Mjamzito anapitia changamoto hizi, je nini chanzo?

Kizibo

JF-Expert Member
Jul 3, 2018
3,871
8,381
Heshima kwenu wakuu.
Kuna mama /dada ni mjamzito. Sio ujauzito wake wa mara ya kwanza.

Anapitia changamoto hizi.

★Tumbo kuuma chini ya kitovu, linauma baadae linaachia lenyewe na kujirudia rudia.

★ Kichwa kuuma mara kwa mara.

★ Kuhisi baridi sana mara kwa mara.

★ Kuhisi kizunguzungu

Watalaamu wa afya na wakubwa (mna uzoefu) naomba kufahamu nini hasa chanzo cha haya matatizo kwa mjamzito??

Je, ni hali ya kawaida, yaani huwatokea wajawazito wengine??

Je, suluhisho ni nini??

NB: Hajaanza kliniki na hajaenda hospitali kufanyiwa check up.

ASANTENI SANA NA MBARIKIWE SANA.
 
Mimi si nwanamke lakini experience ya wife katika hizo. 75% kunakuwa na shida hasa kichwa na baridi kali. Achek afya mapema
 
1. Aende hospitali. Hakuna Daktari au mtaalamu mahiri atakupa ushauri pasipo kuonana na mgonjwa.

2. Tumbo kuumwa chini akapime UTI

3. Kichwa kuuma mara kwa mara ni aidha hana damu ya kutosha au maji mwilini.

3. Kizungu Zungu pia inatokana na upungufu wa damu au maji.

4. Kuhisi baridi ni dalili ya homa. Bado itakuwa ni UTI au malaria.

Ungeeleza mimba inamiezi mingapi?
Ni ya kwanza au yangapi?

Muhimu: asifanye chochote kienyeji pasipo maelekezo ya Daktari waliyeonana uso kwa uso na akachukua vipimo
 
Mimi sio mtaaalamu ila nina uzoefu maana nina watoto kama wote.

Tumbo kuuma na kuacha kama ni mimba changa ya chini ya wiki 12 ni kawaida lakini pia inaweza kuwa tatizo.
Kichwa kuuma mara kwa mara kizunguzungu, akapime wingi wa damu.

Mpeleke hospital mkuu inawezekana hizo dalili hazina uhusiano na ujauzito pia.
 
Heshima kwenu wakuu.
Kuna mama /dada ni mjamzito. Sio ujauzito wake wa mara ya kwanza.

Anapitia changamoto hizi.

★Tumbo kuuma chini ya kitovu, linauma baadae linaachia lenyewe na kujirudia rudia.

★ Kichwa kuuma mara kwa mara.

★ Kuhisi baridi sana mara kwa mara.

★ Kuhisi kizunguzungu

Watalaamu wa afya na wakubwa (mna uzoefu) naomba kufahamu nini hasa chanzo cha haya matatizo kwa mjamzito??

Je, ni hali ya kawaida, yaani huwatokea wajawazito wengine??

Je, suluhisho ni nini??

NB: Hajaanza kliniki na hajaenda hospitali kufanyiwa check up.

ASANTENI SANA NA MBARIKIWE SANA.
Habari!

Kwa mwanamke yeyote anaehisi au kujitambua ni mjamzito, sera ya sasa inamtaka kufika kuthibitisha au kuanza Kliniki ya Uzazi mara moja/hakuna sababu kusubiri.

Pia mama atapata elimu ya uzazi na utunzaji mzuri wa afya yake pamoja na kiumbe alichonacho. Atapata virutubisho hitajika kulingana na umri wa ujauzito. Pia , tiba mahsusi na ushauri kulingana na afya yake.

Kwa changamoto anazopitia mhusika, si rahisi kupata jibu mwafaka kulingana na kutokuwepo kwa maelezo zaidi ili kupunguza au kuongeza uwezekano wa matatizo yanayomsibu. Pia ukaguzi wa mwili/examination ni muhimu.

Haya unaweza kuyaona kwenye maelezo hapa chini:

[ ] Tumbo kuuma chini ya kitovu, linauma baadae linaachia lenyewe na kujirudia rudia.
1: Maambukizi ya UTI.

2: Shida kwenye mfumo wa chakula.

3: Nyonga kutanuka/kutegemea na umri wa ujauzito.

4: Tatizo linalohusu mimba yenyewe.


[ ] Kichwa kuuma mara kwa mara.

1: Hii inaweza kuwa inaambatana na mabadiliko ya vichocheo wakati wa ujauzito.

2: Maambukizi yoyote ya virusi, malaria au bakteria.

3: Kutokula vyema au kunywa maji ya kutosha

4: Kutokupumzika vyema

5: Upungufu wa damu

[ ] Kuhisi baridi sana mara kwa mara.

1: Maambukizi yoyote kati ya: virusi, bakteria, UTI na malaria.

[ ] Kuhisi kizunguzungu.

1: Hali ya ujauzito wenyewe.

2: Kutokula au kunywa maji ya kutosha.

3: Kutokupumzika vyema.

4: Madhira ya maambukizi hapo juu.

5: Presha yake kushuka.

6: Upungufu wa damu


Suluhisho:
Unaweza kuona mlolongo wa mchanganyiko wa matatizo hapo juu. Ila mengine yanaweza kuondoka kupitia maelezo zaidi ya mgonjwa, vipimo vya awali/vital signs, ukaguzi wa mwili na baadaye vipimo maabara. Hapo ndo umuhimu wa KUFIKA KWENYE VITUO VYA AFYA NA KUWAONA WATAALAMU WA AFYA UNAPOONEKA.

Timiza wajibu wako sasa kikamilifu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom