusamehe sisi wanaume Namshukuru Mungu upasuaji ulifanyika vizuri alitoka Theatre vizuri walitoa uvimbe kwa maelezo ya Daktari.

Namshukuru Mungu nililipia malipo yote Hospital japokuwa malipo private hospital bila bima ni gharama mno lakini sikuwa na jinsi, mzazi mwezangu alikuwa anateseka, sikupenda mwanangu awé na mawazo ya ugonjwa inayosumbua mama yake.

Suala ikaja tayari kafanyiwa upasuaji, hana pesa, hana bima, je akiugua atafanyaje kabla hajapona? complication ya upasuaji atatibuje? Nililipia bima ilibaki kupeleka passport na kwa kuwa watu wanahitajika sita niliamua kutoa mdogo wangu moja nimweke kama mke wangu ili asiteseke hata kwa mwaka au miaka mwili ili asipate shida ki afya endapo nikioa nitamtoa.

Nimepanga akipona vizuri nitajibana nimpe kamtaji aanzishe hata biashara ndogo ndogo coz amefanyiwa upasuaji ameshauriwa asifanye kazi ngumu, na kazi yake kulimia watu kwa mkono, ndipo mkono iende mdomoni.

Nimeamua kufanya haya sio kwamba nina hisia naye kimapenzi, hapana hata kidogo, ni mke wa mtu, naheshimu mke wa mtu.

Nimefanya hivyo kwa kujibana sana kipato changu ni kidogo sana lakini kanizalia kabinti tena copy yangu, nimemwonea huruma maisha yake aliyoyapitia na mateso anazopitia na bado anaendelea kupitia magumu.

KAMA ULIMPA MIMBA /ULIZAA NA BINTI KIPINDI CHA UJANA LAKINI MUNGU KAKUONYESHA NJIA HATA KIDOGO, BORA UFUATILIE MWANAO UJUE MAENDELEO YAKE, FIKIRIA ANGEKUWA MTOTO WAKO KAFANYIWA HIVYO UNGEJISIKIAJE?
 
Mkuu sijigambi, ilinitokea kutokana na utoto na hata binti mwenyewe bado alikuwa hajakomaa cha kumweza kujitambua sana kuwa yupo siku za hatari.Hata wewe yawezekana ujana wako ilikutokea kibahati mbaya .mimi sikuwa na uwezo wa kumsaidia kipindi hicho kulingana na ukweli wa maisha lkn sikufarahia yeye kupata kupata mimba lkn hali halisi ndio hivyo.
Wewe ndio umemuharibia maisha yake na bado unajigamba unamuonea huruma.
 
Mbona mimi siamini kama hii stori ni ya kweli
Mkuu huo ndio ukweli ,mzazi mwezangu tumezaliwa kijiji kimoja ,na kwao sio mbali sana na kwetu, tunajuana vizuri kifamilia.Watu walijua nimezaa nae mtoto na nikirudi home lazima nifuatilie maendeleo ya mwanangu, mtoto alishatuunganisha ...yani siku moja nilimfuata mwanangu nimsalimie hakuwa na raha kwa sababu mama yake alikuwa anaumwa amelala nyumbani .kila nikimsemesha anaongea lkn hana raha,Ukiwa mwelewa unaweza kutambua hali halisi.Kingine mwanangu ndio mkubwa naamini nikimsomesha anaweza kumsaidia mama yake, pamoja na wadogo zake kuliko kumwacha na mama yake ateseke wakati nina uwezo wa kumsomesha kibongobongo na kutimiza ndoto yake.Furaha yangu ni kumsimamia mwanangu na yeye aje asaidie mama yake naamini nimefanya cha maana kuliko kutuma matumizi tu wakati maendeleo yake kimasomo na kimalezi sio rafiki kabisa.
 
Mkuu huo ndio ukweli ,mzazi mwezangu tumezaliwa kijiji kimoja ,na kwao sio mbali sana na kwetu, tunajuana vizuri kifamilia.Watu walijua nimezaa nae mtoto na nikirudi home lazima nifuatilie maendeleo ya mwanangu, mtoto alishatuunganisha ...yani siku moja nilimfuata mwanangu nimsalimie hakuwa na raha kwa sababu mama yake alikuwa anaumwa amelala nyumbani .kila nikimsemesha anaongea lkn hana raha,Ukiwa mwelewa unaweza kutambua hali halisi.Kingine mwanangu ndio mkubwa naamini nikimsomesha anaweza kumsaidia mama yake, pamoja na wadogo zake kuliko kumwacha na mama yake ateseke wakati nina uwezo wa kumsomesha kibongobongo na kutimiza ndoto yake.Furaha yangu ni kumsimamia mwanangu na yeye aje asaidie mama yake naamini nimefanya cha maana kuliko kutuma matumizi tu wakati maendeleo yake kimasomo na kimalezi sio rafiki kabisa.
Ubarikiwe sana kijana, natamani hawa wanaojiita wanaume wajifunze kwako
 
Umetudanganya kwenye BIMA.
NHIF pekee ndio yakubali watu6 ika haikubali ndugu. Inakubali watoto wa kuzaliwa na mke wa ndoa na wazazi tu
Kuanzia mwaka gani? Tuna takiwa kuuliza kwanza... Hawa ndugu hawatakiwi kuanzia mwaka gani... Wapo ambao mpka Leo wanaweka ndugu japo wenyewe hawataki...

Kuna wengine hawana uwezo wa kuzaa, hawataki kuzaa... Wamebadili huu utaratibu juzi juzi... Kwa mawazo yao ghafi
 
Back
Top Bottom