Mwanamke na Salary Slip yangu

Mwanamke na Salary Slip yangu

flood

Senior Member
Joined
Jul 10, 2017
Posts
131
Reaction score
202
Kwanza kabisa niwasalimu vijana wenzangu tunaowaza kujikwamua katika umaskini. Kumekuwa na dhana ambayo mimi kwangu naiona ni kama chachu ya maendeleo kwa vijana wa kisasa, dhana hii ni juu ya kushare na mpenzi au mke kile unachokipata hata kama sio kwa 100% namaanisha mshahara au kipato.

Hapa ni pale wanasema za kuambiwa changanya na zako ujijibu, katika kukua kwangu nilikuwa nikisikia wazee wakisema mwanamke haoneshwi wala hatakiwi kujua kipato cha mpenzi au mume wake lakini niliiga kwa familia moja ya ndugu yangu wao walikuwa wanashare kile wanachokipata na japo kilikuwa kidogo ila walifanikiwa sana.

Sasa na mimi baada ya kufikia hatua ya kuishi na mwenzangu nikaamua niwe na share nae kipato kwa kumuonesha salary slip na kabla ya kupata mshahara tulikuwa tunakaa chini na kuweka malengo na matumizi na kumbuka mda huo yeye alikuwa hana kazi na elimu yake niya 4m four wakati mimi nina bachelor.

Baada ya mda alipata kazi na alikuwa akipata hela nyingi na hapo ndipo niliona sikukosea kumuonyesha mfano maana baada ya mda mfupi tuliweza kununua kila kitu na hata nyumba tuliyokaa tukahamia kwenye kubwa na tukafanikiwa kujenga na nyumba standard ndani ya mwaka na nusu tuu hapo nikiwa na 27yrz na yeye ana 23yrz only.

Nawashauri vijana wa kiume msiache kushare na wapenzi wenu vipato vyenu na umpe nafasi ya yeye kutoa maoni na ushauri juu ya matumizi ya hicho mnachokipata hata kama hakupata fursa ya kuendelea na masomo na hii itakusaidia kumjua mind set yake.

Sijaweka nukta unaweza kudondoka experience yako katika hili
 
Ukiwa na bahati hiyo usidhani kila mmoja anayo. Wanawake wengine atataka kila lake lifanyike kwakuwa ana uhakika mzigo umeingia. Vipo vya kufanya (kushare) lakini si hilo hapana
 
Ni nzuri,inafaa sana,kwa baadhi ya wanandoa ambao wana malengo.
Hata mimi ninaitumia,inatupatia wepesi wa kutimiza malengo ya familia.
Pia hii husaidia mwenzako kubana matumizi,kwaajili ya kukamilisha lengo lenu.

Angalizo,lazima ujiridhishe na tabia za mwenza wako kabla ya kumshirikisha.
Kwan yaweza tokea kaugonvi,mwenzako akakomba mzigo,na kusepa.
Au nae anachota anahamisha account nyingine,
 
Inategemea na mwanamke. Ukiona hajielewi usilogwe kumwonyesha kipato. Otherwise mpe hadi kadi ya bank akae nayo kama akili ipo
 
Hongera mkuu.

La muhimu ni kupata mwenza Mwema
 
  • Thanks
Reactions: wax
Three things to hide your enemy

1.Your income
2.Your next move
3. ..........

Usubiri paka utakapokuwa na uhakika kwamba ni friend not enemy.
 
Kwanza kabisa niwasalimu vijana wenzangu tunaowaza kujikwamua katika umaskini.
Kumekuwa na dhana ambayo mm kwangu naiona ni kama chachu ya maendeleo kwa vijana wa kisasa, dhana hii ni juu ya kushare na mpenzi au mke kile unachokipata hata kama sio kwa 100% namaanisha mshahara au kipato.
Hapa ni pale wanasema za kuambiwa changanya na zako ujijibu, katika kukua kwangu nilikuwa nikisikia wazee kwakisema Mwanamke haoneshwi wala hatakiwi kujua kipato cha mpenzi au mume wake lakini niliiga kwa familia moja ya ndugu yangu wao walikuwa wanashare kile wanachokipata na japo kilikuwa kidogo ila walifanikiwa sana.
Sasa na mm baada ya kufikia hatua ya kuishi na mwenzangu nikaamua niwe na share nae kipato kwa kumuonesha salary slip na kabla ya kupata mshahara tulikuwa tunakaa chini na kuweka malengo na matumizi na kumbuka mda huo yeye alikuwa hana kazi na elimu yake niya 4m four wakati mm nina bachelor, baada ya mda alipata kazi na alikuwa akipata hela nyingi na hapo ndipo niliona sikukosea kumuonyesha mfano maana baada ya mda mfupi tuliweza kununua kila kitu na hata nyumba tuliyokaa tukahamia kwenye kubwa na tukafanikiwa kujenga na nyumba standard ndani ya mwaka na nusu tuu hapo nikiwa na 27yrz na yeye ana 23yrz only.
Nawashauri vijana wa kiume msiache kushare na wapenzi wenu vipato vyenu na umpe nafasi ya yeye kutoa maoni na ushauri juu ya matumizi ya hicho mnachokipata hata kama hakupata fursa ya kuendelea na masomo na hii itakusaidia kumjua mind set yake
Sijaweka nukta unaweza kudondoka xperience yako katika hili
Bado wote hamjakua.
 
Ulitaka kutuambia kuwa na we una nyumba....
 
Ningekua sekondari nikaulizwa dhima ya mwandishi ninini, ningejibu
1. Anapata salary slip
2. Ameoa
3. Ana nyumba
4. Anapenda watu wajue
 
Ni nzuri ukipata mwanamke mwenye akili kama huyo wako
 
Back
Top Bottom