Furahia ujana wako mama, vilele wanavifika wenzio huko ujanani, wakifika ule umri wa makwazo makuu (ambapo tarehe zenye umuhimu zinapungua sana zinabakia za anniversary na birthdays za watoto tu), hicho kilele utakuwa unakiona kile paleeeeee lakini hukifikii hata ukivutwa na winchi! Basi unakuwa unapanda nusu kilima, unashuka. Ukijaribu tena inakuwa robo kilima, miguu inachoka, unakata tamaa unajirudia zako kwenye tambarare unajilaza na mwenzio mnasimuliana mambo yenu ya mwaka 47, na kausingizi hakoooo kanawabeba hadi ng'ambo ya pili penye ndoto murua, mara unaota umebeba kajukuu, mara unaota mwanao eti kawa profesa, nk. Alarm inalia kuashiria 'wake up' time, chumba kinageuka ofisi immediately mnaanza kuulizana ushauri kuhusu mambo ya ofisini kwenu, hayo mtaendelea nayo hadi kwenye breakfast table, kwenye gari mkielekea kazini, na mkifika ofisini kila mtu anamsahau mwenzie hadi mtakapokutana tena jioni kupeana michapo ya yaliyojiri. Kilele cha mlima? Hakuna anayeulizia. Inakuwa usiku inakuwa asubuhi, na kuendelea na kuendelea.
Panda kilima hadi miguu itakapogoma, hata kama unabaki kinywa wazi, kabla hazijaja siku za kulala bondeni.
Panda kilima hadi miguu itakapogoma, hata kama unabaki kinywa wazi, kabla hazijaja siku za kulala bondeni.