mwengeso
JF-Expert Member
- Nov 27, 2014
- 9,227
- 6,666
Nimesoma makala yenye kichwa cha habari hapo juu katika gazeti la 'Nipashe Jumapili Julai 17, 2016' iliyoandikwa na Mwanahabari 'Mary Geofrey'.
Mwandishi naamini amewakilisha mtazamo, hisia na matarajio ya wanawake wengi. Kama ni hivyo basi, katika mwono, mawazo na maswali mengi, je, hili halipingani na hitaji la wanawake la usawa kwa kila jambo isipokuwa maumbile!
Baadhi ya hoja zake kuhusu matunzo nanukuu:
1) Kuna baadhi ya wanaume ni wabahili sana, yaani kutoa fedha kwa wapenzi wao wanaona shida, wengine wanatoa lakini shingo upande.
2) Baadhi wanatoa visingizio kwamba kumpa pesa mwanamke kwa ajili ya kujikimu na kununulia mavazi ni sawa na kupoteza.
3) Siyo lazima mwanamke akuambie naomba kitu fulani, ni jukumu lako kufahamu aina ya vitu anavyopenda na unapaswa kumnunulia nk.
Anahitimisha na "kama hautoi matunzo kwa mpenzi wako basi jua umemuruhusu atoke nje ili apate kile anachotaka". Hili linakumbusha sakata lilijitokeza, katika kikao cha bunge kilichokwisha, pale Mbunge mmoja alipowaambia wabunge wanawake ni baadhi ya "babies" za watu kupata ubunge.
Mh wanajammvi, hilo nalo WAZO!