Bondpost
JF-Expert Member
- Oct 16, 2011
- 6,647
- 9,473
Ndugu zangu wanaJF, jamii imekuwa na unyanyapaa wa aina ya kipekee dhidi ya wanawake au wanaume wasio na uwezo wa kupata mtoto. Wamekuwa wanyonge na hata imekuwa tishio katika kudumu ndoa zao. Jamii imechukulia kila binadamu anazaa na asipoweza basi anaonekana kama hafai.
Najiuliza swali, kwani mwanamke kutokuwa na uwezo wa kuzaa inamfanya asiwe mwanamke? Je kuzaa pekee ndio uanamke?
Nimejaribu kuangalia nimegundua wanawake wengi ndio wa kwanza kuwanyanyapaa wale wasio na uwezo wa kupa a mtoto, kwa mfano, madada, mama yako mzazi, hata bibi wa mwanaume aliyeoa mwanamke mwenye matatizo ya uzazi.
Tumekuwa tunawaweka katika kundi la jinsia tofauti na wanawake wengine wakati kila kitu ni mwanamke just kutokuzaa. Nikajiuliza sana kwa nini mtu hajapata mtoto kwa miaka kadhaa anatengwa wakati nae anatamani mtoto ila uwezo hana, ila akipata ndio wanajamii wanajikomba kwake!
Ndugu zangu, mwanamke kutokuzaa haimfanyi yeye kutokuwa mwanamka kwani hata wale wenye uwezo wa kuzaa sio wote ni wakamilifu kwa kila sekta ya uanamke.
Nawasilisha hoja, nawaombeni tuchangie kwa ustaarabu.