Mwanamke mwenye mtoto!

Mwanamke mwenye mtoto!

Ndugu napenda kukuambia ukweli kuwa ni aghalabu sana kukuta mwanamke mwenye mtoto akavunja mahusiano ya moja kwa moja na baba mtoto wake. Mimi binafsi nimeona mifano mingi sana, hakika sikushauri kuoa mwanamke mwenye mtoto wakati mabinti wamejaa.

Mtoto ni kiunganishi kikubwa sana kwa wazazi hao wawili hata kama si leo bali hata kesho. Siku mtoto akiwa mkubwa mwenye uwezo akaamua kumuita Baba yake kisha akamuita mama yake, je unahisi utakuwa katika hali gani? Mapenzi ya waliozaa huwa kuisha ni ngumu sana hata kama waliachana katika hali mbaya, msamaha huwa upo japo kuoana itashindikana.

Ingia ukijua kuwa kuwa unaenda kukabiliana na changamoto nyingi katika familiya mbili tofauti, nikimaanisha mtoto wa mkeo na watoto wako ambako kote mkeo atacheza kama mhusika mkuu.
 
duh wamekukatisha tamaa kabisa mkuu. anyway, wanasema wengi wape? all the best...
 
Lakini pia sio kiunganishi. Kuna waliobeba mimba ili waunganishwe na haikuwa hivyo...na haijawa.

umesema mimba. Lakin atakapozaliwa mtoto lazma waungane kwa namna yoyote ile............ Lakin hata kenge huwa haamin kama kuna hatar mpaka aone damu
 
acha zako bana ina maana ww hunaga self decision from inner part of ua heart?

Problem shared-problem solved. Kwani hapa nahitaji uamuzi au mawazo? We kazi yako kutoa hoja maamuzi ni yangu.
 
duh wamekukatisha tamaa kabisa mkuu. anyway, wanasema wengi wape? all the best...

Mkuu, sidhani kama yupo aliyeandika kwa lengo la kumkatisha tamaa, ila naamini wengi wameangalia worst possible scenario.

Changamoto ndani ya nyumba zipo, kuwe na mtoto wa nje ama kusiwepo. Ila ni lazima M.E.M.A afahamu ukweli kuhusu kuishi na mtu mwenye mtoto nje ya ndoa.

At the end of the day, it's his decision to make!!!!
 
Last edited by a moderator:
Wakuu salaam.

Husika na kichwa cha habari hapo juu, pasi na kutoa kisa kirefu naomba mnisaidie kwa kujibu swali hili: Kuna tatizo gani kuoa mwanamke aliyezaa na mwanaume mwingine, na huyo mwanaume hajafa..na mtoto pia yupo ila yupo kwa baba yake?

NB: Mwanamke anasema kwa mwanaume huyo hakuna future na sio mtu ambaye anaweza kuishi naye. Anafanya mpango wa kumchukua mwanae na ikishindikana basi atamuacha huko..akiwa mkubwa atatamtafuta. Mpaka sasa watu wa upande wa baba wa mtoto hawataki mtoto achukuliwe.

Iwe kwa mwanamke au mwanaume mfano wake ni kujiuliza:
Kuna shida kununua gari used?
 
Duh, mapenzi kitu kigumu sana....! Mwombe Mungu akusaidie kufanya maamuzi...@ M.E.MA
 
watu8 nilikuuliza swali kule jf doctor hujanijibu, thread ya blood groups


Kisa chako hakijakamilika...

Hebu tuelezee sababu za hao wazazi kutengana, walifunga ndoa kabla au lah?
 
Last edited by a moderator:
Hakuna binadamu aliyekamilika... wapo waliooa mabikra lakini hizo ndoa hazitamaniki...
 
Iwe kwa mwanamke au mwanaume mfano wake ni kujiuliza:
Kuna shida kununua gari used?

Magari sio sawa na watu. Yametengenezwa hivyo hivyo haya uwezo wa kujirekebisha wala kufikiri. Not human being. By the way used ya mbele ni mpya huku kwetu. Kuna walionunua mapya pia km0...likazama mtoni siku ya kwanza ya safari. So tusinunue magari mapya kisa yanazama mtoni!!?
 
Back
Top Bottom