Mwanamke na nyoka ama nyoka na mwanamke vyovyote vile

Mwanamke na nyoka ama nyoka na mwanamke vyovyote vile

Chimbuvu

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2012
Posts
4,401
Reaction score
2,345
Eva alipokula tunda katika bustani ya edeni,akampatia adamu naye akala na macho yake yakafunguka akajiona yupo uchi.
Kwa miaka ya karibuni tumeshuhudia mahusiano mengi yakivunjika,yakisambaratika tatizo ni nini?je ni mti gani huo ambao eva ameona tunda lake na kulila na kumpatia adamu?

Tukiujua huo mti mapema inabidi tuukate ikiwa kama hawa hajakula tunda lake lakini kama ameshakula tunda sasa ni suala lingine.kwa nini rate ya mahusiano ama ndoa kuvunjika ni kubwa sana katika nchi zilizoendelea kuliko nchi masikini?
Kwa nchi ya marekani asilimia 80 ya ndoa huishia kuvunjika a.k.a hazidumu,kwa nini?
Je ndoa zilizopo mijini na ndoa zilizopo vijijini zipi zinazodumu?

Ni za vijijini ndio ndoa zinazodumu zaidi kuliko za mijini.
Ni tofauti gani ama gap lililopo kati ya ndoa za watu waishio mijini na vijijini?je wanawake wa vijijini ni wanyenyekevu na wanawaheshimu waume zao kuliko wanawake wa mijini?

Ama ni uoga wa wanawake wa vijijini?
Je tupo tayari kufukuzwa katika eden ya ndoa?
La hasha huu mti wa katikati tuung'oe na matunda yake tuyaharibu na tule matunda ya mti wa uzima.
Lakini huo mti ni upi?hilo tunda ni lipi? Ni elimu,teknolojia,maendeleo ama?

Je ni kweli watu wenye mafanikio wengi ndoa zao zina matatizo kuliko wanandoa wasio na mali?
Kama ni kweli basi kuna kipimo cha mafanikio hatutakiwi kukivuka? Na huyu nyoka ni nani ambaye yupo katika huu mti tumpie kichwa afe?je ni media zinazotangaza mahusiano yaliyovunjika kila siku ya wasanii?je ni wale wanaowatangazia watoto wetu wajue kutumia kondomu wakiwa shule za msingi?
Wanaume tufanye nini tusije kuulizwa kwa nini tumekula hilo tunda..........
 
Afu wewe... Kwa hasira sichangii uzi wako... U know wara am seying!!!
 
Nchi zilizoendelea ni haki sawa zinawaponza na hao unawasema wa mjini nao wakakimbilia Beijing kusaka haki sawa nani kawadanganya kwenye ndoa kuna haki sawa? biblia iligawanya majukumu...mwanaume ampende mkewe...mwanamke amtii mmewe.Tofauti na hapo hakuna amani kwenye ndoa.
 
Tunafanyaje kama wanaume maana ndio tutaitwa wa kwanza kuulizwa .

Nchi zilizoendelea ni haki sawa zinawaponza na hao unawasema wa mjini nao wakakimbilia Beijing kusaka haki sawa nani kawadanganya kwenye ndoa kuna haki sawa? biblia iligawanya majukumu...mwanaume ampende mkewe...mwanamke amtii mmewe.Tofauti na hapo hakuna amani kwenye ndoa.
 
Uzi una maswali mengi paka mtu unashindwa uanze kujibu lipi..
 
Kuanzia heading hadi habari yenyewe, sijajua Chimbuvu unataka kujadili jambo gani....
 
Last edited by a moderator:
Uzi una maswali mengi paka mtu unashindwa uanze kujibu lipi..

Anzia lolote mkuu. kwa nini ushindwe kujibu? Jibu yale uliyona ufahamu nayo na ambayo una muda wa kuyajibu...Sasa hapo umejibu nini
 
Haya ebu nijitutumue!

Kiufupi ndoa ni commitment' hivyo '' No commitment' no marriage'' sasa wengi wetu tunachukulia juu juu swala la ndoa na tunakurupuka nalo!

Na ndio maana hazidumu! Kikubwa tuweke mbele upendo' maana upendo huvumilia! Na tukumbuke makusudi ya Mungu ni kuifanya ndoa iwe ni sehem ya amani, upendo, furaha, na sehem iliyojaa vicheko! Sasa kwa ndoa nyingi zasasa imekuwa kinyume chake' watu wengi wanajutia kuoa/kuolewa!

Hapo vipi nadhani kidogo nimejaribu kujibu sehem ya maswali yako mkuu!
 
Kwa nini wanajutia kuolewa ama kuoa? Nini tatizo? Media zinavyotangaza wanawake bila wanaume wanaweza ama elimu?
 
Umegusia wanawake wa vijijini na ndoa zao . Nafikiri wanadumu kwa sababu ya hofu kwani hizo tabia walizo nazo wanaume wa vijijini hazitofautiani na wa mjini. Jamii inayowazunguka nayo ni kiwazo sababu mwanamke anajua akishindwa kuishi na mumewe basi ataaibisha familia na ukoo wake. Kwa mtazamo wangu migogoro ya kwenye ndoa inasababishwa na lack of true love. Kama watu wataamua kupendana na kuheshimiana mambo yatakua mazuri tu.

Kuhusu wenye mafanikio, baadhi yao walianzia chini sasa mambo yalipokuwa mazuri mume anaona huyo aliye naye sio type yake hivyo huanza kutoka nje kutafuta mwenye hadhi yake . Hapo ndipo migogoro huanza.
 
Kwa hiyo Ablessed mafanikio ni moja ya matatizo sasa ama?
 
Last edited by a moderator:
kuvunjika kwa ndoa kuna changiwa na mambo mengi sana, tunachotakiwa ni kumuomba Mungu atuepushe na atujalie upendo wa kweli na uvumilivu kwa wenzi wetu
 
Hahah!!! hilo kila mtu analijua

Miye nataka kujua hoja ya sredi yake maana naona kama anazunguka point hadi havieleweki...

Wakati mwingine to shoot straight at the point ni much better rather than trying to be a smart pants nakuweka maneno mengi which doesn't make sense
 
Back
Top Bottom