Watu8
Platinum Member
- Feb 19, 2010
- 70,953
- 93,931
Habari yako,
Pole kwa kadhia za ujauzito zinazokukuta na bila shaka hiyo ni mimba yako ya kwanza.
Kwa kawaida kabla hata ya kupata ujauzito ulipaswa kupata elimu ya uzazi na kuelekezwa mambo kadha wa kadha.
Kinachokutokea sio tatizo bali ni hali ya kawaida kwa mwanamke yoyote na hali hiyo itapungua kwa kadiri mimba itavyokuwa ikikua.
Kutokana na mabadiliko ya vichocheo mwilini, wanawake wengi huwa wanapata hali ya kichefuchefu, matiti kuwa mazito na wakati mwingine huuma yanapobonyezwa, miguu kukosa nguvu na dalili lukuki wakati wa trimester ya kwanza 'miezi mitatu ya mwanzo ya ujauzito'.
Unachotakiwa kufanya ni kufika kituo cha afya au kliniki upate kuonana na madaktari na kuwaeleza hali yako, utapewa huduma stahiki.
Kwa sasa jitahidi ule vizuri, ulale muda mrefu na fanya mazoezi mepesi ya viungo.