Mwanamke ni chombo cha starehe(?)



Hapa hatuzungumzii neno; Chombo wala hatuzungumzii neno; mwanamke na wala hatuzungumzii neno; starehe, Tunazungumzia maneno yanayojenga hii sentensi kwamba; " Mwanamke ni chombo cha starehe".

Ni hiyo sentensi nzima kwa ujumla ndiyo inayomfanya leo mwanamke awe dhalili duniani, na mimi nashangaa eti wewe Safuher inakuaje unaunga mkono kauli zinazowatia utumwani wanawake (mama zetu), hivi ni wewe huyo Safuher ninayekujua ndani ya jf au mwingine???, umekumbwa na kitu gani kuunga mkono kauli za "kitwaghuti"??!!
 
Kwani kuna sehemu mimi nimesema kuwa mtume kasema mwanamke ni chombo cha starehe ?



Sent using Jamii Forums mobile app



Hujanielewa, nasema hivi; wewe ulileta maneno ya mtukufu mtume (saw) yasemayo kwamba; " Mwanamke mwema ni starehe kwa mumewe"--- nikakuambia hayo ni maneno ya hekima ya mtume (saw) yanayoingia akilini kwamba starehe ya mume inapatikana kutokana na wema wa mkewe, sasa niambie haya maneno; " mwanamke ni chombo cha starehe", umeyapata wapi??, kama ulivyopata hiyo kauli ya mtume (saw), je kauli ya "mwanamke- chombo -starehe" (mwachosta) imo katika hadithi za mtume (saw) ili tuiamini kauli hiyo??.
 


Wewe vipi???, unashika hili na mara unashika jingine!!!.

Angalia wewe mwenyewe umenukuu Hadithi ya mtume (saw) kwamba "mke mwema ni starehe kwa mumewe", yaani starehe ya mume kutoka kwa mkewe ni WEMA wa huyo mke, sasa wewe una hakika gani hao uliowataja ni lazima wawe wema kwa waume zao ili hiyo starehe ya wema wao waume zao wapate???, yaani hapo unazungumzia juu ya Wake na waume zao na kulingana na nukuu yako ya hadithi, starehe anayoipata mume ni Wema kutoka kwa mke wake, umeelewa kidogo??!!🤣🤣

Suala lililopo mezani ni; "mwanamke ni chombo cha starehe" na wala sio "mke ni chombo cha starehe kwa wema wake", na ndiyo maana katika post yako ya msingi na vyangudoa uliwaorodhesha katika kundi la "mwanamke ni chombo cha starehe" (mwachosta).

Ile post ulipaswa kuweka heading hii; ""mke mwema ni starehe kwa mumewe"", hapo sasa ndiyo ungewaweka Mama zetu, dada, shangazi, mabinti, mama wadogo zetu wakiwa pamoja na waume zao nk, hii ingekuwa imekaa vyema.
 


Mkuu Safuher narudia tena, shida sio neno, starehe, wala sio neno mwanamke pia sio neno Chombo, shida ni hii sentensi ya ujumla kwamba; "mwanamke ni chombo cha starehe", hii ni sentensi inayotumiwa vibaya kuwadhalilisha wanawake, wanawake wamefanywa kama vyombo, nyenzo, visaidizi vya kukidhi haja za starehe za Wanaume, kama nilivyosema sentensi hiyo ukiigeuza katika kiingereza inakuwa ni; "A woman is a comforting stuff" (japo hupendi kiingereza), sasa angalia ni jinsi gani wanawake wanavyo wa- comfort wanaume:-

(1) Macasino---- humo wamejaa wanawake wanaojiuza kwa ngono na kutembea utupu.

(2) Ring girls--- hao ni wasichana wanaopita nusu uchi ndani ya boxing ring kuonyesha rounds.

(3)Face off girls--- hawa ni wasichana walio nusu uchi wanaoonyesha matangazo ya biashara ya makampuni katika boxing match press conference.

(4) Business barners---- Utaona picha za wanawake wakiwa nusu uchi katika matangazo ya biashara.

(5) Bendi za Music--- utaona wenenguaji wa kike wako nusu uchi huku wakinengua mbele ya akina SAFUHER.

(6) Midundiko, kangamoko,, vigodoro--- kote huko ni wanawake kumwaga radhi kwa kwenda mbele;------- kisa ni kauli kwamba; "Mwanamke ni chombo cha STAREHE".

Mwanamke naye maskini kawa "brain washed" naye kawa mtunwa wa mwanamume kufanywa vyovyote kuwa chombo cha starehe.

Wakati ndio huu kuacha mfumo dume kuwagandamiza wanawake viumbe dhaifu, ni wakati wa kuwakomboa kama jinsi mtukufu mtume (saw) aliposema "mke mwema ni starehe kwa mumewe"-- na sio ""mwanamke ni chombo cha starehe"", hiyo ni kauli ya kimagharibi wala sio kauli ya kiislamu.
 
Unapinga nini sasa wakati mimi nimeonesha kuwa neno chombo ni sifa ya kusifia.

Na neno starehe linafahamika.

Kwa hiyo chombo cha starehe unapata maana sahihi hapo iliyokusudiwa na mimi.

Wewe unasema ni umagharibi kwa muono wako,kwa muono wangu mimi sioni kama ni umagharibi kwa sababu hali inaonesha hivyo.

Mimi nilishakuambia ya kuwa chombo ni sifa nzuri na wewe unekubali.

Kwa nini neno chombo likiwa pamoja na neno starehe libadilike maana iwe mbaya ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa kunukuu ndo iwe nimesema kuwa mtume kasema mwanamke ni chombo cha starehe ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu sasa kama wao wametumia vibaya unataka uniingize mimi katika wao wakati mambo niliyoyasema yako wazi kabisa.

Yani marejeo yako wamagharibi kwa kuwa wao walisema hivyo basi unataka walivyomaanisha wao iwe sawa na mimi.

Mwanamke ana jukumu kubwa la kumpa starehe mwanume na hii ni kutokana na kuwa mwanamke kaumbwa kipekee na yeye ndio ukomo wa starehe zote.

Sasa wewe unafuata walichosema wamagharibi nwadhalilishaji ndo unafanya marejeo kuoinga hoja yangu badala yake uangalie kioi nimemaanisha M

Sent using Jamii Forums mobile app
 


"MWANAMKE NI CHOMBO CHA STAREHE"----- hapo ndipo penye shida.

Kweli و بالله huoni shida katika hayo maneno??, licha ya ufafanuzi na mifano yote niliyokupa???, ngoja nimuite muhusika labda anaweza na yeye kutoa mchango wake.

Kwa taadhima nakualika Auntie FaizaFoxy uangalie hayo maneno je ni maneno yenye heshima kwa nyie mama zetu??.

Mbaya zaidi ni maneno yanatoka katika kinywa cha "Muisilamu" kudhalilisha wanawake.
 
Mkuu hapa tatizo ni kuwa umeshaathirika na fikra za wamagharibi ambao wanatumia sentensi hiyo kwa mtazamo hasi.

Sasa ukikutana na mtu anaetumia senteensi hiyo kwa mtazamo ungine unataka ufosi kuwa kama ule wa wengine.

Kama tunakubaliana kuwa neno chombo ni la kumsifia mwanamke basi kwa msingi gank neno hili lenye sifa nzuri likiungana na neno starehe ati inakuwa umedhalilisha ?

Neno gani katika hiyo sentensi linaashiria kudhalilisha wakati hapo maneno ni matatu (mwanamke,chombo,starehe)?


Sent using Jamii Forums mobile app
 


Nadhani Auntie FaizaFoxy atakuja tumsike mchango wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…