Mwanamke mjamzito kupata kichefuchefu na kutapika: Chanzo na tiba yake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanamke mjamzito kupata kichefuchefu na kutapika: Chanzo na tiba yake

Discussion in 'JF Doctor' started by Kahema, May 12, 2011.

 1. Kahema

  Kahema JF-Expert Member

  #1
  May 12, 2011
  Joined: May 21, 2010
  Messages: 202
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Swali No 1
  Tafadhari naombeni msaada kwa yeyote anayejua nini chanzo cha mama mjamzito kutapika na kichefuchefu kila mara.

  Kama kuna dawa please nisaidieni nijue kwani nina ndugu yangu anapata taabu sana.

  Swali No 2 kutoka kwa sijui nini

  Salaam wanaJF, mi ni mara yangu ya kwanza ndani ya jukwaa hili.

  Nina tatizo moja naombeni ushauri wenu, tunatarajia kupata mtoto wa kwanza mwezi ujao Mungu akipenda, ila tatizo linakuja mke wangu anatapika sana hqasa kipindi hiki cha miezi ya mwishoni (hapo mwanzo alikuwa poa kabisa) ila tangu alipoingia kwemye mwezi wa saba hivi akaanza kutapika.

  Ilianza kwa kudai anasikia kiungulia sana na baadae ikamletea kutapika, nilimpeleka hospital wakasema ni hali ya kawaida na wakampa dawa za kuzuia kutapika na kiungulia na kweli ile hali ikapoa ila baada ya mguda mfupi tu ikarudi tena, tukaenda tena wakampa dawa kiungulia kikaisha kabisa ila ikabaki kutapika.

  Nikimuuliza mke wangu kama ana chochote cha ziada anachojisikia kama maleria au kuumwa kitu kingine chochote anadai hamna kabisa yuko poa na hajisikii kuumwa popote ila bado anatapika, hospitali wanasema ni hali ya kawaida na inatokea ila mpaka napata wasiwasi (unajua tena ndo first born anakuja).

  Yaani anaweza kukaa nyumbani wiki moja au mbili inayofta yupo hospitali wamemlaza kumuwekea drip za maji (wakati mwengine na sindano za kuzuia kutapika) yaani hali ndo hivyo.

  Sasa kama kuna ushauri mwingine wowote please nisaidieni waungwana.

  Swali No. 3 kutoka kwa MsakaGamba

  Habari zenu mabibi na mabwana.

  Naomba msaada wenu wa hali na mali wenye michango yakinifu na yenye mashiko itakayo nisaidia kumtibu mke wangu.

  Mwenzangu kila anapo kuwa mjamzito huwa anasumbuliwa sana na kutapika, mimba ya kwanza ilikuwa balaa sana maana alianza kutapika ikiwa na mwezi mmoja na hali hiyo ikaendelea mpaka alipofikisha miezi tisa. Ilikuwa kila anacho kula hakikai anatapika kiasi kwamba ilifika wakati akawa anatundikiwa drip ya maji ambayo imechanganywa na dawa ya kuzuia kutapika na haikuwa inampa nafuu ya kudumu.

  Niliambiwa kwa sababu ni mimba ya kwanza nivumilie, nimekaa apumzike miaka 5 kwa kuwa niliigopa sana ile hali lakini pia kuweka interval nzuri kati ya mtoto wa kwanza nawa pili.

  Tumeamua tupate mtoto wa pili ila kinacho nishangaza mwezi bado niwa kwanza na ameanza tena kutapika kama kipindi akiwa na ujauzito wa kwanza! Kwa sasa kila anachokula anatapika, hii inanipa woga kuwa huenda akazoofu kama jinsi alivyo kuwa kwenye mimba ya kwanza.

  Wabobezi na wataalamu wa haya maswala naombeni msaada wenu. Miaka 5 iliyo pita sikuwa memba humu. Hivyo naomba jf dokta iwe msaada kwangu katika kipindi hiki kigumu kwangu.

  Naomba watakao changia wawe ambao wako tayari kunisaidia kwa ushauri/dawa au matibabu. SITAKI DHIHAKA TAFADHARI.

  Swali No 4 gidytitus - Mjamzito kutapika baada ya tendo la ndoa

  Wataalam wa afya na wale wakongwe waliomo kwenye ndoa kwa muda mrefu naombeni ushauri wa kitaalam na kiuzoefu!

  Mke wangu anatapika mara nyingi baada ya tendo la ndoa hasa pale anapokuwa na amefikia mshindo (Kileleni) au kumaliza.

  Hali hii imeanza kumtokea akiwa na ujauzito wa miezi 5, na kwa kuwa sisi ni wageni katika hii taasisi ya ndoa tumekuwa na hofu na mara nyingine kudhani kuwa ni disorders za preg but kwa kweli inatupa hofu na mara nyingine hata kuogopa kufurahia tuzo yetu tulopewa na mwenyezi Mungu.

  Tunaomba ushauri, Je kuna madhara yanayoambatana na kutapika huku?

  Asanteni.

  Mchango,Maoni ya WanaJF

   
 2. Visenti

  Visenti JF-Expert Member

  #2
  May 12, 2011
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 1,031
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 133
  Hutokana na mabadiliko ya mlingano/uwiano wa vichocheo (hormones) wakati wa ujauzito, kuna baadhi ya vichocheo vinapanda kwa kiasi kikubwa na kusababisha kichefuchefu na kutapika.

  Dawa za kuzuia kutapika zilizo nyingi huleta usingizi na kulegea mwili, lakini kunabaadhi cheche hazina tabia hiyo, kwa mfano dawa inaitwa NOZICK, ni vema ukakurana na dakitari bingwa wa akina mama i.e OBSTETRICIAN.
   
 3. Kahema

  Kahema JF-Expert Member

  #3
  May 12, 2011
  Joined: May 21, 2010
  Messages: 202
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Asante ndugu yangu, mwanzo mzuri.
   
 4. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #4
  May 12, 2011
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Chanzo cha mama mja mzito kutapika au kujihisi kutapika (kichefuchefu) ni mabadiliko ya mfumo wa hormone mwilini mwa mwanamke anapopata ujauzito.

  Mzunguko wa mwezi wa mwanamke unatawaliwa na hormones (follicle stimulating hormone, lutenizing hormone, estrogen na progesterone) ambazo levels zake kwenye damu zinbadilika kutokana na kipindi cha mzunguko.

  Lakini pindi anapopata mimba kunakuwa na mabadiliko ya baadhi ya hizi hormones (zinapungua sana kiasi chake kwenye damu au kupotea kabisa), na hormone inaitwa human chorionic gonadotropin inakuwa kwa kiasi kikubwa kwenye damu na kuchochea hali hiyo.

  Haya mabadiliko huwa yanatokea miezi miwili hadi mitatu ya kwanza ya ujauzito, na ndio katika kipindi hicho mwanamke mwenye ujauzito anajisikia kichefuchefu, kutapika na mabadiliko mengine mfano kukosa usingizi, kula sana au kutokula, hamu ya kula vitu kama udongo etc.

  Kama anatapika sana kiasi cha kuhatarisha kupoteza maji na/au madini mwilini (hyperemesis gravidarum) basi mgonjwa atahitaji sindano za kuzuia kutapika (antiemetic) na/au drip za kuongeza maji.
   
 5. Kahema

  Kahema JF-Expert Member

  #5
  May 12, 2011
  Joined: May 21, 2010
  Messages: 202
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  thanks man. good advice.
   
 6. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #6
  May 12, 2011
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,073
  Likes Received: 1,806
  Trophy Points: 280
  Good explanation man!
   
 7. sijui nini

  sijui nini JF-Expert Member

  #7
  Nov 25, 2011
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 2,382
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  Salaam wanaJF, mi ni mara yangu ya kwanza ndani ya jukwaa hili.

  Nina tatizo moja naombeni ushauri wenu, tunatarajia kupata mtoto wa kwanza mwezi ujao Mungu akipenda, ila tatizo linakuja mke wangu anatapika sana hqasa kipindi hiki cha miezi ya mwishoni (hapo mwanzo alikuwa poa kabisa) ila tangu alipoingia kwemye mwezi wa saba hivi akaanza kutapika.

  Ilianza kwa kudai anasikia kiungulia sana na baadae ikamletea kutapika, nilimpeleka hospital wakasema ni hali ya kawaida na wakampa dawa za kuzuia kutapika na kiungulia na kweli ile hali ikapoa ila baada ya mguda mfupi tu ikarudi tena, tukaenda tena wakampa dawa kiungulia kikaisha kabisa ila ikabaki kutapika.

  Nikimuuliza mke wangu kama ana chochote cha ziada anachojisikia kama maleria au kuumwa kitu kingine chochote anadai hamna kabisa yuko poa na hajisikii kuumwa popote ila bado anatapika, hospitali wanasema ni hali ya kawaida na inatokea ila mpaka napata wasiwasi (unajua tena ndo first born anakuja).

  Yaani anaweza kukaa nyumbani wiki moja au mbili inayofta yupo hospitali wamemlaza kumuwekea drip za maji (wakati mwengine na sindano za kuzuia kutapika) yaani hali ndo hivyo.

  Sasa kama kuna ushauri mwingine wowote please nisaidieni waungwana.
   
 8. o

  omholo Member

  #8
  Nov 25, 2011
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa kweli dawa ya kutibu kuacha kutabikakwa mjamzito ni ngumu kwa sabababu ni mabadiriko ya hormone kwenye mwili,cha msingi hospitali wakupe dawa za kuzuia kutapika,atumie machungwa,akitapika sana nenda waongeze drip,vinginevyo ni kwa miujiza ya Mungu.
   
 9. daughter

  daughter JF-Expert Member

  #9
  Nov 25, 2011
  Joined: Jun 22, 2009
  Messages: 1,274
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Lakini umeenda kwa wataalamu wa masuala ya uzazi au ni hospitali tu ili mradi? Najua kutapika huwa ni kawaida lakini hadi kufikia ilo la kuwekewa drip,..
   
 10. sijui nini

  sijui nini JF-Expert Member

  #10
  Nov 25, 2011
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 2,382
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  Tumejaribu kwenda hospitali za serikali na sasa tumeamua kwenda za binafsi pia..zote wanasema ni hali ya kawaida tu na wamempima wanasema hawaoni tatizo lolote na isitoshe wanasema dogo(mtoto) yuko poa kabisa na wameshapiga mapa tarehe inayowezekana akajifungua kutokana na hali ya mtoto ...ila hata mimi huku kutapika huku..!?? lah..:A S-confused1:
   
 11. o

  omholo Member

  #11
  Nov 25, 2011
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dada walichokuambia ni ukweli kabisa ni mambo ya kawaida ukiwa mjamzito acha mawazo jitahidi kunywa maji,juice, na kula vyakutosha wakati unapoacha kutapika kurudisha maji na madini unayopoteza ukitapika.
   
 12. sijui nini

  sijui nini JF-Expert Member

  #12
  Nov 25, 2011
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 2,382
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  Asante...ila nikurekebishe kidogo am not she!! otherwise thanks na nitajaribu kumshauri hivyo..
   
 13. o

  omholo Member

  #13
  Nov 25, 2011
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hakuna shida ujumbe niliuelekeza kwa mhusika ndo maana nikasema she,hata hivyo wewe na yeye ni mwili mmoja mnaweza tumia she/he kwa pamoja maadam hakuna madhara.
   
 14. Mganga wa Jadi

  Mganga wa Jadi JF-Expert Member

  #14
  Nov 25, 2011
  Joined: Mar 12, 2008
  Messages: 278
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kwa kawaida kutapika hotokea sana miezi minne ya mwanzo, na baadaye huenda kunapungua kadri mimba inavyokua. Kama umeanza kutapika miezi ya mwishoni ni vizuri kwenda kwa wataalamu waliobobea kwenye magonjwa ya kina mama na uzazi utasaidiwa.
   
 15. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #15
  Nov 25, 2011
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Pole kaka ila ni jambo la kawaida kwani kila mimba inapotunga huwa na vibwanga vyake wengine wanakuwa wako powa hawana shida huwaoni wakitapika wala kutematema mate ama kuchagua vyakula, wengine ni kulala hasira sizizo kuwa na kichwa wala miguu, wengine jambo kidogo tu ni kulia utafikiri kafiwa.

  Wengine kutapika mwanzo hadi mwisho anapojifungua na wengine miezi ya mwisho hutapika sana na kuchangua vyakula kama ndio kwanza mimba imetunga,ama wengine ni bedi resti mwanzo mwisho hivyo hiyo ya wifi yetu ni jambo la kawaida usiwe na wasiwasi huwa inatokea cha kumsisitiza ale vizuri na ikitokea kuna vitu anavyovimenda avile kwa wingi maji mengi ni mihimu na matunda kwa wingi.

  Ikiwa mtakuwa na wasiwasi na hicho kijacho cha mwanzo ni vizuri mkaenda kwa madaktari bingwa wa kinamama watawasaidia, ila kwa upande wangu ni kawaida sana kwenye hiyo hali, wapo marafiki zangu wakaribu waliokuwa na hiyo hali.
   
 16. sijui nini

  sijui nini JF-Expert Member

  #16
  Nov 25, 2011
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 2,382
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  Asante mkuu..nitafanya hivyo!!
   
 17. rasmanyara

  rasmanyara Senior Member

  #17
  Jan 5, 2012
  Joined: Sep 12, 2011
  Messages: 198
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Habari za majukumu wana Jf. Nina rafiki yang ana Ujauzito wa Miezi miwili inaelekea mitatu,tatizo lake ni kwamba huwa anatapika kila wakati anapokula au kunywa maji. Hali hiyo amekua nayo baada ya wiki kama kupita tokea apate huo ujauzito.

  Mwenye kufahamu suluhisho au ushauri wa kupunguza tatizo hilo naomba msaada.
   
 18. DAWA YA SIKIO

  DAWA YA SIKIO JF-Expert Member

  #18
  Jan 5, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 985
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Hii ni kawaida hasa katika miezi mitatu ya mwanzo, na hasa kwa mimba za kwanza. Hali hii huitwa morning sickness. Lakini inapozidi sana kiasi cha kuchosha itahitaji msaada wa daktari,hali hii huitwa hyperemisis gravidarum.
  So kama ni serious hadi kutapika kila kitu na kila wakati mjamzito apelekwe kituo cha tiba haraka !
   
 19. Mtalingolo

  Mtalingolo JF-Expert Member

  #19
  Jan 6, 2012
  Joined: Aug 4, 2011
  Messages: 2,188
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Lakn kwann utolee mfano mwenzako wakati muhanga niwewe mwenyewe? Haya fuata ushaur huo hapo juu.
   
 20. n

  ngwana ongwa doi Member

  #20
  Jan 6, 2012
  Joined: Dec 26, 2011
  Messages: 75
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kuongezea hapo ajitahidi kunywa maji ya kutosha,kutumia dawa za kuzuia kutapika,kula chakula kidogokidogo badala ya kula chakula kingi kwa wakati mmoja.
   
Loading...