Mwanamke ni chombo cha starehe(?)

Mkuu unaandika vitu vingi kazi kusoma.

Lengo langu nimeandika.

Nakuuliza tena kwa mujibu wa nani ati ukisema chombo ni kudhalilisha ?

Kama ni common sense nikakuuliza kama mimi common sense yangu haisemi hivyo unasemaje ?



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nimeongea kiswahili,hayo ya comfort woman unasema wewe mkuu.

Zungumza nilichomaanisha mimi sio unaweka maana zako mkuu.

Alafu kila msemo ni methali kwma ni hivyo kwa mujibu wa nani kwamba kila msemo ni methali ?

Huu wangu ni msemo tu sio methali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 


Mwanamke ni Chombo cha nini???-- chombo cha starehe!!!---- starehe gani???.

Mwanamke ndiye anamlea mume, ndiye anayelea watoto, ndiye mwalimu wa kwanza wa watoto na hivi anakuwa ndiye building block ya taifa, halafu wewe unamuita ni Chombo cha starehe kama gari na pikipiki nk!!!.

Huo kweli ndio mfumo dume.

Tafakari kabla ya kuandika jambo.
 


Misemo yote inajulikana na tayari imeandikwa na watu tumeisoma mashuleni halikadhalika methali nazo zinajulikana na tumezisoma mashuleni, sasa kama wewe umeanzisha msemo wako mpya basi ungalisema mwanzo kwamba umeleta msemo mpya usemao; "MWANAMKE NI CHOMBO CHA STAREHE", na kabla ya kuuleta humu ungemuonyesha Mkeo, Dada yako na hata mama yako usikie kwanza maoni yao.
 
Niliposema kuwa ni chombo cha starehe ukaelewa kuwa hana kazi zingine ?

Kusema chombo cha starehe haimaanishi hana kazi zingine.

Alafu nakuuliza neno chombo cha starehe kama ni udhaliloshaji ni kwa mujibu wa nani ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hayo ni maoni yako.

Sikuomba maoni popote.

Huwezi kunipangia.

Wewe kama una utaratibu wako kabla ya kupost kama huwa unawaoneaha hao ulowataja hapo basi huo ni wako siwezi kuufuata.

Alafu nikishawaambia uliowataja hapo juu ndo utakubali kuwa manamke ni chombo cha starehe au umeandika tu kama malalamiko mkuu Mokaze.

Neno mwanamke ni chombo cha starehe kuwa ni udhalilishaji kwa mujibu wa nani ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtume aliwahi kusema kuwa

"Starehe ya dunia ni mke mwema "

Kwa maana mtume anaamini kuwa ili ustarehe basi uwe na mke mwema hapo ndo utastarehe uzuri.

Unadhani Mtume kakosea kusema kuwa starehe ya dunia ni mke mwema ?



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Alafu nakuuliza neno chombo cha starehe kama ni udhaliloshaji ni kwa mujibu wa nani ?


Wewe unataka iwe kwa mujibu wa nani ili uamini kwamba uachosema sio sawa??
 
Hayo ni maoni yako.

Sikuomba maoni popote.

Huwezi kunipangia.


Siwezi kukupangia lakini cha ajabu unataka kujua ni kwa mujibu wa nani kwamba maneno yako;" MWANAMKE NI CHOMBO CHA STAREHE" sio maneno mazuri napata wapi ??!,

Sasa wewe unataka nitoe ushahidi wapi ili ujue kwamba maneno hayo siyo mazuri??, kama umeshindwa kupata ushauri kwa wahusika (wanawake) waliokaribu nawe je nikikuambia unaposema; Mwanamke ni chombo cha starehe ni sawa na kusema "a woman is a tool for comfort" utakataa??!!.

Nakwambiaje, Changudoa anayejitambua, anayejiuza mitaani ukimwambia kwamba yeye ni kwa ajili ya starehe lazima atasononeka tu sembuse mwanamke wa kawaida!!!.
 


"Starehe ya dunia ni mke mwema," unaona kauli za hekima hizo??, siyo hiyo kauli yako ya ajabu kwamba "Mwanamke ni chombo cha starehe"

Katika kauli hiyo ya mtume (saw) inaonyesha starehe ya mke kwa mumewe ni wema wa huyo mke na sio vinginevyo.

Mkuu, Sasa andika post nyingine itakayobeba kichwa; "starehe ya dunia ni mke mwema"
 
Sasa kama unakubali kuwa starehe ya mwanaume duniani ni mke mwema na huyo mke ndio mwanamke.

Tunarudi pale pale kuwa neno chombo ni sifa ambayo nimeitumia kumpendezesha mwanamke,mfano mtu akisema "umekiona chombo kile kinapita" hapa akikusudia mwanamke na unajua kuwa kauli kama hizi zipo.je hapo neno chombo ametumia kukashifu au kusifia ?

Mtu akisema anataka jiko neno jiko kasifia au kakashifu ?

Mtu akisema "nimepata chuma ccha ukweli" akikusudia manamke je hapo neno chuma lengo asifie au akashifu na kudhalilisha ?



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa kama huna marejeo huoni kama unalazimisha nifuate mtazamo wako ?

Unajua kuwa miongoni mwa mambo yakuwaleta watu kwenye fikra moja ni kuwa na marejeo ya aina moja ?

Sasa kama wewe unafosi mimi nione kuwa neno chombo ni udhalilishaji alafu huna marejeo huoni kuwa unalingania kwa upofu ?


Sent using Jamii Forums mobile app
 


Mkuu unataka kupindisha mada; mada ni; "MWANAMKE NI CHOMBO CHA STAREHE", je kauli hiyo inayo heshima kwa wanawake??-- wala hatuzungumzii kuhusu mwanamke kama mke.

Hadithi ya mtume (saw) uliyoileta inazungumzia specifically juu ya starehe za wema wa "mke" kwa mumewe wala haizungumzii juu ya starehe za wanawake kwa ujumla.

Yaani mke akiwa mwema kwa mumewe mume anapata starehe lakini mke akiwa mwovu mume ataishi maisha ya "jehanamu".

Mifano uliyoitoa haihusiani kabisa na kauli yako kwamba "Mwanamke ni chombo cha starehe", ni starehe ipi hiyo aliyonayo mwanamke??, huwezi kupinga maana ya hayo maneno ni; "A woman is a comfort tool" sio maneno mazuri na kamwe huwezi kuyatamka mbele ya kadamnasi labda huwe hujitambui.
 


"Mwanamke Sio chombo tu bali chombo cha starehe"----ugomvi upo hapo, ni starehe ipi unayoizungumzia hapo??
 
ndivyo ilivyo ndio maana wakajiuza na kudanga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…