mkonowapaka
JF-Expert Member
- Feb 19, 2010
- 1,493
- 767
Je, umri wa hiyo mimba ni wiki ngapi?? Kama bado ni mimba changa(below or around 12 weeks) ni kawaida kwa mjamzito kuexperience hali hiyo. Je ameshaanza clinic? Kama bado, nakushauri aanze clinic, na huko atapata msaada zaidi kuhusu hali hiyo. Mara nyingine kunakuwa na vitu vinavyosababisha hali hiyo ya kutapika kuzidi sana, kama vile mimba ya mapacha,na matatizo yanayohusiana na mimba.............
Aende hospitali afanyiwe na vipimo ikiwemo ultra sound ya hiyo mimba ili ku-rule out vitu kama ujauzito wa mapacha(multiple gestation), then daktari atamuanzishia dawa kadri inavyofaa na kwa dosage sahihi, usikubali kumuanzishia dawa tuu kienyeji, kila mgonjwa ni tofauti na daktari atatoa dawa sahihi na dozi sahihi kulingana na ugonjwa, na atamuongezea dozi au dawa au kumpunguzia kadri ya maendeleo yake yatakavyokuwa.
Nakutakia malezi mema ya ujauzito wa mkeo, umtunze na kumuangali vizuri zaidi katika kipindi hiki, ahsante sana
asante kwa ushauri mzuri na wa kitaalamu....noted!!
ni below 12 weeks,ningependa kujua kwa utaalamu wako,pale muhimbili (incase upo dsm na ni daktar wa binadamu)..naweza kuonana na daktari gani mzuri wa masuala haya ya ujauzito..ningependa apate the best treatment...ambayo naona muhimbili ndio wapo maexpert zaidi