Mwanamke Mjamzito Afanyiwa Ukatili wa Kutisha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanamke Mjamzito Afanyiwa Ukatili wa Kutisha

Discussion in 'Matangazo madogo' started by MziziMkavu, Dec 11, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Dec 11, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,614
  Trophy Points: 280
  Mwanamke Mjamzito Afanyiwa Ukatili wa Kutisha
  [​IMG]
  Veronica Deramous mwanamke anayetuhumiwa kulipasua tumbo la mwanamke mjamzito kwa nia ya kuiba mtoto wake Thursday, December 10, 2009 2:35 AM
  Mwanamke mmoja wa nchini Marekani ambaye alikuwa na ndoto ya kupata mtoto, amefunguliwa mashtaka ya kujaribu kuua baada ya kulipasua kwa kutumia kisu tumbo la mwanamke mjamzito akiwa na nia ya kuiba kichanga kilichokuwa tumboni mwake. Mwanamke mwenye umri wa miaka 40 aliyetambulishwa kwa jina la Veronica Deramous mkazi wa Maryland, Marekani aliwatangazia familia yake pamoja na mpenzi wake kuwa ana mimba na anatarajia mtoto hivi karibuni.

  Lakini ukweli ni kuwa Veronica hakuwa na mimba na alitiwa mbaroni akikabiliwa na mashtaka ya kujaribu kuua baada ya kulipasua tumbo la mwanamke mjamzito ili amuibie kichanga chake kilichokuwa tumboni.

  Taarifa ya polisi ilisema kuwa Veronica alitengeneza urafiki na mwanamke mjamzito aliyekuwa hana makazi akilala mitaani akimlaghai kuwa atampa makazi kwenye nyumba yake na atampa vyakula na nguo bure.

  Lakini mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 29 alipoingia nyumbani kwa Veronica, alifungwa mikono yake na kuwekwa mateka kwa siku tano.

  Taarifa ya polisi iliendelea kusema kuwa Veronica alijaribu kulipasua tumbo la mwanamke huyo ili kukiiba kichanga chake kilichokuwa tumboni.

  Hata hivyo mwanamke huyo alifanikiwa kutoroka kabla ya Veronica hajakamilisha azma yake baada ya Veronica kupitiwa na usingizi.

  Mwanamke huyo aliokolewa na polisi waliomkuta kwenye maegesho ya gari ya nyumba hiyo huku akivuja damu kwa wingi.

  Aliwahishwa hospitali ambako ilibidi azalishwe kwa njia ya upasuaji na mtoto wake wa kike alizaliwa salama akiwa na afya njema na ameamua kumpa jina la "Miujiza".

  Veronica anashikiliwa na polisi akikabiliwa na mashtaka ya kujaribu kuua na utekaji.

  http://nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsId=3716222&&Cat=2
   
 2. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #2
  Dec 14, 2009
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,793
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  ... Inashangaza sana kwamba bado katika dunia hii hii kuna wengine wanatupa jalalani ama ****** watoto wanaowazaa!!
   
 3. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #3
  Dec 16, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Very bad.........wasiwasi wangu ni kuwa Bongo tutaiga as soon as possible
   
Loading...